Bajeti bomu yastukiwa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti bomu yastukiwa!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lole Gwakisa, Dec 7, 2010.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wafadhili na wabia wa maendeleo nchini wamehoji kutokuwepo umakini katika kutayarisha Bajeti ya mwaka wa fedha 2010/11.
  Afisa mmoja wa ubalozi wa Norway MrSvein Baera, ameenda mbali zaidi na kudai,"poor budget preparations.....underminethe credibility of the budget as an effective policy and planning tool".(THE CITIZEN-7th Dec 2010)
  Kwa lugha rahisi wafadhili hawa wanasema uswahili umezidi
  Mfano waliotoa ni kuwa bajeti iliyosomwa na kupitishwa Bungeni ni tofauti kabisa na ile iliyopelekwa IMF.
  Vilevile wanadai makadirio ya mapato kwa mwaka wa bajeti ni malubwa kulikp ukweli wenyewe.
  Mbaya zaidi,wanadai,matumizi ya Serikali ni makubwa kuliko mapato hivyo kuingia katika deficit.

  Mfano halisi,katika Bajeti TRA walipewa malengo ya kukusanya 2.9 Trilioni kwa miezi ya July/Sept,fedha iliyokusanywa ni 1.3Trl. Matumizi ndo usiseme,yanagonga 1.9Trl kipindi hicho hicho.
  Mhe.Mkullo Vipi tena?
   
 2. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Uchakachuaji umo kwenye damu ya hawa viongozi. Sasa wanataka kuwafisadi hata wafadhiri wakidhani ni majuha kumbe wenzao wanasoma between the lines
   
 3. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Full Sanaa katika bandari ya salama then utasikia mtu anakwambia NIAMINI.....hakuna kuaminiana hapa ni Kukaa chonjo 24/7 koz kuanzia Serikali mpk wananchi ni USANII.....Utaona hakuna atakaechukuliwa Hatua......koz wote wanalijua chezo hilo...walitaka wahisani wachangae zaidi ili wapige cha juu.....
   
 4. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkullo kamwambia mwenyekiti wa wahisani....'hilo linazungumzika'
  Serikali hii fulu magumashi....
   
 5. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka kuamini haka kamchezo kachafu ndo wamekacheza kwenye bajeti hii na kushtukiwa ? Oooh puhliiizzz...
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Lole Gwakisa ni ukweli usiopingika kwamba sanaa hizi zitaendelea for the next five years, Watanzania walikuwa na chance pekee Oct30 and they did burn it. Na huyo mkulo naye vile vile ni sanaa tu. Anywayz tunaambiwa kwamba watanzania wengi ndiyo wanataka serikali ya namna hii!!!!!!!! Hebu imagine pamoja na upuuzi wote huu humsikii predidaa hata siku moja akisisitiza kubana matumizi ya serikali. Huyo PM wake badala ya kuzungumzia policies anaibuka na kukataa shangingi!! Inakatisha tamaa mpaka basi, kuna wakati unaweza kujikuta unakufuru kwamba enywayz hayanihusu!!!!!
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hii ni aibu kubwa kwa serikali kuonesha ujanja ujanja wa kuwa na bajeti mbili moja iliyopitishwa na bunge na nyingine ya kuombea hela kwa wafadhili!! Sasa kama serikali yenyewe inaonesha mfano mbaya wa kuwa na bajeti mbili , wananchi walipakodi nao kwanini wasiwe na vitabu viwili vya risiti madukani mwao kama njia ya kukwepa kodi?
   
 8. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Natamani sana kujua walipeleka budget gani huko IMF na kwa wahisani. Halafu nifanye comparison na budget waliyopitisha bungeni. Ili nipate picha halisi ya nini walikuwa wanaficha kwa wahisani au kwa wabunge au kwa wananchi kwa ujumla.

  Na ni nani aliandaa ile budget ilioenda kwa wahisani; Ni Mkulo pekeake au Baraza zima la mawaziri lilihusika?

  It's so disgusting. No wonder nchi inakopa from commercial banks!
   
 9. j

  jmisana Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio mchezo wao kila mwaka za mwizi arobaini na hii ndo 40 yao wameshikwa hao!AIBU.Wamechakachua bajeti ili wapate fedha iliyochakachua matokeo ya uchaguzi uliopita Nov 2010.
   
 10. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na hoja. Hivi wanatumia kigezo gani kuwataka TRA wakusanye 2.9 trillion/mwezi na kwa kiwango gani wanawashirikisha TRA katika kufanya makadirio?? Kwa jinsi nijuavyo kwa muda mrefu sana, nadhani tangu July 2008, TRA hawajafikia lengo la makusanyo kwa kuangalia jumla ya kodi zote zinazokusanywa. Mtu anaweza kufikiria labda TRA hawafanyi kazi yao lakini huenda pia makadirio ni makubwa sana kulingana na hali halisi.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Umenena Mkuu Ndinani, inabidi Serikali iliangalie hili kwa makini, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!
  Hata hivyo serikali ijitahidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kuondokana na hali hii ya deficit.
   
 12. N

  Nightangale JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiongozi ukifikiria sana unaweza kufanya mambo ya ajabu sana.
  Binafsi nimechoshwa na mabo ya hii serikali. Acha watu waukane uraia wao!
   
Loading...