Bajeti: Wafahamu bajeti ya halmashauri,mji,manispaa au jiji lako.....????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti: Wafahamu bajeti ya halmashauri,mji,manispaa au jiji lako.....?????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TRACE, Jun 23, 2010.

 1. TRACE

  TRACE Member

  #1
  Jun 23, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 91
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Wandugu,kila mara utakuta watu wakilalamika kuwa HALMASHAURI,MJI,MANISPAA AU JIJI yao hayana maendeleo wakati raslimali wanazo.Naomba niwaulize swali la msingi wao pamoja na wewe unayesoma hapa kuwa waweza kujua mipango ya HALMASHAURI,MJI,MANISPAA AU JIJI juu ya bajeti itakayotumika mwaka wa fedha 2010/11 na kama mambo yakiwa siyo yale waliyoyapanga uweze kuwa na uwezo wa kufuatilia na kuhoji ?

  Kama jibu utaniambia kuwa ni kazi ya Diwani au Mbunge wako kujua hilo je,ulipomchagua uliangalia/utaangalia uwezo wake wa kufuatilia ili aweze kukuelemisha na kukufungua macho wewe uweze kujua ?

  Na Je,kama yote kwako hujawahi kuyawaza unafikiri lini ni muda muafaka kwako kujua jinsi matayarisho ya bajeti yanaanza na jinsi yanavyoathiri maendeleo ya HALMASHAURI,MJI,MANISPAA AU JIJI yetu na kisha lawama tunawatupia wengine badala ya kujilaumu wenyewe?

  Itakuwa vizuri tukilijadili hili hapa kwa kina kwani hapa kuna watu wa kila aina na uwezo tofauti

  Nawakilisha
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu...i like this, lakini nahisi haupo clear! Correct me if am wrong. Unataka tujadili bajeti za halmashauri zetu? Kama ni hivyo, nadhani humu ndani hakuna, narudia tena, HAKUNA mtu anayejua bajeti ya halmashauri yake au hata matayarisho yake. Tatizo nililogundua, including for me, wengi wetu hatuna fundamentals au MISINGI imara. Tunapiga kelele na kudhani tunajua, lakini kama kweli tungejua, CCM isingeweza kututisha. Mimi sijui bajeti wala nani wa wapi pa kwenda kujua mipango yetu ya maendeleo katika halmashauri yangu!!! Na nina uhakika nikiomba kutuma mtu watasema ninapoteza muda wao!!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Let alone kujua bajeti detailed like it is, wananchi tunachotaka kuona ni matokeo ya bajeti!...Kujua details za bajeti ni ngumu, lakini pia ni watu wangapi watakuwa na access nayo ili kuhesabu kila shilingi?...Tunahitaji mashimo yazibwe, barabara ziwe na drainage, taka zizolewe kwa wakati, maji japo ya MCHINA yapatikane!...and for those things we are ready to go at somebody's throat!
   
 4. TRACE

  TRACE Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 91
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Nawashukuru wandugu kwa kuwa na interest ya kufahamu ni kwa vipi na namna gani bajeti za Halmashauri,Manispaa au Majiji yetu huandaliwa.Kwa uchache nitaweka nondo kidogo na kama kutakuwa na maswali nitajaribu kuwajibu.

  Bajeti huandaliwa na wananchi wa eneo husika na kisha mawazo au vipaumbele vyao hasa katika miradi ya maendeleo hukusanywa na watendaji wa halmashauri kiidara na kuwakilishwa halmashauri,manispaa au majiji kwa ajili ya kupata mpando kamili wa bajeti ikiunganishwa na bajeti za matumizi mengineyo(OC) pamoja na makadirio ya bajeti za mishahara kwa wafanyakazi walipwao kwa mapato wayakusanyanyo manispaa,walipwao kwa fedha zitokazo hazina na watarajiwao kuajiriwa huwa maripo yao hutengwa kabisa

  Vile vile Manispaa,Majiji na Halmashauri hupewa fedha na wahisani mbali mbali wa ndani na hasa nje ya nchi katika miradi ya maendeleo mahsusi hasa Kilimo na mifugo,vita dhidi ya ukimwi,maji,barabara,maendeleo ya watumishi wao,afya,elimu msingi na sekondari na nyingine nyingi ambazo hutakiwa kushughulikia matatizo husika tu na sio vinginevyo.

  Kwa urahisi uliokuwepo,mara baada ya kila bajeti kukamilika hutumia mfumo wa PlanRep2 (Planning and Reporting Database) kucompile bajeti za kila idara na kupata faili moja la Halmashauri,Manispaa au Jiji na Kupeleka Mkoani kwenye Database ijulikanayo kama PlanRep Meso ambayo inauwezo wa ku compile na kufanya analysis ya kila halmashauri na ku compile data za kila mkoa na kupata Data za Nchi nzima na kutengeneza fila moja.

  Mara baada ya bajeti kupelekwa Mkoani kwa mapitio ndio inakuja kuletwa Wizara ya Fedha kwa kuhakikiwa mara ya mwisho na kuunganisha bajeti za Balozi zote,wizara zote kupitia System ya SBAS ambayo hutoa bajeti ya nchi nzima na hapo ndipo unaweza kupata summary za kila aina uzitakazo na mwisho hupelekwa Bungeni.

  Ni kwa uchache tu ila kama kutakuwa na swali nitakuwa najaribu kuyajibu

  Nawakilisha
   
 5. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Cha muhimu ni nini kimetokana na budget hiyo
   
Loading...