Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Hawako strategic. Wangeifanya milioni moja wangepata hela nyingi, watu wengi wangejitosa. Kuifanya milioni 5 watapa pesa kidogo sana kwa kuwa itakuwa unajilebo wewe fisadi.
 
Gari yenyewe Corolla ya mil 7, na umejipinda pinda hadi ukanunua, registration ya mil 5 ya nini?
Kiwese chenyewe waweka shil 10 elf kila ukifika sheli, watanzania tuache matanuzi.

Hao wa kuweka namba maalum ni wale wa mashangingi ya milioni 200-500, kwao mil 5 ni vijisenti!
hapo kwenye red kiwese chenyewe bado ukiwa kwenye foleni unazima gari
 
Suala ni kwamba mpango huo utaiingizia mapato nchi au ni yale mambo ya kutumia Tshs 20/= halafu unapata Tshs10/=. Hawa wazee wamechoka waachane na haya mambo ya uongozi hiki siyo chanzo cha mapato
 
Suala ni kwamba mpango huo utaiingizia mapato nchi au ni yale mambo ya kutumia Tshs 20/= halafu unapata Tshs10/=
 
Safi kabisa ili watanzania waweze kujionesha moja kwa moja kwa watanzania wenzao kwamba wamebobea katika utandawazi wa dunia ya leo kwa mambo ya kileo na ni wakati mwafaka kwa wazee wetu wasiojiweza angalau hizo 5ml. Ziwapatie mahitaji yao muhimu japo kwa wale walioko kwenye vituo.vilevile ni wakati mzuri kutafakari upya katiba yetu kwenye kipengele cha ujamaa kwani kile kipengele kingine cha kujitegemea ndicho hasa kila uchao kinasafishiwa njia vizuri.
 
Nimeona tangazo la TRA kuwajuza nyie mnaotaka namba za magari za kipekee kuwa mtapashwa kilipia sh mil 5, hii imeakaaje? Naona kama TRA wamekuw over ambitious, nilidhani wangeweka ada ndogo ili hata hizi bodaboda zangu nizitilie namba maalum kama CCM1 etc, how do you look at this anyway?.
 
Kha...! Wakati inajadiliwa ulikuwa wapi? Mbona ilijadiliwa sana humu na bungeni? Kuna mmoja ameshaweka katika gari yake "MUGANYIZI"
 
Back
Top Bottom