Bajeti iliyosomwa juzi siyo tu ni hewa bali pia hata mchakato wenyewe wa bajeti umejaa ulaghai. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti iliyosomwa juzi siyo tu ni hewa bali pia hata mchakato wenyewe wa bajeti umejaa ulaghai.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jun 11, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jana waziri wa fedha Mkullo alisikika akikanusha madai yaliyotolewa na mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe, aliyeelezea ya kwamba waziri alitoa bajeti hewa. Pamoja na kauli yake hiyo, bado naungana na Zitto kusema kwamba bajeti aliyowasilisha bungeni hivi majuzi ni hewa. Hii inatokana na ukweli kwamba katika hali halisi bajeti inazo pande mbili; nazo ni matumizi na vyanzo vya matumizi hayo. Sifa mojawapo ya msingi ya bajeti ni kwamba pande hizo mbili zinapashwa zilingane. Jambo la ajabu ni kwamba mpaka anawasilisha bajeti yake bungeni, waziri Mkullo alikuwa hajawa na uhakika ni kiasi ngani cha fedha zitapatikana kutokana na vyanzo vilivyopo. Ukweli huo unadhihilishwa na mambo mawili; kwanza kwa kauli yake mwenyewe waziri Mkullo alidhibitisha ya kuwa mafuto ya petroli yanatozwa tozo 20 na kwamba serikali ilikuwa bado haijaamua ni tozo zipi kati ya hizo itazipunguza ili kushusha bei ya mafuta. Hivyo kwakuwa kupunguzwa kwa tozo hizo bila shaka kutahadhiri upande wa mapato wa bajeti husika ni dhahili pande hizo mbili ziyo linganifu. Jambo linaloifanya iwe hewa. Lakini pengine baya zaidi, kulingana na ratiba iliyotolewa na katibu wa bunge, hiyo bajeti hewa imepangwa kupitishwa na bunge kabla hata ufafanuzi wa ni tozo zipi zitapunguzwa kwenye bei ya petroli. Katika hali hiyo mtu anajiuliza nini maana ya bunge! Mbali na hayo hata muswanda wa kuruhusu serikali kuanza kutumia fedha zilizopo kwenye bajeti umepangwa kupitishwa kabla ya kuanza kujadili makisio ya wizara moja moja. Sasa mtu anajiuliza baada ya kupitisha bajeti na ikaanza kutumika kwanini bunge liendelea kuteketeza mabilioni ya fedha kujadili makisio ya wizara wakati makisio hayo tayari yalikwishapitishwa na bunge lenyewe!
   
 2. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni sahihi haina kitu kabisaa kwa mlalahoi ,bei ya mafuta itafika 3000/= muda si mrefu ,kilichofanyika pale ni porojo za mkulo si bageti,watanzania sijui tutaamka lini ,yaani tunadanganywa kama watoto ,
   
Loading...