Bajeti inayosomwa bungeni ni bajeti ya Tanzania au ya Tanganyika?

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,130
1. Kwanini hii bajeti inajumuisha wizara zote za muungano na zisizo za muungano?

2. Bajeti inayoishia 2021/2022, trilioni 39 Zanzibar imechangia kiasi gani kwenye makusanyo?

3. Hii misaada na mikopo kuna formula ya mgao kati ya Tanzania bara na Zanzibar Ila sijaona formula ya kulipa mikopo hii inalipwaje?

4. Kwanini mishahara ya watumishi wa SMZ ni midogo kulinganisha na idara na taasisi za Muungano? Zanzibar itoe mishahara midogo kwa watumishi wake kisha ichangie watumishi wa Muungano walipwe hela nyingi hili swala linawezekana?
"Au ndio mzigo mzito mpe Mnyamwezi"

Kuna vitu vinahitaji ufafanuzi wa kina kwenye haya mambo.
 
Hiyo ni bajeti ya Tanganyika! Ila cha kushangaza humo bungeni utakutana na Wazanzibar nao wanakula posho! Sijui huwa wanawakilisha nini!

Na wakati huo huo, huwezi kuwakuta Watanganyika kwenye lile Baraza lao la Wawakilishi kule Zanzibar wakipokea posho! Au kuhudhuria vikao vyao!

Muungano wa hovyo kabisa huu!
 
Hiyo ni bajeti ya Tanganyika! Ila cha kushangaza humo bungeni utakutana na Wazanzibar nao wanakula posho! Sijui huwa wanawakilisha nini!

Na wakati huo huo, huwezi kuwakuta Watanganyika kwenye lile Baraza lao la Wawakilishi kule Zanzibar wakipokea posho! Au kuhudhuria vikao vyao!

Muungano wa hovyo kabisa huu!
Acheni tule kwa ^njefu^ (plural ya urefu) za kamba zetu!
 
Mtanganyika haruhusiwi kununua ardhi z'bar.
Ila tuna wapemba kibao wameshikiria mahekari na mahekari uko ruvu
 
Kuna wazanzibari kibao wanafanya kazi kwenye Halmashauri zetu, mfano huku Namtumbo wamejaa tele.
 
Muda Utaongea Ila Watu Wamechafukwa Sana Wana Hasira Nyongo Imejaa
 
CCM chama Cha mapinduzii

Ndio washapindua meza.. .. chezeni dance na ndombolo wao Wana msewe.. njuga zinachikicha we acha tu.. ...
 
Mnazidi kutuchanganya tu maana kwa sasa hivi Pemba ina nguvu sana kuliko sehemu nyingine yeyote hapa nchini.
 
Back
Top Bottom