Bajeti ya 2021 ni ya matajiri tu. Wananchi wa kipato cha kawaida jipozeni kwenye kubet tu,haina maslahi kwenu

2019

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,982
4,457
Alieona sehemu mwananchi wa kawaida kuguswa na bajeti ya mwaka 2021 alete hapa na sisi tuone.
Boda boda kupunguziwa adhabu toka 30k mpaka 10k, kumbuka wenye pikipiki wengi ni mabosi,vijana wanapeleka hesabu tu,hapo kijana kafaidika nini?

Sehemu pekee yenye watu wa hali zote ni kubet. Waziri kapunguza kodi toka 20% kwenye zawadi mpaka 15% je ana hamasisha uchezaji kamari? Kuna hasara gani mtu akiacha kucheza kamari?

Makato ya 100 kwenda juu kwenye ununuzi wa vicha na miamala kupitia simu. Mwananchi wa kawaida anafaidika na nini hapa? Umemuongezea mzigo au umempunguzia?

Ongezeko la asilimia 30 kwenye pombe kali na bia,je watu wakinywa gongo mtawakamata? Hapa pesa ya kununua bia tena. Mwananchi wa kawaida umempunguzia nini?

Toka Magufuli aingie madarakani ni mwaka gani umeona bia imepanda? Je hii ni hujuma au makusudi au mtego kwa Mwigulu kushindwa hii wizara?

Kweli tumepata rais mpole, mwenye utu na mama anaejali,lakini bila kufikiria maisha ya watu wote huo upole una maana kweli?

Kumbukeni Mwenye nacho atazidi kuongezewa.
 
Kusema ukweli hii bajeti ni ya hovyo kuwahi kutokea. Imeandaliwa kwa lengo moja tu kuu; kuwanyoosha WANYONGE wa Magufuli.

Kwa aina hii ya bajeti, nitashangaa sana kuona baadhi ya Watanzania wakiendeleza ngojera zao za kuifagilia ccm! Ccm haina msaada kwa Watanzania walio wengi! Isipokuwa tu kikundi chao cha watu wachache.
 
Mkuu kwenye bia umepotosha nachojua Mimi Ni kwamba Kodi imepungua kiasi kwamba bia ya 1500 Sasa HV itauzwa 1000
Umeisoma lakini au umeadisiwa? Kama kuna ongezeko la asilimia 30 hapo ni kupungua au kuongezeka? JF wameipost huku naweza kukuletea na wewe ulete yako
 
Umeisoma lakini au umeadisiwa? Kama kuna ongezeko la asilimia 30 hapo ni kupungua au kuongezeka? JF wameipost huku naweza kukuletea na wewe ulete yako
Usipotoshe,

Bia inayozalishwa ndani, imepunguzwa Kodi.

Bia na vilevi vingine vinavyoingizwa kutoka nje, Kodi imepanda
 
Mtoa mada unacholalamika hakina mashiko.

Faini ya elfu 10 badala ya elfu 30,
inamsaidia zaidi bodaboda maana unaweza zunguka kutwa nzima ukaingiza elfu 32,000.

Jioni ile ndo unaenda kukabidhi hesabu kwa boss,

Mara Traffic uyo,
akakuwasha faini ya elfu 30, ukilipa unabaki na elfu 2 mfukoni.

Safari ya kwenda kwa bossi inaishia hapo hapo,
Iyo buku 2 Unajipinda kwa mama ntilie unaila WALI MAHARAGE.

Apo tayar bodaboda ushaumia,
Na boss HAWEZI kukuelewa.
 
Nipe hiyo hutuba ya bajeti nisome mwenyew
 
Back
Top Bottom