Bajeti 2012/13: Serikali kuuza mashangingi yake kupunguza gharama...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Ni habari ya leo leo ndani ya Mwananchi

Na Waandishi Wetu

BAJETI ya Serikali ya mwaka 2012/2013 inatarajiwa kutumia Sh15 trilioni katika vipaumbele saba ikilinganishwa na Sh13.5 trilioni zilizotengwa mwaka 2011/12.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk William Mgimwa aliileza Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi kuwa matumizi ya kawaida ya Serikali yanatarajiwa kuwa Sh10 trilioni na fedha za maendeleo ni Sh5 trilioni.

Dk Mgimwa alimweleza mwandishi wetu kuwa kipaumbele cha kwanza katika Bajeti yake ya kwanza tangu kuteuliwa hiyo ni miundombinu.

Kwa mujibu wa waziri huyo, miundombinu imegawanyika katika makundi manne ya reli, umeme, maji salama, usafirishaji na uchukuzi ambavyo vimetengewa jumla ya Sh4.5 trilioni.

Vipaumbele vingine vya Serikali ni kilimo, viwanda, rasilimali watu, huduma za jamii, utalii, biashara ya ndani na nje na huduma za fedha.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kuwa katika bajeti hiyo, fedha zilizopelekwa Wizara ya Uchukuzi kwa ajili miradi ya maendeleo ni Sh252 bilioni huku sekta ya usafiri wa reli ikitarajiwa kutumia Sh130 bilioni.

Katika Bajeti hiyo ya maendeleo, Wizara ya Ujenzi imetengewa Sh693 bilioni, wakati sekta ya nishati ikiwa nayo imepewa umuhimu na mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka mikoa ya kusini umetengewa Sh325 bilioni.

Mwelekeo huo wa bajeti unaonyesha pia kwamba, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetengewa jumla ya Sh364 bilioni.

Kuuza mashangingi

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilisema katika mkakati wa kubana matumizi, Serikali itapunguza matumizi ya magari ya kifahari kwa kiwango kikubwa.

Katika hatua hiyo, inatarajiwa pia kupiga mnada baadhi ya magari hayo yanayotumiwa na mawaziri, manaibu waziri, makatibu wakuu na wakurugenzi na kununua magari madogo yenye gharama nafuu.

Hata hivyo, chanzo chetu kilisema waziri huyo hakufafanua suala hilo akisema atalizungumza zaidi wakati wa kuwasilisha Bajeti hiyo Mjini Dodoma.

Takwimu za Serikali za mwaka juzi, zilionyesha kuwa Serikali Kuu hadi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilikuwa ikimiliki magari 40,000, kati yake 11,000 yakiwa ya kifahari.

Tayari Wizara ya Ujenzi kupitia timu ya wataalamu mwaka Aprili, 2007 ilitoa ripoti ya namna bora ya kupanga matumizi ya magari ya Serikali kwa kuangalia kila daraja la kiongozi, lakini ripoti hiyo iliishia mezani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

MY Take:
Kuuzwa mashangingi ni mwanzo wa kukubaliwa kwa kilio cha upinzani cha muda mrefu kuhusu matumizi ya magari ya anasa kwa wakurugenzi hadi mawaziri wa serikali ya CCM. Tutarajie mengi zaidi kunyofolewa toka upinzani na kutekelezwa na serikali ya CCM
 
Hongera cdm kwa kuwa na dira nzuri. Wananchi tunawakubali tunawaombea sana. Na ccm nayo inawakubali sera zenu na kvekeleza kimyakimya.
 
Tunasubiri utekelezaji, maana kupanga ni jambo lingine na kutekeleza ulichopanga ni jambo lingine.

Pia, hujatuambia ni kiasi gani budget hiyo inategemea wahisani na kiasi gani fedha za ndani. Binafsi nimechoka na matakwimu ya kibongo ya fedha za budget, maana katika budget ya mwaka jana, pesa zilitengwa miundombinu na sector ya afya, lakini tunaambiwa miradi mingi ya barabara na afya imesimama, ati hakuna fedha, sasa mwaka huu mnapanga nini kipya wakati kama mwaka jana hata nusu ya fedha zilizokuwa ziende kununua dawa MSD hazijatolewa na serikali??

Anyway tunasubiri muuziane hayo mashangingi kwa bei ya kutupa tofauti na thamani yake halisi, maana hata nyumba za serikali mlisema hivyohivyo kubana matumizi, mkauziana kwa bei chee tofauti na bei halisi.
 
Walimu tutakufa! Madeni yetu hata kuguswa! Elimu ya juu na mikopo vipi? Jamani tujipange hata tuandamane! Reli kwa nini isiuzwe? Kuna siri gani hapa! Mahali pengine reli za mwendo kasi sisi ni nkachu x6 hadi kigoma masaa 9o toka dar
 
Yetu macho manake tumekuwa tukisema matumizi ya kifahari ya serikali yetu maskini kwa miaka mingi labda sasa masikio ya watawala yamefunguka. Nasubiri kuona watekeleze, ikumbukwe na Pinda aliwahi kusema anapiga marufuku ununuzi wa mashangingi lakini kila ukikicha yanaongezeka!

Imani yangu ni kuwa, hapa Tz hakuna kiongozi hata mmoja anayestahili kutumia SHANGINGI, napendekeza wanunuliwe magari madogo kama "Corolla/TATA indigo" kwa sababu serikali haina hela. Ni aibu kusikia serikali haina pesa ya kununua dawa za MSD lakini inanunua V8 za watawala walioteuliwa.

Naipenda sana Tz na maajabu mengi ufanyika Tz!
 
Hapa kuna janja toto ktk serikali, kwa intelegence zangu n kwamba mwaka wa fedha uliisha madudu yalifanya baadhi ya miradi kusimama ukiwemo ule wa jimbo la Nzega chini ya mbunge muunda maandamano kutoka facebook mpaka kwenye comment, mwingine ni ule wa barabra toka Tabora Urambo.

Sio tu hiyo, hata ile ya Bariadi ilisuasua na wala Baba makelele wa barabara hakupiga, hapa ikanifanya kuamini kweli pesa imeenda Igunga.

Sasa, mbona hawajaweka pesa ya kufidishia? Yapo mengi yalitakiwa kukamilika mwaka jana watolee ufafanuzi.
 
Bajeti hiyo itaweza kutekelezwa kwa ufanisi kama JK ataacha kufanya utalii kwenye nchi za Ulaya na Marekeni kama anavyofanya yeye na marafiki zake tangu mwaka 2005.
 
Sioni sababu ya wakurugenzi ni makatibu tawala kuwa na magari. Wajifunze kutoka Rwanda
 
dili jipya hilooooooooooo.....

Sitashangaa wakiuziana mashangingi kwa bei cheee....
 
  • Thanks
Reactions: jcb
Tunasubiri utekelezaji, maana kupanga ni jambo lingine na kutekeleza ulichopanga ni jambo lingine.

Pia, hujatuambia ni kiasi gani budget hiyo inategemea wahisani na kiasi gani fedha za ndani. Binafsi nimechoka na matakwimu ya kibongo ya fedha za budget, maana katika budget ya mwaka jana, pesa zilitengwa miundombinu na sector ya afya, lakini tunaambiwa miradi mingi ya barabara na afya imesimama, ati hakuna fedha, sasa mwaka huu mnapanga nini kipya wakati kama mwaka jana hata nusu ya fedha zilizokuwa ziende kununua dawa MSD hazijatolewa na serikali??

Anyway tunasubiri muuziane hayo mashangingi kwa bei ya kutupa tofauti na thamani yake halisi, maana hata nyumba za serikali mlisema hivyohivyo kubana matumizi, mkauziana kwa bei chee tofauti na bei halisi.
Kweli mkuu maana mtu wawezafikiri ktk kuuza ndo itakuwa na msaada kwa waTz kumbe ndo njama za kujinufaisha kwakuuziana wenyewe kwa bei ya kuku! Kweli Tz inaliwa na wenye meno
 
Yetu macho manake tumekuwa tukisema matumizi ya kifahari ya serikali yetu maskini kwa miaka mingi labda sasa masikio ya watawala yamefunguka. Nasubiri kuona watekeleze, ikumbukwe na Pinda aliwahi kusema anapiga marufuku ununuzi wa mashangingi lakini kila ukikicha yanaongezeka!

Imani yangu ni kuwa, hapa Tz hakuna kiongozi hata mmoja anayestahili kutumia SHANGINGI, napendekeza wanunuliwe magari madogo kama "Corolla/TATA indigo" kwa sababu serikali haina hela. Ni aibu kusikia serikali haina pesa ya kununua dawa za MSD lakini inanunua V8 za watawala walioteuliwa.

Naipenda sana Tz na maajabu mengi ufanyika Tz!

Wengi wetu tunaipenda Tz ila hatuipendi serikali iliyoko madarakani kutokana uchafu wanaoufanya. Vijana wakati ni sasa wa kulinda na kuzitunza rasilimali zetu tuamke na tuthubutu kuhoji pasipokuogopa tofauti na hapo tutakuja kurithi maandaki toka migodini!
 
INTERESTING - haya mashangingi ni pamoja na yale ya tume ya katiba ambayo hata makaratasi hayajatolewa?

Eti wananunua huku wakituhadaa watauza kwanini wasipeshe kununua wakazitumia hizo hela kwanza ndo wakaanza kuuza yaliyopo?
 
Hizi hadithi zao tumezizoega longiiii!!!!!! Na wakiyauza watAuziana.
 
Nazidi kuisikitikia Tz yangu, nazidi kuona mwisho wa amani iliyodumu miaka mingi kwani kimya kingi tulichoko nacho juu ya madudu yanayofanywa na serikali yatu mwisho wake uvumilivu utakapotushinda itakuwa mbaya zaidi ya zile nchi zisizokuwa na ukimya, serikali yetu inashindwa kuwa na hata chembe ya aibu na kuamua walao kung'ata huku ikipuliza? Oh!
 
Serikali yetu imeanza kuwa agent wa kampuni za magari naona hapa. Sababu sioni logic ya kuyanunua mengine tangia Pinda alivyosema ya zamani yatauzwa, alafu sasa wanasema watauza wakati kuna mapya ya tume ya katiba. Dah kweli tunaonewa

Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
 
dili jipya hilooooooooooo.....

Sitashangaa wakiuziana mashangingi kwa bei cheee....

Nandivyo itakavyo kuwa maana hawa watu bana! utasikia tangazo la mnada na siku ya mnada itafika ila magari yatakuwa yamesha nunuliwa yote.
Hawa viongozi wapo kujilimbikizia mali tu hawana msaada na sisi wao kwanza sisi baadae ndo kauli mbiu yao.
 
Back
Top Bottom