Bajeti Tegemezi Na Matumizi Yetu Kwenye Misafara: Hivi kweli tunachapa kazi?

Ahsante kwa changamoto Sam na ahsante kwa maelezo. Ila napenda kuuliza, nikiamini kuwa kiongozi wa ngazi ya juu serikalini majukumu yake ni sawia akiwa katika mkoa wowote nchini, je waziri mkuu anapoenda mkoa wowote mwingine mbali na DSM hiyo ndiyo protokali ya misafara?
 
kama kuna ulazima wa kuongozana na wakuu hawa katika ziara, kwa nini yasinunuliwe mabasi kila mkoa ukapewa basi moja?

Nakuunga mkono hapa,kama viongozi wote wa G 8 kwenye mkutano uliofanyika Japan miaka ya nyuma walipanda basi moja sie masikini tunashindwa nini? kwanza wanaweza kubadilishana mawazo humo kwenye basi.
 
Aise...hii sasa imezidi! Kama hali ndo hii si bora Mheshimiwa angefanya ziara zake kwa kusafiri na Helikopta?! na uhakika ingekuwa rahisi zaidi kuliko kutumia 'mashangingi' yote haya...hebu fikiria hizi pesa za kununulia magari haya zinaweza kujenga shule ngapi? zikawasomesha watoto wangapi? au zikachimba misingi mingapi? na kuwarahisishia kazi wamama wangapi wanaehangaika kutafuta maji kila siku? Ndugu zangu haya ni maswali ambayo inabidi tujiulize na tutafakari. Badala ya kuwa na Ambulance si wangempenyesha Daktari moja na ki 'first aid' kit chake kwenye hayo magari mengine. Pembeni na Waziri Mkuu, hao wenzake si wangetumia Bus Moja, pamoja na Police escort kwa ajili ya usalama. Kwa mwendo huu hatufiki popote!
 
Naona sasa watu tunakuwa wajinga... u mean to tell me that of all the misappropriation that happens in Tanzania hili ndio mmeona kubwa..lol
mngekuwa na akili mngegundua kuwa huu ni msafara wa PM akiwa kwenye ziara including, as stated above. RC, PRC, DC au ma DC wote wa mkoa husika, usalama, na maafisa wengine wengi.. Mimi nimkazi wa Oysterbay na mara nyingi nakutana na msafara wa waziri mkuu... ukweli ni kwamba akiwa dar-es-salaam akienda kazini anakuwa na gari yake, mbili za walinzi na piki piki... sasa muache kuwa mnatoa hoja zisizo na kichwa wala mkia... This is the loss of objectivity in exchange for jazba... mnakuwa kama Michael Moore..lol..

Mkuu hoja inajibiwa kwa hoja huna sababu ya kulazimisha watu wakukubali kwa kuwa wewe unakaa osterbay, unachotakiwa kusema ni sababu zinazokufanya uamini kuwa msafara huu ni sahihi kwa nchi ambayo ni masikini kama tanzania.

Hta kama anakwenda mkoani anatakiwa kuwa na msafara ambao unreflect matatizo ya watanzania, au ndio yaleyale ya hata kama nyasi watu wale lakini waziri mkuu awe na msafara mkubwa kama hule.

Hivi Al Qaeda walikuja lini tanzania kiasi cha waziri mkuu kuwa na msafara wa aina hiyo, kama waziri mkuu anaogopea maisha yake namna hiyo najiuliza alifanya nini kwa watanzania kiasi cha kuwaogopa namna hiyo.
 
My thousand words....!

steved-albums-mh_pinda-picture168-msafara-pinda-morogoro-mjngw3b.jpg

Mie naipenda hii Honda! Waniambie tu wakati wa dili za kuuziana ninunue!:D
 
Naona sasa watu tunakuwa wajinga... u mean to tell me that of all the misappropriation that happens in Tanzania hili ndio mmeona kubwa..lol
mngekuwa na akili mngegundua kuwa huu ni msafara wa PM akiwa kwenye ziara including, as stated above. RC, PRC, DC au ma DC wote wa mkoa husika, usalama, na maafisa wengine wengi.. Mimi nimkazi wa Oysterbay na mara nyingi nakutana na msafara wa waziri mkuu... ukweli ni kwamba akiwa dar-es-salaam akienda kazini anakuwa na gari yake, mbili za walinzi na piki piki... sasa muache kuwa mnatoa hoja zisizo na kichwa wala mkia... This is the loss of objectivity in exchange for jazba... mnakuwa kama Michael Moore..lol..

Ndg kinyambiss pole na maisha ndg yangu.Nimefurahi ulivyojichanganya hapo kwenye wino mwekundu.kumbe aliwa Dar Kikazi anakuwa na magari machache na (kwa mujibu wako) unamaanisha akiwa mikoani picnic ndo anakuwa na msafara mreeeefu.Ndg funguka macho.Hata huko alikokwenda mikoani ni ziara ya KIKAZI.

Sisi hatuongelei kukaa kwako Oysterbay sijui wapi na kuuona msafara wa waziri mkuu.Mimi nakaa majita na nimekuwa najiuliza kwenye hiyo picha,kama lengo ni kumlinda waziri mkuu iweje huyo mjengwa aliyempiga picha na kamera yetu ya kijiji aweze kuichambua na kuipata gari ya waziri mkuu na kuonekana hadi plate namba yake????assume huyo mjengwa angekuwa na Bunduki angepata nini???Kama suala ni ulinzi KINACHOLINDA SIYO HAYO MAGARI NA KUFUATANA au kupangana Hivyo.Fikiria vizuri.By the way,utaona hapo kuna gari la askari wa OCD yaani hao wa GD wenye nguo za kaki na bado nyuma kuna gari la FFU eti la swipa na kati kati kuna wengine wanausalama na zingatia kuwa RPC ana bodigadi na OCD pia ana bodigadi,sasa kwa nini wote hao wasiwe gari moja kumlinda mkuu kwenye msafara wake?????Pia ujue kuwa kuna wanausalama ambao wao hawako kwenye msafara huo yani nusanusa.Wee vipi bwana kusema sasa sisi tumekuwa wajinga???wajinga ni nani kati ya sisi na wewe usiyejua kitu.

Mimi nimewahi kuwa kwenye misafara miiiiingi tu kama hiyo.Wa mwisho ilikuwa ni ukaguzi wa njia za mbio za mwenge wakati wa zamani kidogo.Lakini tulikuwa na busara katika matumizi.Tulitumia magari ya RSO na RPC tu kufanya kazi hiyo lakini tulibeba kila Idara.
Unataka kusema kuwa kwenye ziara hiyo RPC,RSO,OCD,DSO hawawezi kuwa gari moja na RC,DC,REO,Mkurugenzi na Mbunge gari moja kama hoja ni Viongozi kuwepo na hao maaskari polisi GD na FFU wakawa gari moja kama hoja ni ulinzi?????Kwa akili zako matumizi ya hiyo pikipiki niamaki nini hasa????Kama ni kutaadharisha kwa ving'ora huoni kama hiyo gari ya polisi ina king'ora??????
Acha hizo na Oysterbay yako.Karibu majita tuvue samaki
 
Ndg kinyambiss pole na maisha ndg yangu.Nimefurahi ulivyojichanganya hapo kwenye wino mwekundu.kumbe aliwa Dar Kikazi anakuwa na magari machache na (kwa mujibu wako) unamaanisha akiwa mikoani picnic ndo anakuwa na msafara mreeeefu.Ndg funguka macho.Hata huko alikokwenda mikoani ni ziara ya KIKAZI.

Sisi hatuongelei kukaa kwako Oysterbay sijui wapi na kuuona msafara wa waziri mkuu.Mimi nakaa majita na nimekuwa najiuliza kwenye hiyo picha,kama lengo ni kumlinda waziri mkuu iweje huyo mjengwa aliyempiga picha na kamera yetu ya kijiji aweze kuichambua na kuipata gari ya waziri mkuu na kuonekana hadi plate namba yake????assume huyo mjengwa angekuwa na Bunduki angepata nini???

Karibu majita tuvue samaki

Majita kudos, sikuiwaza hii hata kidogo. Inamaanisha angemtarget vizuri sana huyu wetu mheshimiwa sana. Hatari hii.
 
Watanzania tukiambiwa ni wavivu au tunapenda kujongo kazi na uselule tunakataa.

Angalia jinsi misafara ya viongozi wanapokwenda kukagua shughuli mikoani au kwenye safari za kimataifa, kuna utitiri wa watu si chini ya mia ukiongeza Wananchi ambao wanaambiwa wajikusanye kushangilia!

Angalieni hii picha na muone waliojikusanya. Naamini mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wakurugenzi wa maendeleo wake na mkuu wa polisi, mkuu wa wilaya ya Mwanga na wakubwa wenzake, mkuu wa wilaya ya Same ambayo ni jirani pamoja na wapambe wake, si ajabu mbunge wa Mwanga na Same wako hapa, njoo wenyeviti wa vijiji, kata, tarafa na sasa uje kichama, Mwenyekiti wa CCM mkoa, wilaya, vijiji, katibu wa chama na wengine wengi.

Bado wale wanaosafiri na Kiongozi mkuu kutoka makao makuu na wasaidizi wake!

When do people work in Tanzania?

125147.jpg
 
Mzee unawatakia mema hao au??

Lazima uupambe msafara wa mkubwa vinginevyo jina lako litaingizwa kwenye kitabu cheusi (you will be black-listed). Suala la kufanya kazi kwao siyo muhimu ili mradi wako madarakani. Sidhani kama kuna mtu hajui hilo!!
 
Hapa hujaongelea resources wanazotumia kama magari, posho na vingine, hawana huruma na taifa wanlitia hasara mara mbili kazi hawafanyi na wanatumia resources zilizotengenezwa na wachache wenye kufanya kazi.
 
Mgeni aje..mwenyeji apone!
Kuzusha sherehesherehe ndiyo jadi yetu.Msafara.... huishia na dhifa!Gharama, gharama, gharama.... msalaba anaubeba mlala hoi.Pole zetu watz.
 
Let's think SMALL.

Kama kuna ulazima wa kwenda na magari na kuandamana na hao wote.
Je, RC na DC hawawezi kupanda gari moja, kwa nini?

Kuna mwiko gani RPC na OCD kutumia gari moja?

Mkurugenzi wa Halmashauri naye apande gari la Gari na Mbunge/Wabunge.

Bibi Ntilie,

"Wanaweza kufa kwa ajali na hivyo kuwa gharama za mazishi na uchaguzi mpya....."

Swali kwa nini kutokee ajali nao wako kwenye msafara? ni barabara mbovu, mwendokasi mbaya au gari halifanyiwi maintenance kila mara kwa kuwa Dereva na mafundi wametia ndani pesa na spare parts kwa kuwa mishahara midogo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom