Bajeti Wizara ya Afrika Mashariki UPDATES: Sitta Kikaangoni, Zitto ampa Shavu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti Wizara ya Afrika Mashariki UPDATES: Sitta Kikaangoni, Zitto ampa Shavu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Aug 19, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bajeti Wizara ya Afrika Mashariki UPDATES: Sitta Kikaangoni, Zitto ampa ShavuBaadhi ya Wabunge wa CCM kutoka kambi ileee (Naomba niishie hapo) wameonekana dhahiri kutimiza azma yao ya muda mrefu ya kumwadabisha Mzee wa Viwango na Spidi Babu Sita baada ya Kuonyesha kuduwazwa kwao na kutojua anachokifanya Sitta ni kipi katika Wizara ya Afrika Mashariki.

  Akizungumza kwa mapozi na kusindikizwa na makofi (ambayo sina shaka ni ya wanakundi – sijasema mtandao) Gosbert Blandes wa Muleba amehoji kwa nini Wizara hiyo imekuwa haiweki bayana mambo na utendaji wake katika jumuiya na hivyo kutojulikana hasa ni lipi ambalo wanalifanya kwa manufaa ya Taifa katika jukumu hilo walilotumwa kuuwakilisha Uma wa Watanzania.

  Akiwa kama kaduwazwa hivi na Kauli hii ya Gosbert, Sitta alipokea Nyundo nyingine ambayo iliwalenga wabunge la Afrika Mashariki ambao mbunge huyo alisema wao mara zote wamekuwa wakipigiwa kura na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na huonekana kipindi cha kuomba kura wakipitapita huku na huko na baada ya kuchaguliwa Bunge halijui wanafanya nini na wako wapi (Huku makofi meengi yakilipuka kuonyesha kukungwa na hoja hiyo)
  Wizara hiyo imelaumiwa kwa kushindwa kuweka mikakati ambayo itawasaidia watanzania kumudu shuluba za jumuiya ya Afrika Mashariki na kuongeza pato la Taifa.

  Hata hivyo katika hali isyokuwa ya kawaida alipewa Nafasi ya upendeleo kutokana na muda uliokuwa umesalia Kiongozi kaimu wa Upinzani Bungeni Mh. Kabwe ambaye kwa upande mmoja alimwaga data za mafanikio kwa umoja huo (ambazo sina shaka kwa uswahiba na Sitta, atakuwa alimmegea haya ili amsafishe)
  Kabwe alionekana kuwashambulia wabunge wanaoilaumu Wizara (Huku Sitta akionekana kukunwa sana na kupiga makofi mazito katika benchi lake) hiyo kwa kuonyesha mabadiliko katika GDP kutoka miaka ya 2006 hadi 2010 ambapo kuna ongezeko la karibu bilioni 20 ukilinganisha na bilioni 16 za Kenya japo hakubainisha hizo fedha ni kwa currency moja ya Tanzania au kila Nchi kwa currency yake.

  Pamoja na kujaribu kumcover Mzee wa Viwango hakusita kuhoji utambuzi wa miopaka ya Nchi ambayo inaonekana Nguvu na umuhimu umeelkezwa katika mipaka inayounganisha Tanzania na Kenya Zaidi
  Akimnkuu Profesa Kabudi Paramagamba Zitto amedai kuwa tatizo la watanzania ni wepesi kukiri udhaifu wetu na wagumu kukubali mafanikio hata kama madogo. Zitto pia alionyesha kwa kiwango gani tumefanikiwa kuuza Nje kuliko kuagiza kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki .(Tunauza nini hivi au ndo huu mchele na mahindi ya wizi????)Baada ya Zito alichangia Serukamba ambaye bifu lake na Mzee wa Viwango tunalijua mna muda mwingi aliishia kuponda kulikopitilizaMy TAKE:
  • Hebu tujiulize Wizara hivi kweli imefanya nini kwa kipindi hiki na hawa wabunge amabo leo wameombwa ikiwezekana Mihutasari ya vikao vyao iletwe na wabunge waisome kujua kinachoendelea huko.
  • Mafanikio ya Wizara hii ni sahihi kupimwa kwa ongezeko la GDP?
  ADIOS
   
Loading...