Bajeti iliyowasilishwa haijali Maskini wa ukweli hata kidogo

Nelembe

Member
Jun 18, 2012
7
1
:hand:Wana JF; Binafsi nimesikitishwa sana na Bajiti ya Mheshimiwa Dokta......... ambayo haikuzingatia kuwa kuna watu ambao ni walalahoi pasee! Angalia inavyotaka kodi iongezwe kwenye mawasiliano (Simu) ambayo wapika Vitumbua, Mama Ntilie, Wamachinga nk wanamiliki Simu ambazo wamenunu za Mchina ili kuwasaidia katika kufanya biashara zao. Senti wanazopata watu hawa ni "Hand to Mouth", sasa watalazimika kulipia mawasiliano kwa gharama kubwa! Wanaochota Madini kule Shinyanga, Geita, Arusha nk, Bajeti ya Mheshimiwa haiwasumbui hata kwa Senti tano! Wafanya biashara wanaopata hadi Shilingi Millioni tatu (3,000,000/=), Bajeti ya Dokta haiwasumbui, acha wapumuzike! Mfanyakazi mwenye Mshara unaofikia Millioni Mbili, PAYE anayotozwa kila mwezi ni zaidi ya Laki Sita! Jamani mimi nalazimika kukubaliana na wazo la Mstahiki Meya wa Jiji kubwa hapa Tanzania aliposema wengine labda wanafikiria kwa kutumia "Makalio"! Wana JF; tafakali, chukua hatua!
 
ccm wameanza sarakasi, R.Ndansa anaunga mkono 100% budget, lakini analalamika bei ya pamba, matumizi hewa, miradi ya mabilioni imekuwa kama vichochoro za pesa kupitia, anafannanisha takukuru na vinyago vya kwenye majaruba, ndege wanakuja watua kwenye mabega kama hakitikisiki wanaanza kula mpunga.

pia anaponda usalama wa taifa.

Ajabu kweli, utaungaje mkono 100% arafu unalalamika zaidi ya 90%. aibu tupu
 
hi ndio bongo falsafa ya mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho hata kile kidogo atanyang'anywa naanza kuiona ikifanya kazi
 
Back
Top Bottom