BAJETI imejaa ulaji wa wakubwa kupitia POSHO,Nitaipinga: MBUNGE WA KISESA { CCM } | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAJETI imejaa ulaji wa wakubwa kupitia POSHO,Nitaipinga: MBUNGE WA KISESA { CCM }

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, Jun 16, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Ndugu wajumbe,
  Katika hali ya kutekeleza maelekezo ya raisi wetu (sikivu) Dr. JK ya wabunge kuisimamia vyema serikali sikivu!, baadhi ya wabunge wa CCM wameapa kutoipitisha bajeti yetu
  "ya kupambana na mfumuko wa bei":  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) ameapa kuipinga bajeti ya Serikali iliyowasilishwa juzi, kwa maelezo kwamba imejaa ulaji wa wakubwa kupitia posho, warsha na safari zao za nje huku mamilioni ya Watanzania masikini wakifa kwa kukosa matibabu.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mpina alisema bajeti hiyo inakiuka azimio la Bunge kwamba kwa kila mwaka wa fedha angalau asilimia 35 itengwe kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha za matumizi ya kawaida ziwe asilimia 65. Lakini Mpina ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi alisema bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, waliipinga kuanzia kwenye Kamati ya Fedha na kuishauri Serikali iibomoe, lakini hawakufanya hivyo.

  Mbunge huyo alisema yuko tayari kufukuzwa CCM akitetea fedha zaidi zitengwe kwa ajili ya miradi ya maendeleo, kwani warsha, sherehe, ununuzi wa samani, magari ya kifahari unaweza kupunguzwa au kuahirishwa ili kuwapa Watanzania maisha bora.

  “Hiki ninachofanya si usaliti kwa chama, kwani ninachotetea ni kukisaidia chama chetu kiweze kutekeleza miradi yenye manufaa kwa wananchi na si kutenga fedha nyingi kwa posho na sherehe,” alisema Mbunge huyo. Akichambua bajeti hiyo, Mpina alisema katika azimio la Bunge iliazimiwa kitengwe kiasi kisichopungua Sh trilioni 2.7 kutoka mapato ya ndani na zielekezwe kutekeleza mpango huo.

  “Hivyo bajeti ambayo imewasilishwa na waziri si sahihi kwa mujibu wa mpango wa maelekezo ya Bunge,” alisema. Akitoa mfano wa ulaji huo, Mbunge huyo alisema mafungu nane tu ya Wizara ya Nishati na Madini na Fedha yameongezwa kiasi cha Sh bilioni 4.8 kwa ajili ya posho na safari za ndani na nje ya nchi, wakati fedha hizo zingepunguzwa na kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

  Alisisitiza kuwa kitendo cha Serikali kutenga Sh trilioni 2.2 badala ya Sh trilioni 2.7 ambayo ni tofauti ya Sh bilioni 500 kugharimia miradi iliyoainishwa katika mpango huo, kumesababisha miradi mingi kutengewa fedha kidogo na mingine mingi kukosa fedha kabisa, hali ambayo alidai inazorotesha utekelezaji na maana ya kuwa na mpango. Mpina alisema kibaya zaidi, katika bajeti hiyo mapato ya ndani yameongezeka hadi Sh trilioni 1.5 huku matumizi ya kawaida yakipanda hadi Sh trilioni 1.9 wakati fedha za maendeleo zikipungua na kuwa Sh bilioni 397.8 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2011/12.

  “Hapa inajidhihirisha kuwa Serikali haina nia ya dhati ya kupunguza matumizi ya kawaida,” alisema Mpina. Alisema kwa kipindi kirefu, imekuwa ikiahidi kupunguza matumizi ya kawaida ili kuongeza kasi ya utoaji huduma na uwekezaji katika sekta zinazokuza uchumi na kupunguza umasikini; lakini hivi sasa pato kuu la Taifa linatumika kuendesha Serikali.

  Mpina alisema wakati Serikali ikiendekeza matumizi makubwa yasiyo na tija, Watanzania wanakufa kwa kukosa huduma za tiba, dawa, waganga, maji safi na salama, elimu bora kutokana na upungufu mkubwa wa madarasa, nyumba za walimu, vifaa vya kufundishia na maabara.

  Pia miundombinu mibovu ya barabara, umeme na reli, ukosefu wa viwanda vya kuongeza thamani kunakosababisha wakulima kuuza mazao yao kwa bei ndogo, hasa pamba, mkonge, korosho na mifugo. Alisema mpango wa maendeleo ni mkataba kati ya wananchi na Serikali, lazima wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi waulinde kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote.

  Alisema kama Serikali ilipata fedha za kufidia benki na wafanyabiashara walioathirika na mtikisiko wa uchumi kwa jumla ya Sh trilioni 1.7 “iweje leo ishindwe kupata Sh bilioni 500 kugharimia yaliyoainishwa katika mpango wa maendeleo?”

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Andrew Chenge alisema ingawa Waziri wa Fedha ameanza kwa mwelekeo mzuri, lakini matumizi ya kawaida ya Serikali yanapaswa kugharimiwa na fedha za ndani.

  Mbali ya kusisitiza bajeti ya maendeleo iongezwe hadi asilimia 35, amesema kama Watanzania wanataka uchumi ukue na kuondoka na umasikini, lazima kilimo kibadilishwe na kiwe chenye tija. “Mwelekeo mzuri, wameanza vizuri,” alisema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM) aliyepata kuwa Waziri katika Awamu ya Nne. Mwenyekiti huyo aliyechaguliwa hivi karibuni kuongoza Kamati hiyo ya Bunge, alisema licha ya kuanza vyema yapo mambo ambayo hayakumridhisha katika bajeti.

  “Lazima tufanye matumizi ya kawaida kwa kutumia mapato ya ndani. Hili tulilizungumza katika Kamati yetu wakati wa mashauriano na Serikali. Lakini tulisema kwa kuwa Waziri ni mgeni, ndio kwanza ameteuliwa, tumpe muda, ajipange hadi bajeti ya 2013/14,” alisema Chenge

  . Alisema ni vyema pia sekta binafsi ikawekewa mazingira mazuri ili kushawishi ukuaji wa uchumi; huku akieleza kwamba tayari kampuni za bia na sigara zimeeleza kusikitishwa na ongezeko la bei katika bidhaa zao.

  Kuhusu kilimo, alisema lazima Serikali isaidie kuweka miundombinu bora ya kilimo na kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote ili wakulima waweze kutoa mazao yao mashambani na kuyapeleka sokoni.

  Alisema si hivyo tu, bajeti inapaswa kulenga watu wa vijijini ambako ndiko waliko asilimia kubwa ambao ni wakulima, ili kuzalisha kwa wingi na kuiwezesha nchi kuwa na uchumi imara. Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema baadhi ya maeneo, Serikali haijafanya vizuri katika bajeti ikiwamo kutoa nafuu ya kodi kwa kampuni kubwa zikiwamo za madini.

  Alisema unafuu huo wa kodi haufai kwa kampuni na viwanda vikubwa, wakati wanapaswa kulipa kodi kubwa. Aidha, Sendeka alilalamikia kiwango kidogo kilichotengwa kwa umeme, Sh bilioni 400, akisema hazitoshelezi kwa sababu ya gharama kubwa za kukodi mitambo ya kuzalisha umeme zinazobebwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

  Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alitaka Serikali itaje kiasi cha mishahara kilichoongezwa, badala ya kuachiwa waziri wa kisekta, kwa sababu hilo ni moja ya maeneo yanayohitaji uzito.
  Aidha, alilalamikia matumizi kuwa makubwa, kutofutwa kwa posho, mfumuko wa bei akisema umejikita katika kuagiza chakula nje na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji katika mabonde makubwa nchini. Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto alisema bajeti hiyo imejikita zaidi katika mikopo na madeni.
  Katika hotuba yake ya Bajeti, Dk Mgimwa alisema katika bajeti hiyo yenye kubeba Sh trilioni 15, asilimia 70 itakuwa kwa matumizi ya kawaida na asilimia 30 kwa matumizi ya maendeleo.

  Wakati hayo yakijiri, wabunge wa CCM walikuwa na kikao jana asubuhi; na miongoni mwao walieleza kutoridhishwa ni kutofutwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika malighafi za viwanda vya nguo na mavazi.

  Mmoja wa wabunge hao wa CCM, alieleza kuwa licha ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda kamati maalumu ya wadau wa sekta ya pamba na viwanda vyake, mapendekezo ya kamati hiyo hakuyazingatiwa katika bajeti.

  Mapendekezo yalikuwa ni viwanda kupewa msamaha wa VAT kwenye bidhaa za nguo na mavazi, na ilielezwa kuwa hilo linawezekana kwa sababu kiwango kinachokusanywa sasa ni karibu Sh bilioni moja kwa mwaka.

  Sosi: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania
   
 2. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa CCM anainga bajeti iliyoandaliwa na wana CCM! kweli tanzania nchi ya kidemokrasia.
   
 3. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mbona hakusain fomu ya zittooo........?
  Wale waleeeeee.....
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Siasa ni mchezo wa aina yake!
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Amekurupuka toka usingizini akaropoka hayo maneno kama kawaida ya magamba!
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu huu ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa na JK kuwa wabunge wa ccm lazima waisimamie serikali.
   
 7. Mufa

  Mufa Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anatafuta umaarufu mnafiki tungengemuelewa kama angesaini kumtoa waziri mkuu
   
 8. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Heshimu waliokuzidi umri kijana. usiwaite waheshimiwa wanafiki
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuona ccm inaangukia kisogo ameamua kuwekeza kwa wananchi kwaajili 2015 ikizingatiwa umri wake bado ni Mdogo anamuonea wivu deo filikunjombe kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Ha ha "mbavu zangu"
   
 10. Ansah Miles

  Ansah Miles JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hana lolote mnafiki tu Huyu
   
 11. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mtake radhi mweshimiwa wetu!
   
 12. W

  Welu JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  We aache uongo tangu lini CCM mliacha kuimba wimbo mtamu hata mkitoka usingizini usemao ndiyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!
   
 13. N

  Njaare JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ataishia tu kama Kigwangala. Kigwangala alifuta hoja yake kwa madai kuwa serikali sikivu ya chama chake imesikia malalamiko ya wakulima wa pamba hivyo anaiunga mkono. Mpaka leo wakulima wa pamba wanasota. Huyu naye atasema serikali imemsikia hivyo anaiunga mkono bajeti mia kwa mia.
   
 14. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mwacheni akifanyie kazi alichokisema msimvunje moyo jamani, kuna mantiki kubwa tu na hao kin chadema watamsaidia kufikisha ujumbe. whether anataka umaarufu si mbaya kwani hakuna anayetafuta umaarufu ambaye hupita barabara nyeupe lazima akanyage watu ndipo apate umaarufu.
   
 15. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mh.Mpina anazo hoja za msingi ni lazima tumsupport hata kama imani zeru ni tofauti na kwa hata akina ZZK na wengineo wa cdm hataunga mkono hoja ya bajeti ni mtaji wa chama na siyo kutoa negative and unfounded arguments against the MP.
   
 16. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ni mnafiki mbona wakati wa ndiooo hakatai ...wanapiga kalele halafu naunga mkono hoja ujinga gani huo...wabunge wa ccm ni wanafiki hebu fikiria wanampigia makofi waziri akitaja nchi wahisani aibu gani hii na yeye ni mmoja wapo wanafurahia kuomba

   
 17. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hoja yako haina mashiko, sasa ndio ameanza mmpe support. kwani walionanza walianzaje? walizaliwa wanaweza na kama ndio hivyo mbona wapinzani wengi walitoka CCM mbona hamuwabezi na kuwafukuza???
   
 18. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ni kweli kaka, watu humu kuna wengine hawafikirii kwa undani.
   
 19. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  historia inamuhukumu hakuna hata siku moja atafanya anachosema ni kutafuta umaarufu wa muda mfupi wako wapi kina kilango ...anajaribu kuiga cdm ....mwiso wa siku utasikia wabunge wote ccm tukutane ukumbi wa pius msekwa....wakitoka huko ndiooooooooooooooo.....akiona aibu asiingie atoke wakati wa kuhitimisha hoja....afanye kama deo au lugola kukataa movu kivitendo sio mdomo.
  huyo sio mbunge mpya ni wa muda mrefu anajuwa mengi ukiona ya ccm huyawezi unahamia kwingine


   
 20. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Townsend mimi sina data zake za nyuma, kama wewe unazo na unasema kurefaa huko nyuma alifanya nini then you have right to say. Mimi ndo kwanza nimemsikia hivyo nilitaka kumpa chance . .. .
   
Loading...