Bajeti Kuu ya Serikali 2021/22 ni kipimo cha uongozi wa Rais Samia

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Macho na masikio ya wananchi yapo Dodoma kwenye Bunge la Bajeti kufuatilia ikiwa bajeti hii itakuwa mkombozi kwa wananchi ama la.

Ikumbukwe bajeti nyingi za awamu ya tano zilijielekeza kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo mathalani ununuzi wa ndege, ujenzi wa SGR, Stieglers, flyovers nk.

Bajeti hii itatoa mwanga ikiwa rais wa sasa ataendeleza yale ya mtangulizi wake ama ataanza zama zake. Tumeshasikia baadhi ya viongozi wakidai kuwa wanaendelea kutekeleza ilani ya CCM 2020-2025 lakini Rais hafungwi na ilani hii, anaweza kuelekeza wizara husika wakarekebisha bajeti zao.

Je, vipaumbele vitakuwa vipi?

  • Ajira?
  • Maslahi ya watumishi?
  • Elimu?
  • Afya?
  • Kilimo?
  • Miundombinu?
au?

Maendeleo ya watu + Maendeleo ya vitu = Maendeleo ya nchi na wananchi

Mpango wa bajeti 2021/22 ni Tr. 36.26

Bajeti iliyopita ilikuwa Tr. 34.88
 
Back
Top Bottom