Bajeti Mbadala Ya Upinzani 2008/2009.

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Nimewaletea BAJETI YA UPIZANI KAMA ILIVYOSOMWA LEO BUNGENI NA KIONGOZI WA UPINZANI.
 

Attachments

  • SHADOW BUDGET 2008 POPULAR.doc
    238 KB · Views: 262
Hii Bajeti imechelewa kutumwa kutokana na matatizo ya kimtandao huko Dodoma .

Nawatakia kuisoma kwema.
 
Kwa mara ya kwanza leo wakati Bajeti hiyo ikiwasilishwa buneni viongozi wa kambi ya upinzani walikuwepo buneni ili kuwapa support wabunge wao.
Viongozi hao walikuwa ni Freeman Mbowe-CHADEMA, Prof.Lipumba CUF, Mwakilishi wa NCCR MAGEUZI .

Baada ya kusomwa viongozi hao pamoja na wabunge wote wa kambi ya upinzani walikaa na kupata chakula cha mchana pamoja ,na kupanga mkakati wa kuibana serikali kuhusiana na bajeti kuanzia kesho na kuendelea mpaka kieleweke na wao watajipanga kisiasa pia ... huenda wakaenda tena mikoani kama mwaka mwaka jana na kulazimisha mawaziri kuwafuata japo hakuna hilo fungu kwenye bajeti ya serikali.
 
Ili mwanga ufanye kazi ni lazima giza lije, wao kwanza(watawala) sisi (wananchi)tunafuata! tunashukuru kwani inapakulika kirahisi.
 
Hivi ndiyo vitu vya kukaa na kuongea sasa hivi. JF jamani wengine tuko ughaibuni tuleteeni mambo yanayotokea kila siku huko bungeni ikiwamo michango ya wabunge mbalimbali. Hivi ndivyo vitu sasa tuchambue pamoja na ile ya serikali
 
Posted Date::6/16/2008
Kambi ya upinzani bungeni yatangaza bajeti ya Sh 8.1 trilioni
*Watpendekeza bei ya mafuta ya taa ipingue Sh250
*Wataka ratiba ya safari za Rais kwa mwaka iwe wazi

Ramadhan Semtawa na Salim Said
Mwananchi

KAMBI ya upinzani imetoa bajeti mbadala ya Sh8.1 trilioni kwa mwaka 2008/09, ikilinganishwa na Sh7.2 trilioni ya serikali, ambayo pamoja na mambo mengine, imeonyesha jinsi nchi inavyopoteza mabilioni ya shilingi kutoka vyanzo mbalimbali, yakiwamo madini na misamaha ya kodi.

Bajeti hiyo mbadala ambayo ilisomwa jana bungeni mjini Dodoma kiongozi wa kambi hiyo na Waziri kivuli wa Fedha Bungeni, Hamad Rashid Mohamed (Wawi-CUF) na nakala yake kupatikana jijini Dar e s Salaam, pia imetoa mapendekezo mbalimbali huku ikitaka Ripoti ya Rais kuhusu kuchunguza mikataba ya madini iwasilishwe bungeni ili ijadiliwe.

Bajeti hiyo mbadala inaitaka serikali kutoa ratiba ya safari za Rais na mawaziri kwa mwaka, ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na malipo hewa na kupendekeza kima cha chini cha mshahara kwa mtumishi wa umma kuwa kiwe Sh 250,000.

Ndani ya hotuba ambayo imechambua sekta moja baada ya nyingine, pia imetoa bajeti mbadala kwa fungu la fedha kwa maeneo ya kipaumbele ikilinganisha na zile lililotengwa na serikali.

Kambi ya upinzani katika bajeti yao mbadala, imependekeza sekta ya Miundombinu kutengewa asilimia 21 ya bajeti, Elimu, asilimia 22, Kilimo, asilimia 12, Afya, asilimia 10, Nishati asilimia 8, Maji, asilimia 10 na Matumizi mengineyo asilimia 17.

Kuhusu mapungufu ya makusanyo ya mapato ya serikali, kambi hiyo ilisema kutokana na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) katika Wizara na Idara za Serikali walizochambua, ilibainika upungufu wa makusanyo ya mapato, mrahaba usiokusanywa kutoka Kampuni ya Almasi ya Williamson Ltd ni Sh 841.1 bilioni , Tansort Sh206.6 bilioni.

Kambi hiyo pia imemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi apeleke taarifa bungeni za uchunguzi wa ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) majengo pacha ya benki hiyo na makamuni ya Mwananchi Gold Mine na Meremeta.

"Waziri alieleze Bunge lako tukufu thamani halisi ya gharama za ujenzi wa majengo ya pacha Benki Kuu (Twin Tower) kuwa yanazui imeshazidi dola za Marekani 500 million au wastani wa Sh600 billion."

Kambi hiyo pia ilitaka taarifa za uwekezaji wa Mwananchi Gold Mine wa dola za Marekani 5,512,398.55 hadi tarehe 30 June, 2006 na kama BoT iliendelea kuwekeza katika kampuni hiyo binafsi na kiasi gani cha mapato kilichopatikana hadi sasa.

"Kambi ya Upinzani inataka kupata taarifa ya kina kuhusu tathmini iliofanywa na BoT juu ya mradi huo. Pia tunataka kupatiwa taarifa rasmi juu ya umiliki wa mgodi huu sasa," alisema.

Kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano (JFC), kambi hiyo ilifafanua kwamba katika Kamati iliomba kupewa taarifa juu ya JFC, Waziri katika majibu yake (mwaka jana 2007/2008) alijibu: ?Wakati uamuzi kuhusu mapendekezo ya Tume unasubiriwa, bajeti ya 2007/08 imetenga mgao wa Zanzibar kwa utaratibu wa asilimia 4.5 ya misaada ya bajrti ?.

Hata hivyo, kambi hiyo ilisema waziri katika hotuba yake ya bajeti ya 2008/09 alisema: "Tume ya Pamoja ya Fedha inachambua maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ya ziada ili kuziwezesha Serikali hizo mbili kufikia maamuzi kuhusu mapendekezo ya Tume?.

Kuhusu mchakato wa zabuni ya kuipata Kampuni ya Alex Stuart Asseyers, kambi hiyo ilisema wakati ikiwasilisha maoni yake Bajeti ya 2004/2005/2006/2007 na 2007/2008, illiulizia juu ya kukiukwa kwa utaratibu wa kumpata mzabuni wa kuchunguza mauzo ya dhahabu unaofanywa na kampuni ya Alex Stuart Asseyers.

Hata hivyo, nje ya mategemeo Serikali haikusema ni kiasi gani cha mapato kimepatikana kutokana na taarifa ya baada ya Serikali kuilipa kampuni hiyo si chini ya dola 65,000,000 (sawa na Sh 85bilioni), inayotokana na mapato ya mrahaba wa 1.9 asilimia kati ya 3 inayopata Serikali kiasi ambacho kingeweza kukopesha wanafunzi 20,000 wa vyuo vikuu.

"Upinzani na Watanzania kwa ujumla tunaona haya ni mapungufu makubwa katika matumizi ya rasilimali na zaidi pale Serikali, inaposhindwa kueleza Bunge lako Tukufu mapato yaliyopatikana kutokana na kazi ya Alex Stuwart Asseyers. Badala yake imeunda Kamati ya Bomani ambayo ni ya sita katika miaka mitano (5miaka ) kuhusu jambo hilo hilo moja. Je, huu ni usanii au nini, Mheshimiwa Spika ?"

Kambi hiyo imetaka kupitiwa upya kwa Sheria ya Madini ya mwaka 1998, ili kuwezesha mrahaba unaotokana na makampuni yanayochimba madini uwe asilimia tano kutoka tatu huku mbili zikibaki katika halmashauri husika.

Upinzani ulifafanua kwamba, kutokana na serikali kutokuwa makini, ikiwa ni pamoja na udhaifu wa sheria ya Madini, imejikuta ikipoteza jumla ya Sh 1.3 trilioni katika kipindi cha miaka mitatu kutokana na ukuguzi uliofanywa na Kampuni ya Alex Stuart.

Kambi hiyo iliongeza kwamba, pia kutokana na Sheria mbaya ya Mapato katika sekta ya Madini serikali imejikuta ikipoteza Sh 883 bilioni katika kipindi cha miaka 10, sheria ambayo ilitungwa na Bunge mwaka 1997.

Kuhusu misamaha ya kodi, kambi hiyo ilifafanua kwamba eneo hilo limekuwa likipoteza fedha nyingi ambalo takwimu zinaonyesha kwamba inakadiriwa, Sh 819.9 billioni zilitolewa kama misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha unaomalizika huku misamaha hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni ya kutisha kwani mwaka 2006/2007 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikusanya kiasi cha Sh 20.4 bilioni huku misamaha ya kodi mbalimbali ikifikia sh 19.6 bilioni.

"Hiki ni kiasi kikubwa kwa nchi inayoomba misaada kila kukicha. Kambi ya Upinzani inaona huu ni upungufu mkubwa wa mapato ya wanyonge wa Watanzania kwa kuyatupa bila utaratibu wa wazi na unaoeleweka, ili kuongeza mapato yetu ya ndani Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ipunguze misamaha ya kodi kwa asilimia 50. Uamuzi huu utaweza kuongeza mapato na kuwa Sh 409.95 billion ambazo hazikusanywi hivi sasa."

Kuhusu uuzaji hisa za serikali, kambi hiyo ilisema bado kuna makampuni ambayo serikali ina hisa ambayo ingefaa ziuzwe? kwa wananchi, lakini serikali ipo kimya katika hili, mfano, ni hisa katika benki ya CRDB na kampuni la simu za mkononi ya CELTEL.

Ikichambua sekta ya Kilimo, kambi hiyo ilisema kwa sasa sekta hiyo imeporomoka ikilinganishwa na wakati wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa takwimu, kambi hiyo ilisema hekta za umwagiliaji katika sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi zimepungua kutoka 450,000 kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza hadi 298,888 kwa sasa, hali ambayo inaweza kuifanya nchi kukosa uwezo wa kujilisha hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imekuwa ikikumbwa na uhaba wa chakula.

Kuhusu bei ya mafuta na kodi za serikali, upinzani katika bajeti hiyo , ulisema serikali kwa upande mmoja imekuwa ikieleza kumwondolea umasikini mwananchi wa kawaida, huku wa pili unamuongezea kodi kwa mlango wa nyuma, kwa kutoa mfano wa bei za mafuta ya taa kwenye soko la dunia kuwa ni kubwa ukilinganisha na bei za mafuta ya petroli na dizeli.

"Bei za mafuta ya taa ni 1,182.22 kwa lita huku petrol ikiwa 934.97 na dizeli 1,027.40 , na hali ya bei hizo kwa hapa nyumbani ni tofauti haswa ukizingatia ya kuwa kodi na tozo mbalimbali kwa kila lita yaani Sh 59.10 mafuta ya taa, 545.1 petrol na 520.80 dizeli."

''Kambi ya upinzani inaona kwamba, katika kuonyesha umakini wa kuinua uchumi wetu hizo kodi za ndani zinazotozwa kwenye mafuta tunatoa punguzo la shilingi 250.00 kwa kila lita moja ili kukabiliana na bei ya soko la dunia, hii ndio njia pekee ya kuufanya uchumi wetu ukue," ilisisitiza kambi hiyo.

Upinzani katika bajeti yao hiyo pia ilikuwa ikichambua utekelezaji wa bajeti ya 2007/08, kwa kueleza kwamba, licha ya kuwepo na fedha nyingi zilizotengwa kwa sekta za maeneo ya kipaumbele bado matumizi yalikuwa chini ya bajeti.

Upinzani katika mchanganuo wao, umepanga kiasi cha Sh 5.7trilioni pato la ndani, Mikopo na Misaada ya Nje ikijumuisha 2.4trilioni jumla ni sh 8.1 trilioni.

Mjadala wa bajeti unaendelea kwa wiki nzima sasa kuanzia jana baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha bajeti ya serikali kwa mwaka 2008/09, hapo Juni 12 ambazo pia nchi za Kenya na Uganda zilisoma bajeti zao kama utaratibu uliowekwa kwa nchi hizo wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Katika hatua nyingine, Midraji Ibahim anaripoti kuwa Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Mvomero(CCM), Suleiman Ahmed Sadiq, alisema iwapo serikali hitasimamia kidete suala la wauza mafuta kuchanganya petroli na mafuta ya taa, itaendelea kupoteza mapato.

Sadiq alisema, licha ya kupoteza mapato magari ya wananchi yataendelea kuharibika kutokana mtindo wa baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta maarufu kama chakachua ambao umestawi vituo vya mafuta kati ya Kibaha na Chalinze.

Kuhusu Bandari ya Tanga, Sadiq alisema, hata barabara inayojengwa ya Tanga-Horohoro iwapo bandari hiyo haitaimarishwa, watakaofaidika ni Kenya.

Alihoji uhalali wa mafaili ya walipakodi wakubwa kuhamishiwa Dar es Salaam, huku wakiacha uzalishaji mikoani ukiendelea bila kuwepo usimamizi.


Mbunge wa Mkwajuni(CCM), Mzee Ngwali Zubeir alisema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano, zina nia njema lakini zinaelekea njia ya jehanamu.


Zubeir alisema, tume ya fedha ya pamoja inakumbwa na kikwazo cha watendaji na wakuu wa nchi kutoamua kazi za kufanya.

''Ni aibu asilimia 96 ya mapato inakwenda kwenye misamaha ya kodi, yaani misamaha inalingana na makusanyo yote? Hii ni aibu!'' alisema Zubeir.
 

KAMBI ya upinzani imetoa bajeti mbadala ya Sh8.1 trilioni kwa mwaka 2008/09, ikilinganishwa na Sh7.2 trilioni ya serikali...

Kuna kitu kimepinda hapa!
 
Kwa hiyo wao wangetumia hela zaidi kuliko Serikali?

Inawezekana hiki ni kituko kuliko vyote katika historia ya Bajeti mbadala za dunia, au historia ya vituko!

swala ni kwamba wangetumia pesa nyingi kwenye nini, sekta za kilimo, elimu, afya, miundombinu, sayansi na technologia zinahitaji fungu kubwa kuliko lilipangiwa. Bajeti ya sasa imeunderestimate hizi sector.
 
swala ni kwamba wangetumia pesa nyingi kwenye nini, sekta za kilimo, elimu, afya, miundombinu, sayansi na technologia zinahitaji fungu kubwa kuliko lilipangiwa. Bajeti ya sasa imeunderestimate hizi sector.

Lakini hudhani kwamba, kama nchi yenye bajeti omba-omba, ingebidi Wapinzani tusisitize kubana matumizi badala ya kuongeza?
 
Lakini hudhani kwamba, kama nchi yenye bajeti omba-omba, ingebidi Wapinzani tusisitize kubana matumizi badala ya kuongeza?

kubana matumizi ndio kurudisha nyuma maendeleo, ubane matumizi badala ya kutumia pesa zilizopo kuimarisha huduma. Huko kubana matumizi ndio kumesababisha mafisadi wakapata cha kuchota, why...kwa sababu kulikuwa na pesa ambazo hazikuwa na kazi.
 
kubana matumizi ndio kurudisha nyuma maendeleo, ubane matumizi badala ya kutumia pesa zilizopo kuimarisha huduma. Huko kubana matumizi ndio kumesababisha mafisadi wakapata cha kuchota, why...kwa sababu kulikuwa na pesa ambazo hazikuwa na kazi.

Kama kuna fedha zisizokuwa na kazi mbona sisi ni omba omba?
 
Kama kuna fedha zisizokuwa na kazi mbona sisi ni omba omba?

uomba omba wetu unatokana na tabia yetu ya kujikomba kwa wazungu. Na baada ya kuomba hizo pesa zinaishia kuibiwa na mafisadi. On the other hand hizo pesa hao wafadhili wanazotusaidia sio kwamba wanatusaidia, wanaturudishia pesa zetu walizotuibia wakishirikiana na mafisadi. Tanzania siyo nchi ya kuwa omba omba kabisaaa. Je unadhani kwa nini vyuo vyetu, barabara zetu na mahospitali haziboreshwi kwa kupatiwa infrastructure zinazokidhi mahitaji? kwa nini hatuna maji, wala barabara? jibu ni ukosefu wa fedha.

Wakati huo huo ni mapesa mangapi mafisadi wameiba?
 
Nimewaletea BAJETI YA UPIZANI KAMA ILIVYOSOMWA LEO BUNGENI NA KIONGOZI WA UPINZANI.

...imeondolewa nini?

kwangu imenigomea, napata ujumbe huu;

Works cannot open "blah ...blah..blah", the file may be in use by another appendix, the file format may not be supported by any of the installed connectors, or the file may be corrupt.

halafu 'nikilazimisha' nakutana na blank page!.

kuna aliyei download, aipaste hapa? tafadhali?.

Shukran.
 
Lakini ni omba omba!

by the way bajeti ya mwaka huu ndogo mno, yaani trillioni 7 zitafanya nini? ingebidi waombe zaidi, yaani ingalau kupunguza vijitatizo vya elimu, afya, miundombinu ingebidi iwe ka trillion 10 hivi. Hivi yale madeni pale ATC yatalipwa na pesa gani, TANESCO wanataka mabillioni kuimarisha miundo mbinu yao, bado DOWANS, Richmond na Kiwira, MAJI nao, etc, bado demand ni kubwa kuliko kilichotengwa kwenye bajeti.
 
by the way bajeti ya mwaka huu ndogo mno, yaani trillioni 7 zitafanya nini? ingebidi waombe zaidi, yaani ingalau kupunguza vijitatizo vya elimu, afya, miundombinu ingebidi iwe ka trillion 10 hivi. Hivi yale madeni pale ATC yatalipwa na pesa gani, TANESCO wanataka mabillioni kuimarisha miundo mbinu yao, bado DOWANS, Richmond na Kiwira, MAJI nao, etc, bado demand ni kubwa kuliko kilichotengwa kwenye bajeti.

Lakini wewe si umesema sisi hatutakiwi kuwa Omba Omba? Sasa tuombe zaidi tena kivipi?

Na sisi tukija kuombwa tutoe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom