Bajeti imewasilishwa; Anayetaka namba maalum kwenye usajili wa Gari 5mil

Nataka ninunue Reginald Mengi , Yusuf Manji, Bakhressa, Dewji, nk nina invest kama 20,000,000 baadae watanitafuta...
 
Kama jina lenu common kwa mfano " Rwechungura" atakayewahi atapata kama unavyo register e-mail vile.

Ila mil 5 ndogo sana nawaambieni wabongo wanavyopenda sifa mtakuja kuniambia after 2 years balaa tupu mjini. Mimi naona wangefanya milioni 10.
 
umeshaambiwa kwa wanaotaka gari kusajiliwa kwa majina yao,sasa kama wewe una gari la mil 7,ukataka uonekane mjini kuwa gari limesajiliwa kwa jina lako ukalipa mil 5,huo ul-fa wako wa kutaka kujionyesha,kuuza nyago,na kutaka kujilinganisha na wale watakaonunua magari ya kifahari wenye pesa zao watakaosajili kwa majina yao,huo ul-fa wa masikini mwenzangu ndo serikali itapata mil 5 kwa kila kichwa!haya mambo sio mageni duniani,ila tuwaachie wenye hela zao, thamani ya gari ikakaribiane na gharama za plate namba,ni ul-fa!mimi naunga mkono hoja yani watanzania wengi hapa watalipia na serikali itapata sana pesa!
But five mill, is too much, hiyo gari umeinunua kwa gharama gani? corola ya 7 mill na plate number ya 5mill?
 
wapi ndama mutoto ya ng'ombe,wapi muzamir katunzi,wapi papa baghdad,wapi papa musofe,wapi chief kiumbe the big boss,wapi kimbau,wapi omary tall,wapi akayesu,wapi papa felician muta,wapi hasheem thabeet supa tolu,wapi muuza nyago na kavitz kako,magari yanayofaa kuwekwa hzo plate no customised ni hummer,vogue,benz v8 biturbo,phantom royce rolls,aston martin,buggati,limousine,jaguar,x5,lamborgine.
 
Swadakta ni bora kubuni mbinu mbadala za kuingiza kipato,kuliko kung'ang'ana na vyanzo vilevile vya siku zote.
 
We can get some finances from this good source of Income. But it will attract only rich people and the Fisads.
 
nakuunga mkono aslimia mia moja!yapo magari ya miaka ya nyuma imara mno na sio makaratasi kama ya sasa.kuchakaa kwa gari ni kutumika kwake,yaani kama limetembea kilometa nyingi.
Tunapokosea ni pale tunapodhani gari lenye miaka mingi ni chakavu! unaweza kukuta gari iiliyotengenezwa mwaka 1999 ina mileage lets say 86,000km na gari iliyotengezwa 2004 ina mileage 250,000km kati ya magari haya mawili lipi chakavu??hii sera ya gari chakavu ni ya kuangalia upya! halafu wenzetu mfano japan hawana haja ya ku damp magari mabovu kwetu maana huwa wana recycle na kuunda mengine au kutumia chuma chakavu kutengeneza vitu vingine!!
 
Ndani ya bajeti mpya, serikali imetangaza rasmi kuwa wamiliki magari wana nafasi ya kuchagua kati ya kuweka jina lake au namba ya gari. Ni mradi mpya hapa nchini unaotumika sana na nchi za ulaya wenye lengo la kuongeza pato la serikali. Mteja wa huduma hii atatakiwa kulipa milioni tano kila baada ya miaka mitatu. Ww unasemaje...changia hoja

Hopeful maafisa wa TRA, watumishi wa mashirika ya Umma kama Ngorongoro, NSSF, PPF Bank Kuu ndio watakuwa walipaji wa hii kodi bila kuwasahau akina Yusuph Manji
 
Zomba

Uko sahihi Kama ni kuilinda mazingira na uchumi simply ni kupiga marufuku mitumba yote kuanzia nguo fridge , engine chakavu na kadhalika watu wanunue vitu vipya. CCM wamechoka kutawala. You can keep on doing comedy. For over 30 years Kila bajeti ikisomwa ni bia,sigara , soda wine na kuongeza PAYE. Why don't they go back na kurudisha kodi ya kichwa which is simple to collect?

Hivi kurudisha JKT bila muafaka wa kijamii and changed structure is more than crazy! It used to make sense wakati elimu ilikuwa bure and there was some control. Leo hii watoto wanalipa Ada from chekechea Hadi Chuo kikuu na hata Ajira rasmi hakuna then why do you go to JKT. Huu ni upumbavu mwingine wa serikali ya CCM. Hili lahitaji mjadala. Kweli CCM ni mabingwa wa kufikiria wakitumia Masaburi ??.
 
sasa hiyo ndo ubunifu sio kuongeza PAYE na lutegemea bia na sigara...kama vipi ttataanza kunywa chimpungu..tuone watakusanya wapi kodi ya bia
 
5Mil ni ndogo sana. Hapa mjini magari yenye plate no binafsi yatakuwa mengi. Wabongo wanahela we acha tu. Serikali ibuni mbini zingine.
 
Naomba kuuliza wadau, sasa ina maana ile tax calculator ya excel inayotolewa na TRA ndio haitumiki tena au inakuwaje?

Kwa anayejua naomba ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom