Bajeti ya CCM imepita Ijumaa ya wananchi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya CCM imepita Ijumaa ya wananchi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Jun 24, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mengi yamesemwa kuhusu bajeti ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2012/13.
  Hivyo kwa wale wafuatailiaji na hata wale ambao hawafuatilii kila mmoja ameshudia mijadala kila kona ya nchi.Upande mmoja tulianza kwa kusikia wengi wakilalama kuwa imeenda kinyume na matarajio na hata makubaliano kuhusu kiasi cha kutengwa kwa ajili ya fedha za maendeleo. Ikafuata wale waliojinasibu kuwa wachumi daraja la kwanza ambao walikuja na dhana mpya na hata kufika mahali pa kuanzisha darasa la ‘public finance' bungeni na kwenye vyombo vya habari. Kwa mambo yalivyokwenda haihitaji masters ya uchumi daraja la kwanza kuona kuwa mambo hayako sawa – na kuwa jitihada zilizotumika siyo za kawaida na lazima kipo kisichowazi.

  1. Siamini kuwa darasa lile lilokuja baadaye pamoja na tafsiri mpya za dhana na mifumo mbalimbali ya uchumi na bajeti kuwa kipi kiwekwe wapi yalizungumzwa na kamati kabla ya bajeti kuwasilishwa.

  2. Ni ukweli usiofichika kuwa ndiyo bajeti ya CCM IMEPITA Ijumaa lakini bado hatukupewa maelezo ya kutosha juu ya:

  · Kuongezeka kwa deni la taifa
  · Kutopelekwa kiasi kikubwa cha fedha zilizoidhinishwa na bajeti ya 2011/12 mawizarani na halmashauri
  · Kwa nini serikali ilikiuka ahadi yao ya kutenga kiasi kisichopungua 35% ya fedha ya ndani kwenda bajeti ya maendeleo.
  · Mkakati wenye mshiko wa kupunguza hali ya maisha ya mwananchi wa Tanzania

  Katika kutaka kujaribu kuwapoza wabunge na wananchi tumeona baadhi ya mbinu za kuwarubuni kwa kuridhia baadhi ya vitu kama kufuta kodi ya bodaboda huku tukiacha maswali ya msingi bila kujibiwa.

  Utaratibu wa Ijumaa wa kupitisha bajeti umetusaidia mambo mawili – moja kujua nani yuko wapi( mfano mbunge wangu alisema ndiyooooo!) na pili vifijo na nderemo za CCM, CCM zilitukumbusha kuwa hii iliyopita ni bajeti ya CCM sasa sisi tuliwatuma bungeni tunawauliza BAJETI YA WANANCHI TUITEGEMEE LINI?
   
Loading...