Bajeti moja ya barabara ya Rais Samia inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,980
4,076

Bajeti moja ya barabara,madaraja na viwanja vya ndege ya Rais Samia FY2021|22 inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano iliyopita,​

"Hakuna kama Samia "​


Kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo endelevu Watanzania hawa masikini inatetemesha,

Rais huyu katika kutambua ili nchi yeyote ile hapa duniani iendelee kwa kasi lazima iwe na miundombinu ya barabara iliyo rafiki na madhubuti,

Rais Samia Suluhu Hassan tayari kwenye bajeti yake ya kwanza yaani FY2021|22 ametoa TZS 2trilioni,

Fedha hii ni kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja,

Kwa msiofahamu,bajaeti hii ni sawa na ongezeko la 100% la Bajeti ya serikali iliyopita ambayo ilitenga Tshs 1trilioni FY2020|21

Sikia hii, Kama gharama ya kujenga kilometa moja ya" lami" kwa kiwango cha kimataifa ni TZS 1BL/Km,

Bajeti hii ya Rais Samia inaweza kujenga jumla ya kilometa mpya 2,000 za lami kwa mwaka huu mmoja wa fedha wa 2021|22,

Kilometa hizi za lami ni sawa na 18.3% ya barabara zote km 10,941 zilizowahi kujengwa tangu tupate Uhuru,

Nakama mwendo ni huu mpaka kufikia FY2030|31 basi barabara zote km 33,649 nchi nzima huenda zitakuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami,

Katika historia ya nchi hii kama kuna mtu anatakiwa kuombewa kwa nguvu zote basi ni huyu Mama,

Kwamsiofahamu,Hayati Rais Magufuli kwa miaka yake mitano alifanikiwa kujenga Jumla ya km 1,004,

Taarifa hii ni kwamujibu wa National Bureau of Statistics (NBS),

Kwa lugha rahisi Bajeti moja ya barabaraba ya Rais Samia inaweza kujenga marambili (X2) ya barabara zote zilizojengwa kwa miaka mitano mfululizo ya Serikali ya awamu ya tano ( A comparative analysis|advantage )

Raha Sana kuwa na Rais mwenye speed kama Mama Samia Suluhu

IMG-20210918-WA0058.jpg


VIVA SAMIA VIVA || VIVA MPANGO VIVA

photo_2021-11-06_10-31-11.jpg


IMG-20220416-WA0020.jpg
 
Sikukosea kumuunga mkono huyu mama,
Kila siku nazidi kufurahi sana, Mimi naamini tutafika mbali sana na Rais Samia, Kumbe mzee baba km elfu tu duu, Nawashangaa mnaotaka kukigawa kama taarifa zenyewe za kazi ndio hizi
 
WATANZANIA AKILI ZITURUDI SASA,

Wale mnaolia na hayati kumbe miaka mitano mlijenga Km 1,004 tu za lami nchi nzima Mungu anawaona?

Hivi kumbe mlikuwa mnawapiga watu fix tu?
Ndio maana mnamwonea wivu mama kipenzi cha Watanzania kwa kufanya yale Watanzania wanataka,

Njooni tuungane tujenge nchi na chama chetu sioni ata haja ya Upinzani Tanzania,

Ndio kwa mara ya kwanza Ujenzi wa barabara,madaraja tunapewa pesa nyingi zaidi kwenye historia ya nchi hii ni kweli,
Mbataka nisimuunge mkono Rais wangu kwa lipi?

Inyeshe liwake nitakuwa na samia
 
Ni habari njema sana, tunaomwombea mama mazuri tunafarijika tukisikia hivi.....tutafarijika zaidi TUKIONA!

Ila mkuu nikuombe jambo moja; tupe tu hizo taarifa njema kila zinapotokea lakini usizijenge katika kuwashindanisha yeye na mtangulizi wake. Sioni afya katika hilo.......walikuwa pamoja na marehemu, itaibua ushindani usio na maana humu na kwingineko
 
KAZI IENDELEE

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote
 

Bajeti moja ya barabara,madaraja na viwanja vya ndege ya Rais Samia FY2021|22 inaweza kujenga mara mbili ya barabara zote za lami zilizojengwa kwa miaka mitano ya awamu ya tano​

=================================
Kasi ya Rais Samia katika kuwaletea maendeleo Watanzani hawa masikini inatetemesha kama wanavyosema, Rais huyu katika kutambua ili nchi yeyote iendelee kwa kasi lazima iwe na miundombinu ya barabara iliyo rafiki na madhubuti, Rais tayari kwenye bajeti yake ya kwanza yaani FY2021|22 ametoa Tshs 2trilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja, bajaeti hii ni sawa na ongezeko la 100% la Bajeti ya serikali iliyopita ambayo iliten
Wakati tunawaambia hakuna kama Samia mlituona mazoba haya sasa takwimu hizo mzipinge tuone,
Samia kama Samia ni Samia tu mpaka 2030 atakayejipendekeza tunalala nae mbele,
 
Ainisha hayo madaraja na barabara ni zipi kwa majina na mikoa,wilaya na hata ikibidi tarafa ili tujue ukweli kama miradi hiyo inaendelea sehemu husika,isije ikawa enzi za Magu mara vituo vipya afya zaidi mia mbili vilijengwa leo mnatuambia ni 34 tu.
 
Back
Top Bottom