Bajeti 2020/21 ni sh tril 34.9: Waziri Mapango atoa mwelekeo huku hakuna nyongeza ya mishahara, pesa inaenda kwenye reli, umeme na uchaguzi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
SERIKALI imesema mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2020/21 ni kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/17 hadi 2020/21.

Vipaumbele hivyo ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu, uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji.

Vingine ni kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Mpango ambalo eneo hilo limelenga kuboresha ufuatiliaji, tathimini na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mpango ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo na taasisi za utekelezaji wa mpango.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango leo jijini Dodoma wakati akiwasilisha mapendekezo ya serikali ya mpango wa maendeleo ya Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali mwaka 2020/21.

Dk Mpango amesema miradi itakayotekelezwa katika eneo ka kukuza uchumi wa viwanda ni kujenga viwanda vingi vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini zikiwemo kilimo, madini na gesi asilia ili kukuza mnyororo wa thamani.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia, uanzishwaji na utekelezaji wa kanda maalum za kiuchumi na kongane za viwanda pamoja na viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo, uvuvi na mifugo na kuongeza thamani ya madini.

" Kwenye kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu ni miradi inayotekelezwa kwenye eneo hilo ambayo imelenga kuboresha upatikanaji wa elimu, afya bora, ujuzi na huduma za maji safi na salama.

Pia tumepanga kuendeleza ujenzi na ukarabati sa miundombinu ikijimuisha miundombinu ya nishati, usafirishaji, ununuzi na ukarabati wa ndege, meli na vivuko. Hapa ndio unapoona tumeanzisha miradi ya kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere, kuboresha shirika la ndege kwa kununua ndege mpya 11 pamoja na ujenzi wa reli ya kisiasa ya Standard Gauge," Amesema Waziri Mpango.

Akizungumzia tathimini ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2019/20, Dk Mpango amesema jumla ya Sh trilioni 12.25 zilitengwa kugharamia miradi ya maendeleo ambapo Sh trilioni 9.24 zilikua fedha za ndani na Sh trilioni 2.51 ni fedha za nje.

Kuhusu mwenendo wa hali ya uchumi nchini, Waziri Mpango amesema mapendekezo ya serikali ya mpango wa maendeleo wa Taifa na kiwango cha ukomo wa bajeti ya serikali mwa mwaka 2020/21 ni ya mwisho katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/17 - 2020/21 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda katika kuchochea mageuzi ya uchumi wa watu.

" Mapendekezo yamezingatia ilani ya CCM ya 2015, katika kipindi hicho cha utekelezaji wa mpango mafanikio makubwa yamepatikana kupitia Rais Dk John Magufuli ambapo katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 pato la Taifa limekua kwa wastani wa asilimia 6.9 kwa mwaka.

Ukuaji huu umechochewa na sekta ya ujenzi kufuatia kuongezeka kwa uwekezaji hususani katika miundombinu ya barabara, reli na viwanja vya ndege na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za maji, kuimarika kwa usafirishaji, uzalishaji wa madini na kuongezeka kwa mazao ya kilimo, " Amesema Dk Mpango.

Akizungumzia sera za mapato na matumizi kwa mwaka 2020/21, Dk Mpango amesema mapato ya serikali yanatarajiwa kuongezeka na hivyo kuwez kugharamia miradi mikubwa ya kimkakati.

Amesema serikali itaendelea kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria ya bajeti sura 439, sheria ya fedha za umma sura 348 lengo likiwa kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma na kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye miradi mikubwa ya kimkakati na muhimu.

Waziri Mpango amesema kwa kuzingatia sera za bajeti kwa mwaka 2020/21 Sh trilioni 34.88 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika. Mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa bajeti ya 2020/21 yamezingatia mahitaji halisi ya ugharamiaji wa miradi mikubwa, ulipaji mishahara na deni la serikali pamoja na utekelezaji wa vipaumbele vya Taifa.

Kwa mwaka 2020/21 serikali imepanga kutumia jumla ya Sh trilioni 34.88 kaa matumizi ya kawaida na maendeleo, kati ya fedha hizo Sh trilioni 21.98 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh trilioni 12.90 kwa ajili ya maendeleo sawa na asilimia 37.0 ya bajeti yote.

Uwasilishaji wa taarifa hiyo umehudhuriwa na Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Mhe Job Ndugai, Mawaziri, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Wabunge pamoja na Wandishi wa Habari.
 
Hawa jamaa ni lazima uwasifu kwa uthubutu na ujasiri wao, hata kama hukubaliani nao.

Hivyo vikura (vingapi)?, hata laki tatu havifiki ya nini viwanyime usingizi?

Kwanza hata hao 300,000, kila mmoja wao angempata mwenzake wa kumshawishi asiwapigie kura, bado hilo lisingebadili chochote katika mipango yao ya ushindi!

Lakini hata ubinaadam tu, na huruma juu ya hawa watumishi hakuna? Kwani makosa yao ni nini hasa hata wasistahiri angalao kupewa motisha wafanye juhudi zaidi huko kazini ili mipango ya serikali ifane - hili nalo sio mhimu kwao?

Je, na hao huko walioko kwenye 'dola' hali zao nao zikoje, bila shaka wao marupurupu ni ya kumwaga, hata kama hawayatangazi kwa uwazi!
 
Unadhani Basi watumishi wanafanya kazi kwa bidii siku hizi

Wanafanya kwa mazoea tu

Utaleta kiongozi atawakaripia watamsikiliza akimaliza wanafuta mavumbi wanaendelea na maisha yao ya kila siku .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaambiwa kila siku njia ya mwongo Ni fupi

Mwaka 2016/17 wimbo ulikuwa hatupandishi mishahara kwa sababu ya uhakiki (watumishi wakavumilia)

2017/18 Wakasema tunapandisha kwanza madaraja,na kumalizia uhakiki, lakini pia Wakasema tume ya kurekebisha mishahara chini ya mzee MKUCHIKA itakamilisha kazi yake ili kuweka uwiano sawa wa mishahara kwa watumishi wa umma (watumishi wakavumilia)

2018/19 watumishi wakaambiwa kwa macho makavu kabisa kwamba MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU,HAKUNA NYONGEZA YA MISHAHARA MPAKA MIRADI MIKUBWA IKAMILIKE (mfano, Nyerere Hydropower Project,ambayo nasikia mpaka kufikia kilele Cha uzalishaji wa megawatt 2115 ni mwaka 2036)

2019/20 Zile habari za mida hakiki kwanza zikapotelea kusikojulikana,sababu pekee ya kutowapatia watumishi wa umma haki zao,imekuwa miradi ya maendeleo kana kwamba mzee KIKWETE hakuwa anajenga miradi ya maendeleo...

Na sasa 2020/21 Kama kweli hakuna NYONGEZA ya mishahara kwa watumishi wa umma,basi itakuwa imekamilika miaka 5 bila NYONGEZA ya mishahara wala kupandishwa madaraja (kwa walio wengi)

Na baada ya hapo wajiandae kwa maumivu zaidi kwani hakuna uchaguzi wa kufanya mzee atishike na kuongeza mishahara hiyo,zaidi zaidi wajiandae na kile kikokotoo kilichowekwa "pending" Cha mtu kupewa 25% ya pesa zako zote, yawezekana bima pia itakuja na mabadiliko makubwa kwa kuongeza makato, michango ya hifadhi ya jamii natabiri pia inaweza kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha kuchangia...

Ni hayo tu,tuwe na asubuhi njema kwa hisani ya bajeti,wengine tuendelee na kilimo cha matikiti tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watumishi hawapigi kura kwa kuangalia haki zao pekee.

Mwingine anampigia kura mgombea kwasababu ni homeboy, dini yake, kabila au hapendi mgombea anayeshindana naye.

Mwingine ilimradi anaweza kula, ameoa na anaweza kukopesheka kwa Muha au kwa mangi anaona hiyo ndio haki na kwamba ndio maisha yake.

Mwingine ni shabiki tu maandazi ni ilimradi upepo unakoelekea ndiko na yeye anaenda.

Mwingine hana maisha binafsi ( maisha yake yanaathiriwa sana na influencers ) hivyo atampigia kura mgombea yoyote atayepigiwa Debe na na aidha Wema Sepev, Harmoize, Diamond, Gwajima, Kakobe, Mwamposa au the likes.

Mwingine ilimradi kapewa hata buku, tshirt, kafadhili ligi ya jogoo kijini au kawanunulia solar zahanati ya mtaa au kanunua pakti ya chumvi hilo tu linatosha kutoa kura.

Mwingine kapewa tu kibarua cha kusimamia uchaguzi anama CCM wanamjali vibaya sana, so kura kama zote
 
Hawa jamaa ni lazima uwasifu kwa uthubutu na ujasiri wao, hata kama hukubaliani nao.

Hivyo vikura (vingapi)?, hata laki tatu havifiki ya nini viwanyime usingizi?

Kwanza hata hao 300,000, kila mmoja wao angempata mwenzake wa kumshawishi asiwapigie kura, bado hilo lisingebadili chochote katika mipango yao ya ushindi!

Lakini hata ubinaadam tu, na huruma juu ya hawa watumishi hakuna? Kwani makosa yao ni nini hasa hata wasistahiri angalao kupewa motisha wafanye juhudi zaidi huko kazini ili mipango ya serikali ifane - hili nalo sio mhimu kwao?

Je, na hao huko walioko kwenye 'dola' hali zao nao zikoje, bila shaka wao marupurupu ni ya kumwaga, hata kama hawayatangazi kwa uwazi!
Watumishi awapendwi awamu hii.Hio miradi yote hadi ikamilike si chini ya Miaka 15 ijayo
 
Tunaambiwa kila siku njia ya mwongo Ni fupi

Mwaka 2016/17 wimbo ulikuwa hatupandishi mishahara kwa sababu ya uhakiki (watumishi wakavumilia)

2017/18 Wakasema tunapandisha kwanza madaraja,na kumalizia uhakiki, lakini pia Wakasema tume ya kurekebisha mishahara chini ya mzee MKUCHIKA itakamilisha kazi yake ili kuweka uwiano sawa wa mishahara kwa watumishi wa umma (watumishi wakavumilia)

2018/19 watumishi wakaambiwa kwa macho makavu kabisa kwamba MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU,HAKUNA NYONGEZA YA MISHAHARA MPAKA MIRADI MIKUBWA IKAMILIKE (mfano, Nyerere Hydropower Project,ambayo nasikia mpaka kufikia kilele Cha uzalishaji wa megawatt 2115 ni mwaka 2036)

2019/20 Zile habari za mida hakiki kwanza zikapotelea kusikojulikana,sababu pekee ya kutowapatia watumishi wa umma haki zao,imekuwa miradi ya maendeleo kana kwamba mzee KIKWETE hakuwa anajenga miradi ya maendeleo...

Na sasa 2020/21 Kama kweli hakuna NYONGEZA ya mishahara kwa watumishi wa umma,basi itakuwa imekamilika miaka 5 bila NYONGEZA ya mishahara wala kupandishwa madaraja (kwa walio wengi)

Na baada ya hapo wajiandae kwa maumivu zaidi kwani hakuna uchaguzi wa kufanya mzee atishike na kuongeza mishahara hiyo,zaidi zaidi wajiandae na kile kikokotoo kilichowekwa "pending" Cha mtu kupewa 25% ya pesa zako zote, yawezekana bima pia itakuja na mabadiliko makubwa kwa kuongeza makato, michango ya hifadhi ya jamii natabiri pia inaweza kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha kuchangia...

Ni hayo tu,tuwe na asubuhi njema kwa hisani ya bajeti,wengine tuendelee na kilimo cha matikiti tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Machinga nao mwisho ni mwaka huu ukipita uchaguzi nao watachagua pa kwnda
 
Hiyo hela wataitoa wapi? Mwaka huu utekelezaji wa bajeti haufiki hata 50% kwa maeneo mengi ya serikali. Hiyo miujiza ya kupata trl. 34 itatoka wapi?
 
Tunaambiwa kila siku njia ya mwongo Ni fupi

Mwaka 2016/17 wimbo ulikuwa hatupandishi mishahara kwa sababu ya uhakiki (watumishi wakavumilia)

2017/18 Wakasema tunapandisha kwanza madaraja,na kumalizia uhakiki, lakini pia Wakasema tume ya kurekebisha mishahara chini ya mzee MKUCHIKA itakamilisha kazi yake ili kuweka uwiano sawa wa mishahara kwa watumishi wa umma (watumishi wakavumilia)

2018/19 watumishi wakaambiwa kwa macho makavu kabisa kwamba MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU,HAKUNA NYONGEZA YA MISHAHARA MPAKA MIRADI MIKUBWA IKAMILIKE (mfano, Nyerere Hydropower Project,ambayo nasikia mpaka kufikia kilele Cha uzalishaji wa megawatt 2115 ni mwaka 2036)

2019/20 Zile habari za mida hakiki kwanza zikapotelea kusikojulikana,sababu pekee ya kutowapatia watumishi wa umma haki zao,imekuwa miradi ya maendeleo kana kwamba mzee KIKWETE hakuwa anajenga miradi ya maendeleo...

Na sasa 2020/21 Kama kweli hakuna NYONGEZA ya mishahara kwa watumishi wa umma,basi itakuwa imekamilika miaka 5 bila NYONGEZA ya mishahara wala kupandishwa madaraja (kwa walio wengi)

Na baada ya hapo wajiandae kwa maumivu zaidi kwani hakuna uchaguzi wa kufanya mzee atishike na kuongeza mishahara hiyo,zaidi zaidi wajiandae na kile kikokotoo kilichowekwa "pending" Cha mtu kupewa 25% ya pesa zako zote, yawezekana bima pia itakuja na mabadiliko makubwa kwa kuongeza makato, michango ya hifadhi ya jamii natabiri pia inaweza kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza kiwango cha kuchangia...

Ni hayo tu,tuwe na asubuhi njema kwa hisani ya bajeti,wengine tuendelee na kilimo cha matikiti tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali inawanajisi watumi ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa mbaya sana
IMG_20191217_113607.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom