Bajeti 2021/22: Kodi ya uzalendo ni kaa la moto. Kila laini ya simu itakatwa Sh. 100 kila siku

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,411
2,000
Mapendekezo ya bajeti ya 2021/2022 ni kwamba moja ya vyanzo vya fedha iwe ni kodi ya laini za simu.

Kila laini ya simu kwa mujibu wa mapendekezo yaliyosomwa na waziri wa fedha itakatwa kati ya Tshs 10/= mpk Tshs 100/= kwa kila siku. Bila kusahau VAT na makato mengine yaliyokuwepo yataendelea.

Yaani wabunge ndiyo wataamuua iwe kiasi gani. Wakiamua tukatwe Tshs 10/= sawa wakiamua Tshs 80/= sawa ama wakiamua Tshs 100/= sawa. Kwa kifupi ni kwamba wabunge watapendekeza kiwango cha kutoza kisichopungua Tshs 10/= lkn pia hakitazidi Tshs 100/=.

Kwa kia siku, haijalishi mtumiaji anaumwa, yuko mahabusu, yuko labour, anauguza ama hatumii hiyo laini atakatwa hicho kiasi.

Ukiweka buku, kabla hujapiga ama hujanunua kifurushi wanakata Tshs 100 yao bila kusahau VAT. Kama hujakatwa kwa muda wa wiki 2 kwasabb hujatumia laini kwa wiki hizo 2 na laini ilikuwa haina kifurush chochote Wala mobile money, basi ukiweka buku yote wanachukuwa na bado unakuwa na deni la Tshs 400/= pamoja na VAT.

Maana yake kwa kutotumia laini wiki 2 (siku 14) unakuwa na deni la Tshs 100/= × 14 = 1,400/=.

Usipoitumia laini kwa wiki 3 ni bora ukasajiri nyingine tu.


Hiyo ndiyo Kodi ya uzalendo aliyoipigia kelele mbunge Zungu na kukubaliwa na waziri Mwigulu.

Tuna mali chungu nzima:
  • Madini ya kila aina,
  • Gesi za kila aina, mpk Helium, .
  • Wanyama pori,
  • Mbuga za wanyama,
  • Misitu,
  • Bahari
  • Bandari,
  • Mafuta,
  • Makaa ya mawe,
  • Mlima mrefu kuliko yote Afrika

Yoote haya yameshindwa kuwa vyanzo bora vya kodi hadi wanakuja kuchukua Kodi ya laini? Tena sh 100/= kwa siku?
 

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
980
1,000
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua.
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
2,018
2,000
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua
jaribu kutumia akili ulizobarikiwa japo robo ndugu

Kwasababu una kauwezo ka kubadilisha mboga ndio unaona maisha umepatia hujali kabisa yule mpiga debe anayepata sh Mia kwa kila daladala

Kwa dalaladala kumi buku hapo

Ana familia inamwangalia

Acha jeuri mzee baba ipo siku utaikosa hio Mia ya kulipia na upo kwenye shida ndio utakumbuka huu upupu hapo!

Povuuuuuuuu😤😤😤
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
2,018
2,000
Kuna wanasiasa uchwara ambao wakipata teuzi na kamshahara ka kubadilisha mboga basi anaona shida kwake kwishney anasahau mbaka kazi aliyotumwa pale kuwapigania wananchi.

Wapuuzi kabisa hawa jamaa sijui hi nchi Kama tutafika aisee kila siku wanatutungia Sheria sisi wa chini na hawajali sababu wao haziwahusu.

So sad!😥😥
 

Teknologist

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
1,240
2,000
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua
Hiyo vocha bei itakuwa na value added tax,
ukiichakachua lazima iwe kama hivi kimfano

8GB - Tshs 20,000
8GB........................Tshs 18500
VAT.........................Tshs 500
Total.......................Tshs 20,000

Au sijui.............
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
12,091
2,000
Acheni kulalamika ovyo tutafute pesa tulipe kodi nchi ipate maendeleo wenzetu wana kodi mpaka 45% lakini wanalipa sisi Tsh 100 tena inaweza iwe Tsh20 watu mnashinda mnaliaaaaaa bas tumieni tu barua
Wala kodi wanalipa hiyo percentage lakini sii u aona walivyo fanya nchini mwao...hela inatumika ipasavyo. Elimu bure mpaka chuo kikuu. Health care ya ukweli, barabara za ukweli.

Tatizo sio kulipa kodi tatizo hiyo hela inatumikaje
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,277
2,000
Waziri Wa Fedha kwa hii bajeti yake ya kipuuzi puuzi, sijui wakulima wa umwagiliaji waongezewe kodi mara hii kodi ya uzalendo ya laini za simu, anatakiwa akapimwe Covid 19 kwa kipimo cha China.

Mwiguli anamfanyia figisu SSH za kisomi, na anauchafua uongozi wa SSH ili achukiwe na wananchi, na kila dalili zinaonesha huyu anautaka Urais 2025.

CCM wajipange wapangike, kuanzia 2015 walivyo wavuruga wananchi kwa hali ngumu ya maisha, kuiba kura na kujipitisha bila kupingwa, kutapeli wafanya biashara, kutukana wananchi, kuharibu biashara, wastaafu kwa upande wao, walimu nao kukosa kazi, vijana ajira ngumu, kuua na kuteka, kubambikiza kesi na kodi, kugeuza bunge kuwa genge la kahawa.. 2025 itakua kasheshe hasa nchi ikipata Katiba mpya.

#Mama Samia amka bado mapema Mama, Mwigulu hakufai kabisa.
 

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,107
2,000
Dah! Ndiyo kufunga mkanda huko? Chuchukulia mfano wewe ni mfanyakazi au mfanyabiashara - umeshakatwa kodi na bado unaendelea kukatwa kodi kwa hela ambayo tayari umeshakatwa kodi? Sielewi hapa, labda mwenye uelewa anifafanulie, tafadhari.
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,011
2,000
jaribu kutumia akili ulizobarikiwa japo robo ndugu
Kwasababu unakauwezo ka kubadilisha mboga ndio unaona maisha umepatia hujali kabisa yule mpiga debe anayepata sh Mia kwa kila daladala
Kwa dalaladala kumi buku hapo
Ana familia inamwangalia
Acha jeuri mzee baba ipo siku utaikosa hio Mia ya kulipia na upo kwenye shida ndio utakumbuka huu upupu hapo!

Povuuuuuuuu😤😤😤
kulingana na urahisishaji wa maisha unaofanywa na hizi simu TZS100 ITS NOT A BIG DEAL WATU WATALIPA MSIANZE KUWATISHA. TUMETOKA MBALI SANA NA HIZI SIMU. NCHI ZINGINE WANALIPISHA ZAIDI YA PALE. AAH WATU WATALIPA KAMA WANAWEZA KUSUBSCRIBE KWENYE HUDUMA ZA MIZIKI,SOKA NA NYINGINE NYINGI WATAWEZA KULIPA HIYO TZS100/DY USITIE SHAKA MTZ
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,171
2,000
Mambo mengine kabla atujafanya tuige kwa wenzetu kwa kutumia wataalamu waliyopata elimu ya kodi kutoka nchi za wenzetu.

I am all for taxation but not innovation za kijinga kama hizi ambazo no one in the world is applying.

Ukisoma JF jinsi wanavyopamba kodi za ulaya na walivyokuwa wanamponda Magufuli na TRA wakati wa zama zake utadhani jamaa alikuwa shetani.

Unabaki unajiuliza hivi hawa jamaa wanafahamu income tax za Europe nchi kama UK kama wewe ni accountant kuna tozo zingine ukiziona unaweza sema dah sasa huu uonevu. Kasheshe sasa hizo tozo za Scandavian countries wale majamaa ndio wanauwa.

Kodi watanzania bado kuzielewa na kuzikubali na hatuna wataalamu wa kutafuta vyanzo bila ya kuuwa biashara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom