barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Hatimaye Serikali kupitia Wizara ya fedha imehalalisha mchezo wa "betting" kama kazi rasmi. Hii inatokana na Waziri wa Wizara ya Fedha kutangaza rasmi kuwa "mikeka na waanika mikeka" wanatakiwa kulipa kodi ya 18% kila mzigo.
Wale wazee wenzangu wa kuanika mikeka sasa tunaingia rasmi kama wachangiaji wa pato la Taifa kwa kuchangia kodi kila tuanikapo mikeka na kupata mzigo. Hii inatuingiza wacheza kamali kuwa "sekta rasmi" inayochangia pato la Taifa.
Kwa wanaofuatilia katika vibanda umiza na maeneo ya Uswahilini, kwa sasa vijana wengi na hata watoto wa shule wamejiingiza kwenye biashara hii kwa kasi ya ajabu sana.
Kianzio cha "kuanika mkeka" ni shilingi 500 tu, hii inafanya mpaka watoto wa shule ya Msingi kujibana na kutumia pesa zao kucheza mchezo huu.
Wakati Serikali ikiwa imefikia hatua ya kuruhusu "mchezo" huu kuwa chanzo cha pato la Taifa, ikumbuke pia kuweka taratibu za ushiriki hasa kwa watoto walio chini ya miaka 18 ambao wanaonekana kuchipukia na kushiriki kwa kasi katika mchezo huu.
Primier Betting na Meridian betting zina mawakala zaidi hata ya wale wa Mpesa na Tigopesa, wametapakaa kila kona. Wakati tunafurahia kupata "chanzo" cha Mapato ya Serikali, tukumbuke pia maadili ya Taifa, hata kabla ya Serikali kufanya huu mchezo kuwa chanzo cha mapato, vibanda umiza mtaani vilijaa pomoni, si kwamba wengi wanapenda sana kuangalia mpira, bali wengi hukaa kusubiri kama "mikeka" walioanika itaanuliwa au la!!
Kwa sasa "betting" imekuwa zaidi ya Ligi kubwa tu za Ulaya Magharibi, imesambaa mpaka kwa ligi za China, Argentina, Brazil mpaka US, Vijana, watoto na wazee sasa wanaweka mikeka mpaka kwenye mbio za farasi, mbwa na hata zile za magari ya "rangaranga"
Wazee wenzangu wa mikeka kazi imeanza, hatimaye Serikali imetutambua kama walipa kodi rasmi na wachangiaji wa pato la Taifa.
Tuhamasishane kwenye vibanda umiza ili tukajiandikishe kwenye BVR ili kuchagua viongozi bora na wazuri, kuepuka hela zetu za kodi zitokanazo na "mikeka" kuliwa na watu wachache.