Bajeti ya Kenya ni Tsh. Trilioni 78, Tanzania ni Tsh. Trilioni 34 na Uganda Tsh. Trilioni 30

Porojo hizo.. angalia kenya wanakusanya kodi kiasi gani?
Bajeti kubwa haiimaanishi kwamba ndio inaleta maendeleo. Kenya wanabandika manamba makubwa kwa sababu kwa sehemu kubwa wanatumia Expenditure-Driven budget yaani sehemu kubwa wanapanga bajeti kwa ajili ya matumizi zaidi kuliko maendeleo na kulipa madeni pia. Mpaka ninapoandika hapa Kenya inakopa zaidi ya nchi zote ukimjulisha kwa pamoja hapa Afrika mashariki ili kujazilishia bajeti yao...
 
Umesahau kuonesha kuwa sisi Tanzania wenye bajeti kidogo ndiyo tunaongoza kwa Population ya watu dhidi ya Kenya yenye bajeti kubwa!! Aisee!! Hapa Sayansi inagoma kabisa.
 
Magufuli alikua anajenga kiti cha afya kwa mil 500 hizo hizo.
Watu wanajenga fensi nyumba ya Mtumishi 1 kwa 500m/- mtaendelea wapi?. Baneni matumizi Fedha ziende kwenye maendelea ya walio wengi. Tuna chuma, Gesi, mafuta, Dhahabu, mbuga, maji nk serikali iwekeze hapo iachane na vikodi vidogo2 kwa wananchi wachovu. Kwenye akili wawekwe sehemu wavumbue vitu, Masomo ya ufundi 80% vitendo na 20% theo vifundishwe. Walisoma sayansi na kudeliver ktk Kazi zao walipwe vizuri nk. Bila hivo tutakalia "ukitaka kula lazima nawe uliwe"
 
Uzalishaji ni Mdogo Sana Tanzania,masoko yamejaa tele huko duniani, ardhi tele,maji tele yanamwagika tu ziwani baharini bure badala ya mashambani.
Zao moja kwa parachichi yaani KILA mtu alime tza na soko hatuwezi lijaza la china.
Sera za nchi mbovu kama hadi karne hii matajiri mnawaita mabebari na mnataka waishi kama mashetani unategemea nini? tunahitaji matajiri waje wawekeze kwenye viwanda na vitoe ajira
 
Bila shaka hapa kwetu kama tunata kuwa na bajeti kubwa ni lazima tufanye kazi kwa bidii na maarifs,tusiwe waoga kuthubutu na kisha tulipe kodi hakika tutawazidi kenya
 
Miaka 36 baada ya mwalimu kung'atuka, wakipitita marais 5, bado unalia lia na Nyerere? Hii sasa ndio mindset ya zama za ujima. Kutafuta wa kumlaumu isipokuwa wewe mwenyewe.

Nyerere ana share yake ya makosa na alilisema na kulikubali. Ila kumlaumu baada ya kuwa na nafasi ya miaka 36 na marais 5 ni upumbavu mkubwa!
Umeona, ujamaa tumeuishi miaka 23, baada ya hapo tukaja na issue ya privatization aka ubepari kwa miaka 36 bado hatuja break through, means mwinyi 10 (ubepari), mkapa(10) ubepari, kikwete(10) ubepari, Magufuli(6 ) ubepari, Samia(4 )ubepari, lakini bado hatuna maendeleo, shida iko wapi?
 
Kinacho tuponza sisi waTz ni falsafa ya kijamaa. Ambayo chama tawala kimeikumbatia falsafa hii kwa nchi za kiafrika inanufaisha watawala wa nchi.
Nchi ya kenya hakuna ujamaa ukishwa kupambana na Maisha yako no One care about you, inawafanya wanapiga sana kazi kwa bidii na kuwa na ubunifu mwingi
 
Utaifishaji wa magufuli haukuwa ubepari bali ujamaa. Kupiga vita matajiri, kazi za ujenzi kuwapa suma jkt au tba hizo ni sera za ujamaa huyo hakuamini ubepari kabisa
 
Utaifishaji wa magufuli haukuwa ubepari bali ujamaa. Kupiga vita matajiri, kazi za ujenzi kuwapa suma jkt au tba hizo ni sera za ujamaa huyo hakuamini ubepari kabisa
Lakini Magufuli huyo huyo kapokea nchi ikiwa na budget ya trillion 22 mwaka 2015 na kaipeleka hadi trillion 29 mwaka 2016na baadae trillion 34.8 mwaka 2020, mbona speed yake ni kubwa kuliko hata hao waliomtangulia? shida yetu kubwa hatujui tatizo wala hatuna Muelekeo hivyo hatuwezi kufikia malengo wala sio ujamaa wala sio ubepari.
 
Lakini Magufuli huyo huyo kapokea nchi ikiwa na budget ya trillion 23 mwaka 2015 na kaipeleka hadi trillion 27 mwaka 2016na baadae trillion 33 mwaka 2020, mbona speed yake ni kubwa kuliko hata hao waliomtangulia? shida yetu kubwa hatujui tatizo wala hatuna Muelekeo hivyo hatuwezi kufikia malengo wala sio ujamaa wala sio ubepari.
Ndugu hicho siyo kigezo cha kiuchumi kuongezeka tarakimu ni uwezo na nchi kujiendesha yenyewe kwenye bajeti yake sisi bajeti yetu ni tegemezi
 
Duh unatia kinyaa kila mada lazima uitaje CHADEMA.Hii mada ni fikirishi kweli kweli kama waTanzania lazima tujiulize tunakwama wapi ?.

Investment! Investment!Investment! Investment!Investment! Investment!
 
Sera ya chadema ni ubepari wenye kuamini uwekezaji wa mitaji,technogia, ubunifu wa sayansi na technologia na ukuzwaji wa sekta binafsi kama ingini ya uchumi , ccm wanaamini nini?

ubepari utauweza? kama tu hii nusu ujamaa wa ccm mnalalamika ivi vp makampuni yakija na kupanga bei wanazotaka bila kujali maskini wenggine, mtaweza????? kenya GB 1 NI 10,000 ya tanzania na mashirika mengine yameshauliwa na competition imebaki safaricom tu tafauti na uku tanzania serikali inabalance!
 
Umeona, ujamaa tumeuishi miaka 23, baada ya hapo tukaja na issue ya privatization aka ubepari kwa miaka 36 bado hatuja break through, means mwinyi 10 (ubepari), mkapa(10) ubepari, kikwete(10) ubepari, Magufuli(6 ) ubepari, Samia(4 )ubepari, lakini bado hatuna maendeleo, shida iko wapi?

shida ni sisi wenyewe, kwa namna moja ama ingine hii mentality ya ajira imetamalaki sana tafauti na wenzetu, cha ajabu wanataka ubepari
 
Kinacho tuponza sisi waTz ni falsafa ya kijamaa. Ambayo chama tawala kimeikumbatia falsafa hii kwa nchi za kiafrika inanufaisha watawala wa nchi.
Nchi ya kenya hakuna ujamaa ukishwa kupambana na Maisha yako no One care about you, inawafanya wanapiga sana kazi kwa bidii na kuwa na ubunifu mwingi

sasa kama uku ukiongeza tu bei ya bidhaa utaskia lawama kwamba kuna mwananchi maskini kijijini huo ubepari mtauwezaaaaa?
 
Back
Top Bottom