BAJETI 2012/2013: Presha juu, presha chini; Serikali kufuta posho za hovyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAJETI 2012/2013: Presha juu, presha chini; Serikali kufuta posho za hovyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Waandishi Wetu

  Toleo la 243 (13 Jun 2012)


  [​IMG]


  • Sh. bilioni saba kutoka bil. 40/- zapunguzwa fungu la Tume ya Katiba
  • Serikali kufuta posho za hovyo, giza tupu ukamuaji kodi wafanyakazi
  • Vichochoro vya ufisadi kila wizara kudhibitiwa, ya CAG yazingatiwa

  SAA chache kabla Waziri mpya wa Fedha, Dk. William Mgimwa, kusoma Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013, bajeti za baadhi ya wizara zimepanguliwa dakika za lala salama, na sasa takriban Sh bilioni saba zimepunguzwa kutoka katika fungu la Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Raia Mwema, limeelezwa.

  Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ndimo lilipo fungu la Tume ya Katiba, na fedha za wizara hiyo kama zilivyo wizara nyingine, zinatokana na mgawo kutoka bajeti kuu, itakayosomwa na Waziri Dk. Mgimwa, Alhamisi, wiki hii, bungeni mjini Dodoma. Bajeti hiyo inatarajiwa kuwa Sh trilioni 15, kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

  Mabilioni Tume ya Warioba
  Mikutano miwili iliyofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Waziri Mathias Chikawe na Naibu Waziri, Angela Kairuki, ndiyo iliyosababisha kufumuliwa kwa bajeti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
  Katika fumua fumua hiyo, bajeti ya Tume sasa imepunguzwa kutoka takribani Sh. bilioni 40 hadi kufikia bilioni 33, kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

  Mkutano wa kwanza uliozaa ‘fumua fumua' hiyo ulifanyika Juni 4, mwaka huu, na wabunge wa kamati hiyo ya Bunge waligoma kupitisha makadirio ya wizara, yaliyowasilishwa na Waziri Chikawe, kwa maelezo kwamba, bajeti ya Tume ya Sh. bilioni 39.95 ni kubwa mno.

  [​IMG]
  Katika hali ya kuthibitisha bajeti kuu ya Sh trilioni 15 itakayosomwa na Waziri wa Fedha bado ni "kasungura kadogo", mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge kutoka CCM, alimweleza mwandishi wetu kuwa, hata bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Sh. bilioni 186.32 ni ndogo ikilinganishwa na majukumu ya wizara hiyo inayojumuisha Mahakama.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, maofisa wa Wizara ya Katiba na Sheria walifuta baadhi ya matumizi ya Tume ya Katiba na fedha hizo kuelekezwa kwenye matumizi mengine.

  "Wizara ilikwenda kupangua bajeti ya Tume na kuipunguza kutoka bilioni 39.95 hadi bilioni 33.94. Fedha zilizopunguzwa zimegawanywa kwa taasisi nyingine za wizara hiyo zikiwemo Mahakama, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Tume ya Kurekebisha Sheria," kinaeleza chanzo chetu cha habari kutoka miongoni mwa wabunge wa Kamati ya Bunge.

  Kwa upande mwingine, taarifa zinaeleza kuwa Tume ya Kukusanya maoni inatarajiwa kuanza kazi yake katika mikoa minane ya Tanzania, ikiwa ni awamu ya kwanza ya utendaji kazi wake.

  Chanzo chetu cha habari kinamnukuu Waziri Chikawe akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge katika moja ya vikao vya hivi karibuni kuwa; "Wataanza (wajumbe Tume ya Katiba) na mikoa minane ya awamu ya kwanza. Wajumbe watakaa huko kwa mwezi mmoja kabla ya kurejea makao makuu kwa tathmini na kurudi katika mikoa mingine."
  Hata hivyo, bado tarehe rasmi ya Tume ya Katiba kuanza kazi ya kukusanya maoni haijawekwa bayana.

  Maoni kuhusu bajeti kuu
  Wakati hali ikiwa hivyo, kwa upande wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wananchi bado wanatilia shaka bajeti kuu ya taifa, kama itajibu kero zinazowakabili.
  Lakini kwa upande mwingine, inaelezwa kuwa bajeti ya mwaka huu inaweza kujibu sehemu ya kilio au shaka hiyo ya wananchi, na hasa upunguzaji wa matumizi yasiyo ya lazima.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kwa sehemu kubwa posho na safari zisizo za lazima kwa viongozi zimefutwa na kiwango cha fedha zilizookolewa kuelekezwa katika shughuli za maendeleo.

  Sambamba na kufuta kwa posho hizo, ‘vichochoro' vya ufisadi miongoni mwa maofisa wa Serikali vinatajwa kudhibitiwa kwa kuzingatia maoni ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Miongoni mwa ushauri wa CAG utakaozingatiwa ni matumizi na matengenezo ya magari ya Serikali, eneo ambalo limekuwa ‘uchochoro' wa kutafuna mabilioni ya fedha kifisadi. Inaelezwa kuwa, tayari Rais Jakaya Kikwete amekwishaanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kupunguza misafara yake nje ya nchi.

  "Si vizuri kuzungumzia bajeti ya Serikali kabla haijawasilishwa bungeni na waziri wetu, lakini nakuhakikishia kuna mabadiliko makubwa sana ya kibajeti. Maoni ya wananchi safari hii yamezingatiwa sana kibajeti. Posho na shughuli zinazoongeza matumizi ya Serikali bila ulazima zimefutwa," anaeleza mmoja wa maofisa katika Wizara ya Fedha, aliyepo Dodoma.

  Kwa upande mwingine, ofisa mwingine kutoka ofisi ya Waziri Mkuu anasema: "Ni kweli kuna mabadiliko makubwa ya kibajeti. Lakini si mabadiliko tu, tunalenga kuwa makini zaidi katika matumizi ya bajeti hiyo na uwezo huo upo kwa kuzingatia timu hii mpya ya mawaziri."

  Lakini piakatika hatua nyingine, Raia Mwema limebaini kuwapo kwa matarajio makubwa miongoni mwa wafanyakazi nchini, kupunguziwa makato ya kodi, na wakati wafanyakazi wakiwa katika matarajio hayo, mchuuzi wa mboga na matunda nje ya Soko Kuu la Arusha, Fatma Hamad (44) amemweleza mwandishi akiomba "Mungu" bajeti isilete ‘maafa' kwa kupandisha bei za nafaka kama maharage, mchele na unga.

  Nao wakulima wa Nyanda za Juu Kusini wanalilia unafuu katika pembejeo za kilimo na mfumo mzima wa kuwapatia vocha za ruzuku, wakitaka SACCOS zitumike badala ya ofisi za wakuu wa wilaya, ambazo baadhi zimekumbwa na kashfa za kuwahujumu wakulima hao.

  Matarajio Nyanda za Juu Kusini
  Baadhi ya wachumi wa kilimo, wafanyabiashara na wakulima katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaitarajia bajeti ya mwaka huu kuja na ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya kilimo.

  "Tanzania tunasema tuna wakulima wadogo zaidi ya asilimia 90, hili ni kundi kubwa sana katika taifa, lakini wakulima wetu hawa ni hand to mouth, bajeti lazima itoe majibu ya kuwaendeleza wakulima wadogo," anasema Christian Amulike ambaye ni mtaalamu wa uchumi wa kilimo.

  Katika hatua nyingine, wakulima wengi wanatarajia Serikali kuwezesha upatikanaji wa mbolea kwa bei ambayo mkulima mdogo ataimudu wakiamini kuwa, utaratibu wa kuzitumia SACCOS ni mzuri zaidi kuliko kusimamiwa na ofisi za wakuu wa wilaya na wakurugenzi.

  Kwa mujibu wa wakulima hao, maeneo mengine wanayotarajia bajeti ya mwaka huu itayapa kipaumbele ni kilimo cha umwagiliaji na uhakika wa masoko ya mazao ya kilimo.

  Mkulima Mpeli Nsekela wa Rungwe, mkoani Mbeya, anashauri kuondolewa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika bidhaa zinazotokana na mazao ya kilimo, akitoa mfano wa maziwa.

  "Maziwa hayana VAT, sawa, lakini mazao yatokanayo na maziwa kama vile siagi yamewekewa VAT, hali ni tofauti kwa jirani zetu Kenya na Uganda, hawajaweka VAT, katika hali hii unaifanya bidhaa yetu kuwa less competitive, matokeo yake bidhaa zitokanazo na maziwa zinazozalishwa nchini zitakosa soko kwani zitakuwa ghali ikilinganishwa na nchi jirani, na soko hivi sasa liko wazi," anasema Nsekela.

  Kwa upande mwingine, Nsekela anasema hakuna uwazi katika mbolea ya ruzuku, wengine wanapata miaka yote, wengine hawapati, haimfikii mkulima, kwa hiyo hainaimpact kwa wakulima, inanufaisha wajanja wachache.

  Matarajio Kanda ya Ziwa
  Kutoka Kanda ya Ziwa, Mwandishi Wetu Deus Bugaywa naye anaripoti matarajio ya wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Kutoka huko, Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) Mwanza na mwandishi wa habari mwandamizi, Nkwabi Ng'wanakilala anasema ili bajeti iwasaidie wananchi wa kawaida ni muhimu ijielekeze katika uzalishaji, kudhibiti mfumuko wa bei, kupunguza makato ya kodi kwa wafanyakazi na kuanza kuimarisha reli ya kati.

  Anasema ni muhimu kudhibiti mfumuko wa bei, kwa sababu kinachofanyika sasa ni kama uhuni katika uchumi, soko limekuwa holela na haliongozwi tena kwa kanuni za uchumi, badala yake hisia na matakwa ya wafanyabiashara ndiyo vinaongoza uchumi.

  Akitoa maoni yake, Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Actions for Democracy and Local Governance (ADLG), Jimmy Luhende, amesema kuwa kwa hali ya uchumi ilivyo sasa hakuna jambo jipya ambalo wananchi wanaweza kutarajia kwa kuwa hali halisi imejaa viashiria visivyo na matumaini.

  "Ziko indicators (viashiria) nyingi kiuchumi zinazoashiria kuwa bajeti hii haitatusaidia, kwanza ni tegemezi, kibaya zaidi mwaka jana tulikuwa na bajeti ya shilingi trilioni 13 lakini hakuna halmashauri iliyopata zaidi ya asilimia 30 ya pesa iliyopangwa, hata hii haitaweza kuwa na lolote jipya," alisema.

  Kwa mujibu wa Luhende, tatizo ni usimamizi wa rasilimali zilizopo na kwamba kama tatizo hilo halijashughulikiwa ni kazi bure kuwa na bajeti nyingine.
  Anasser Mkiwa, ambaye ni mfanyabiashara jijini Mwanza anatarajia bajeti itaweka mazingira mazuri kwa wananchi kufanya kazi na kuishi maisha ya staha kama binadamu.

  Anashauri Serikali ipunguze misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara wakubwa ili Taifa liweze kufaidika na rasilimali zake, akiamini si haki kuwasamehe kodi wafanyabiashara wakubwa na kuwatoza kodi kubwa wananchi masikini.

  Kutoka Kanda ya Kaskazini
  Mwandishi wetu Paul Sarwatt kutoka Kanda ya Kaskazini anaripoti kuwa baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa na maoni mchanganyiko kuhusu matarajio yao, wengi wakitarajia unafuu wa maisha kujitokeza.

  Idd Ramadhani, Mkazi wa Kijiji cha Nduruma ambaye ni mkulima na mjasiriamali anatarajia bajeti itakayoleta unafuu wa maisha.

  "Bajeti ilenge kupunguza mlolongo wa kodi katika bidhaa za msingi kwa matumizi ya kila siku ya maisha ya wananchi wa kipato cha chini kama wakulima na wajasiriamali wadogo,"alisema.

  Ramadhan ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatarajia Serikali kuelekeza fedha nyingi katika kilimo.

  "Katika dondoo za mwaka huu za bajeti tumeambiwa kuwa kilimo kimetengewa Sh bilioni 100 na kati ya hizo Serikali itatoa bilioni 10 tu na zingine zitatolewa na wahisani, sasa kama wahisani hawatatoa hizo fedha maana yake ni kwamba kilimo kitakwama," alisema.

  Aliongeza: "Ni matarajio yetu pia kwamba serikali itaondoa kodi kubwa katika mafuta ya taa ambayo ndiyo tegemeo la watu wengi vijijini wanaotegemea mafuta hayo kama nishati,"

  "Katika bajeti ya mwaka jana ilikuwa kosa kubwa sana kupandisha kodi ya mafuta taa ili kukabiliana na tatizo la uchakachuaji wa mafuta ya petroli, hali iliyosababisha bei ya mafuta ya taa kupanda kwa asilimia 300,"

  "Pia Serikali iwadhibiti watumishi wake ambao ni wadokozi. Hata kama tungetenga kila wizara kuwa na bajeti ya Sh trilioni moja kama zitatumika kifisadi yote ni kazi bure hivyo ni lazima mianya ya kufuja fedha za umma izibwe yote na mwenye majukumu hayo ni serikali na vyombo vyake" alisema.

  Kwa upande wake, Lohay Langay ambaye ni mjumbe wa Muungano wa Vikundi vya Wakulima Mkoa wa Manyara (MVIWATA) aliitaka serikali kutopandisha kodi katika mafuta ya magari ili kuepuka upandaji wa bei za bidhaa nyingine.

  Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Makumira, Elfuraha Laltaika, anatarajia Serikali itawekeza zaidi katika sekta muhimu ambazo ni uvuvi na mifugo.

  Mwananchi mwingine, Anney S. Anney, mkazi wa wilayani Karatu, alieleza kuwa hatarajii maajabu katika bajeti ya mwaka huu kutokana na watendaji serikalini kutokuwa karibu na wananchi, tofauti na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere.

  "Wakati wa serikali ya awamu ya kwanza nakumbuka vizuri Waziri wa Fedha alikuwa akiwasilisha bajeti inayozingatia maslahi ya mtu wa kima chini lakini kwa sasa viongozi hali ni tofauti, viongozi wanasoma bajeti ambayo haibadilishi chochote katika maisha ya kila siku," alisema.

  Fatma Hamad (44), ambaye ni mchuuzi wa mboga na matunda nje ya soko kuu la Arusha anatarajia bajeti yenye unafuu wa maisha, itakayokabili bei za bidhaa muhimu kama sukari, unga, mkate na nafaka za aina mbalimbali.

  "Mimi naomba tu bei za bidhaa hizo zibaki kama zilivyo kwa sasa kwa mfano sukari shilingi 2,000, unga shilingi 1,200 na nafaka kama mchele na maharage ili sisi tunaofanya uchuuzi pia tumudu kununua bidhaa hizo tuweze kulisha familia zetu," aliongeza.

  Maoni haya ya baadhi ya wakazi wa Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa yanatarajiwa kupata majibu katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, inayotajwa kufikia trilioni 15.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hivi ni Wabunge wote wameamka au Sasa Wameona kama Wasipopambana na Ufisadi Raha ya Ubunge wa kudandia Magari ya kifahari Imekwisha.

  Wanafanya kazi nzuri ni Wakali zaidi ya CAG; hii itaisaidia Nchi yetu kweli hasa kutokana na Matatizo mengi tuliyonayo Pesa zitapatikana; hadi Tume ya Warioba imekatwa Pesa Mmm Good!!!
   
 3. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  OK vipaumbele vya bajeti kwa wengi bado kiza mpaka baada ya kesho (that is if JF wakiweka copy, or elese wengine tutabakia kiza), lakini na watanzania inabidi sasa waamke sio kila kukicha tu na statement za asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima hivyo ni hadithi za mbolea na bwana shamba na watoa mbolea and so forth to do with primary production.

  Tutaenda hivi mpaka lini na haya malalamiko ya wakulima hawawezi kuuza bidhaa zao kwengine kwa sababu ya government policies, mara wameuza on credit jamaa wanawasumbua malipo, or elimu ya mkulima iongezwe tuwatoe kwenye stage ya hand to mouth, watafutiwe masoko for f... sake even the president on his foreign trips and international forums talks nothing apart from the poor tanzanian farmer deprived of the market.

  In our times hatuwezi kuwa sustainable as a nation with a large percentage of us farming it is about time sasa tuanze kuuliza what about secondary production na kuanza ku-utilise our commodities into goods hata huko pia kutatoa mishahara na kuwapa watu kazi na kuwafungulia soko la ndani wakulima. Lakini tukiendelea na hadithi za mkulima kamwe (viongozi) hawawezi kuja na sera mbadala za benki (mikopo ambayo hipo business friendly) wala kuja na tactics za ku-nature secondary production.

  Im sick and tired of mkulima stories all the time.
   
Loading...