Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Umetimia mwaka mmoja sasa tangu niandike makala hii nikishutumu vikundi vya propaganda vya chama cha mapinduzi vilivyokuwa vikiongozwa na Humphrey Polepole ambae baada ya kazi hii amehongwa ukatibu mwenezi wa chama hicho twawala,
Msingi wa shutuma hizo nilikuwa nikipinga utetezi wa Serikali kwamba "imekataa" misaada kwakuwa imeamua kuanza kujitegemea, hivyo haitaki misaada ya wahisani wa kimagharibi ama Asia ya Mbali.
Kuna kikundi cha propaganda kilichokuwa kikiongozwa na kada mahiri wa ccm bwana Humphrey Polepole kilijipa jukumu la kupotosha sababu za kunyimwa pesa za za wahisani hasa mcc ya Marekani kuwa mpango huo nimatokeo ya serikali kukataa kunyenyekea misaada kwa vile inaelekea katika kujitegemea na inaboresha makusanyo.
Huu ni uongo na dharau kubwa kwa Watanzania na dunia kwa ujumla, ukweli ni kuwa, Sababu kuu za kunyimwa pesa hizo ni mbili tu.
1. Suala la demokrasia na utawala bora (uchaguzi zanzibar)
2. Suala la uhuru wa habari na kutoa maoni nchini (sheria ya uhalifu wa mitandao ya 2015)
Ifahamike masharti mkuu ya kupata pesa hizo ni lazima ukidhi vigezo hivyo, na tangu 2007 kama Taifa tumekuwa tukikidhi vigezo hivyo na kupokea msaada huo.
Hatutaki kuishi kwa misaada na siku zote tumekuwa tukipigana taifa lijitegemee, lakini wenzetu hawa wanaopotosha leo huko nyuma walituambia kuwa nchi haiwezi kwenda bila kuombaomba. Kipindi cha utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tulikorofishana na mataifa wahisani hasa Marekani na Ujerumani Magharibi wakatunyima misaada, lakini tuliokolewa na shirika la maendeleo la nchi za Scandnavian DANIDA.
Bajeti ya Tanzania 2016/17 kiasi cha trilioni 9 kilikuwa ni makadirio ya misaada ya wahisani tu, lakini mpaka leo wahisani hawa tuliowatarajia wametunyima kabisa, yani wametoa sio zaidi ya 150 bilioni tu, Hapo ndipo utaona nchi imekwama wapi.... Wakati huo Bajeti ya ndani utekelezwaji wake haujavuka 50, kisha mtu anainuka na kurubuni watanzania kwama ugumu wa maisha ni kwakuwa nchi inajenga uchumi (transitions), Polepole na wenzio liambieni taifa ukweli kwamba Taifa linakwenda hivi kutokana na ukata, sio matakwa wala sera ya serikali taifa liende hivi bali matakwa ya kibajeti kufeli.
Leo Taifa kimeamua kuingia kwenye mikopo mikubwa WB na kufanya deni la taifa kukaribia 50trilions kiasi ambacho kinavunja rekodi ya deni la nchi. Majanbazi ya Uchina hayawezi kusaidia bajeti ya Taifa letu labda kutuibia raslimali zaidi ya alivyotuibia huyu mzungu. China inaweza kusaidia Chama cha Mapinduzi kuiba kura tu sio Bajeti ya Nchi.
Niliunga mkono malengo ya kujitegemea hapo 2016 na leo nitaendelea kuunga mkono kujitegemea kwa Taifa letu, lakini ifahamike kuwa bajeti ya 2016/17 tayari pesa hii tuliyonyimwa ilishaingizwa kama bajeti. Hivyo miradi ya umeme vijiji REA, maji, barabara, madeni ya makandarasi nk vimekwama kutekelezwa, na nchi imeamua kwenda kukopa WB na BOA mikopo yenye riba kubwa,na mwisho taifa linaendelea kuwa la kitumwa mbele ya taasisi hizo. Ahadi ya nchi ya viwanda ya mh rais imekwama, kinyume chake imezaliwa inchi ya viwanda vya visasa na ubaazi, badala yake tunategemea mapato ya ndani ili tulipane mishahara na kuendesha serikali tu.
Zingatia makampuni binafsi yanafunga biashara zao nchini, pia kuna panga la punguzo la wafanyakazi kubwa katika sekta binafsi na za umma limetokea, tccl tayari imeachisha kazi watu 400, ACCACIA au Baric imeshaachisha wafanyakazi zaidi ya 600,...... Ni kipitindi kigumu sana kwa taifa letu. Ajira hakuna nk.
Njia bora kwa sasa ni kuweka mahusiano bora na sekta binafsi kuliko kuendesha nchi kwa kodi za kukomoana, Sera ya biashara na kodi itazamwe upya kwakuwa haina ushirika mzuri na sekta binafsi, Duniani kote sekta binafsi ndio inayoinua taifa kiuchumi.