bajeti ya afya 2012/13 na mgomo endelevu wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

bajeti ya afya 2012/13 na mgomo endelevu wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uda, Jun 26, 2012.

 1. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  watanzania tuwe makini kidogo na mwenendo wa serikali yetu!
  Ni muhimu kukumbuka na kuikumbusha serikali iliyopo madarakani kuwa inawajibika kwa wananchi na pia maamuzi ya mwisho ya jinsi gani ya kugawanya rasilimali za taifa ni ya mwananchi.

  Mwezi wa kuminambili mwaka jana tulianza kushuhudia mgogoro kati ya serikali na madaktari,mgogoro ambao ni mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu hasa katika sekta ya afya.nilitegemea kuwa serikali,vyombo vya usalama,bunge na wananchi wangeweza kujifunza kutoka katika mgogoro huu lakini sivyo.

  Naomba nijikite kwa serikali na wabunge!

  Nilitarajia baada ya migomo miwili serikali ya ccm itakuwa imejifunza jambo muhimu kuhusiana na sekta ya afya,kwamba imesahaulika na haijakidhi viwango vya kichama,kitaifa na kimataifa.kwa mantiki hii nilitarajia serikali ingeanza kuonyesha kwa dhati kuwa kuanzia bajeti ya mwaka huu utekelezaji madai muhimu yaliyotajwa na wafanyakazi wa afya ungepewa kipau mbele lakini sivyo!madaktari wamewahi kutuambia kuwa kiwango cha bajeti ya afya kilikubaliwa kuwa 15% ya bajeti yote ya serikali,haya ni makubaliano ya abuja ambayo Tanzania iliyaridhia.mwaka huu wa fedha bajeti ya afya imeshuka kulinganisha na mwaka wa fedha unaoishia.
  Moja ya madai ya madaktari katika mgimo wao ni ukosefu wa dawa na vifaa tiba.kwa bahati mbaya bajeti ya mwaka huu imepunguza kiwango cha fedha iliyotengwa kununulia madawa(kama huamini subiri bajeti ya afya isomwe ujionee)
  mifano hii michache inaonyesha kuwa waandaaji wa bajeti hawakuzingatia madai ya madaktari na malalamiko ya wananchi(ukosefu wa dawa hospitalini),hii ni dharau kwa wadau wa sekta ya afya na wenyenchi kwa ujumla.huu ni uhuni!

  Niende kwa wabunge

  bunge lilishtushwa sana na mgomo wa madaktari uliopita na kuamua kuituma kamati ya bunge ya huduma za jamii kwenda kukutana na pande zote zilizohusika pamoja na wagonjwa.naamini kamati hiyo ilitumia fedha na ilipata ripoti ya chanzo cha mgomo na pia ilielekeza nini kifanyike.je ripoti hiyo ilifanyiwa kazi?je ripoti hii ilitumika katika kuandaa bajeti ya afya ya 2012/13?jibu sina!
  Hivi wabunge wetu wamewahi kuuliza kuhusu kazi hii maalum ya kamati ?au kwa kuwa madaktari walikubali kurudi mezani ,vyombo vya habari vikawa kimya na wananchi wakatulia tukaona mambo yameisha'upepo umetulia'


  Nachelea kusema serikali haina nia ya dhati ya kutatua migogoro ya wafanyakazi au wananchi na sasa wamekutana na watu wasioamini katika usanii(madaktari).
  Je ni nani wa kuisaidia/kuifunda serikali hii?jibu unalo mwananchi na mbunge kataa bajeti mbovu ya afya ya mwaka 2012/13.

  Nawasilisha
   
 2. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  eti posho ya wabunge imeongezwa ili ifanane na wale wa EAC.
  Kwa nini maslahi ya madaktari yasifanane na yale ya EAC?
   
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  serikali dhaifu fikra zake ni dhaifu
   
 4. vimon

  vimon Senior Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  serikali ya wapuuzi.
   
 5. e

  ellyjr8 Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.

  Leo ningependa turudi jamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza ya mada hii, nilijaribu kuainisha madai yetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu "SIKIVU" ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kama hukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe macho KIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leo nilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.


  HALI HALISI HOSPITALINI:


  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke, Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatari kwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO( KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZA UDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..

  Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishahara tu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali, tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
  1. Madai ya madaktari yalianza lini?
  2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
  3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia posho mpya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
  4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwa katika bajeti?
  5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??  SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WA TRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YA MSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZI KUJIONGEZEA(during the same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NA KULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!

  Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idara wamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza 23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katika hospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu ni kushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!  VYOMBO VYA HABARI:


  Katika "episode" mbili za "series" yetu hii ya Mgomo wa Madaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi pale watu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!

  Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajui au wanapuuzia?
  Halafu mnatuita madaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzania wanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtu hauwekwi rehani lakini hatukuingia katika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndio maana muda wa mazungumzo ulikuwepo na hata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikali ikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basi ijipange kuhudumia wananchi.
  Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya pale Star TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali ni haya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kama tungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), na kwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?


  MKAKATI:

  Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili

  1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?

  2. Wanatumia pesa ya nani?

  3. Last ‘episode" walileta wanajeshi,

  KAMA MADAI YA MADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKO SAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??

  KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZI MNAYYOIITA KAZI YA WITO????  MAKOLIGI (colleague)??

  Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afya zao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakosea kidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali "sikivu", hivyo lawama, maombi, na hisia zote pelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time si kwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKE VIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.

  Najua wanasema when you get in a fight you should dig, two graves but I guess you should not fight with someone who has NOTHING to loose,.. We either overestimated the power of Government's responsibility or They(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stop us.. you cant stop what you cant catch, because the more they will push us the worse this is going to get…

  ..Solidarity forever..
   
Loading...