Bajeti Ichochee,Ichachue na Kutekenya Uchumi

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
702
500
Mabadiriko chanya katika taifa lolote lile uambatana na maumivu..Wana wa Israel walipotoka Misri kwenda nchi ya ahadi {yenye asali na maziwa} hawakutembea kwenye tambalale..Walivuka milima na mabonde,walivuka bahari na kupigana vita hata mwisho wa safari yao.

Taifa letu ni tajiri sana..Limejaa kila aina ya utajiri,Tumepofushwa sana na wageni waliokuja na kupata fulsa ya kututawala..Tukatuvisha ufahamu hasi juu ya utajiri wetu wa fikra na maliasiri.Uchumi wetu hauwezi kuwa imara ikiwa tutawategemea watu toka nje wauendeshe,wautawale,wausimamie..Uwekezaji wa ndani unanihusisha mimi na wewe ni muhimu sana katika maendeleo endelevu ya taifa letu sasa na baadae.

Utekelezwaji wa bajeti ya Wizara ya Fedha unategemea sana mapato,Ni aibu kwetu sote kutegemea misaada.Hivyo ukusanyaji wa kodi,tozo toka vyanzo vya ndani vitapewa kipaumbele pasipo shaka.Hata hivyo ni rai ya kuwa taasisi za umma zenye athari mseto katika utekenyaji wa uchumi zishiriki kikamirifu ili kuwezesha mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara,wawekezaji,wajasiliamali ili kufikia malengo,kiu,nia,dhamira,ndoto na maono .

Uchocheaji tanuru la uchumi wa taifa letu ufanyike kimkakati na kwa makusudi ili kukidhi haja na matakwa mtambuka leo,kesho na keshokutwa.Ukamuaji wa maziwa uendane na malisho stahiki apatayo ngombe mzazi..tusikamue hata kumfanya ndama akose maziwa ya kunyonya na kuishi.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,515
2,000
Wana wa Israel walipotoka Misri kwenda nchi ya ahadi {yenye asali na maziwa} hawakutembea kwenye tambalale..Walivuka milima na mabonde,walivuka bahari na kupigana vita hata mwisho wa safari yao.

wafrika acheni uongo na ujinga wa kwenye biblia,hao wanaojiita waisraeli hawajawahi kufanya hiyo safari(exodus) kutoka misri sijui!!!
ni uongo wa wazungu walioupenyeza kwenye kitabu chao walichokiita biblia
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
33,280
2,000
Ni jukumu la wachumi kutueleza njia bora za kuyafikia haya.Wachumi waliosomeshwa na kodi za wananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom