Bajeti 2011: Tanzania tunahitaji kufuta vyama vyote vya siasa tuanze upya!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti 2011: Tanzania tunahitaji kufuta vyama vyote vya siasa tuanze upya!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Jun 19, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  FROM: Facebook: by William Malecela on Sunday, June 19, 2011 at 8:19am

  @ NEW YORK: Hatimaye nimepata nafasi ya kuisoma bajeti nzima ya serikali kwa mwaka 2011/2012, na kwa kweli ninasikitishwa sana na uwezo mdogo sana wa uwajibikaji wa serikali yetu ambao chanzo chake ni uwezo mdogo sana wa uongozi walionao viongozi wetu.

  I mean hakuna uwajibikaji kwa viongozi wetu na vitengo vya dola ni hafifu sana na in some cases ni zero kabisa, yaani hakuna kabisaa. I mean leo Tanzania kipato cha serikali yaani taifa, 70% inategemea kodi kutoka kwa mashirika 15 tu yaliyopo nchini, meaning kwamba the rest of 30% ndio inatoka kwetu wananchi, no wonder hili taifa tunapigizana makelele tu maendeleo hamna, I mean taifa litaendelea vipi na ukusanyaji hafifu wa kodi kama huu?

  Malipo mengi ya watumishi wa serikali hayakatwi kodi, WHY? ni kwa sababu hili taifa tumejiaminisha siku nyingi sana kwamba we are poor na hatuwezi kujiondoa kwenye umasikini, tumeiamini serikali kutuondolea umasikini, serikali ambayo inaongozwa na sisi wenyewe ambao tulishakubali siku nyingi sana kwamba ni masikini tu ndivyo tulivyoumbwa, matokeo yake imekuwa ni National Insanity circling yaani kurudia njia zile zile kila siku kwa kutegemea matokeo tofauti.


  - Miaka 50 ya Uhuru, mpaka leo bado tuna-ptoject bajeti ya taifa ambayo haifanani na kipato chetu cha taifa, tunategemea kutumia Shillingi Trillion 11, lakini uwezo wetu kitaifa ni kipato cha Shillingi Trillion 7 tu, hatuna jawabu la tutapata wapi hiyo gap ya Trillion 5, ingawa tumeruhusu kampuni kama ya Zaintel kutuchezea akili kwa kuuzwa kwa ujanja ujanja kwa Celtel and then to Airtel in the process taifa tumepoteza kodi ya karibu USD $ 312 Million, tumeruhusu Hotel ya Movenpick iliyoanza kama Sheraton, kutuchezea akili wee na kodi in the process tunapoteza kila mwaka kodi karibu USD $ 300 Million, kule kwenye madini ndiko usiseme tunapoteza karibu USD $ 800 Million kila mwaka and the list goes on and on! Sasa kwa sababu tumezoea kutafuta majibu rahisi kwa maswali magumu, tumewakalia koo Wabunge kwamba ndio wachawi wetu kwa sababu ya posho zao!

  - Wabunge wanaolipwa jumla ya Shillingi Million 7 kwa mwezi, 2 zikiwa ni mishahara yao ya mwezi na Tano zikiwa ni gharama zao za usafiri na wafanyakazi wao ambao ni lazima wawe nao kwa ajili ya kuwakilisha majimbo yao ipasavyo kwenye taifa. Sasa tunalilia mbunge asilipwe tena posho ya Shillingi Elfu 70 kwa siku anapokuwa bungeni au kwenye vikao vya kibunge, tunataka atumie hela za msahahara wake, yaani ule wa Shillingi Millioni 2.

  Mbunge akae bungeni ashiriki vikao 73 vya bajeti, akilipia shillingi Elfu 50 kwa siku kwa malazi tu, vikao 73 ni sawa na miezi miwili, sasa jumlisha utapata Mshahara wa Shillingi Millioni 4 na gharama ya malazi tu kwa kipindi kizima cha bajeti ni karibu nusu ya hizo hela zake za ujira, na tunaambiwa kwamba hii ndio inaweza kutusaidia taifa kuokoa hela nyingi sana za kuweza kuliendeleza hili taifa!, hebu angalia hela tunazopoteza kwenye kodi ya madini kila mwaka ni karibu mara 10 ya posho ya wabunge inayoliliwa sana kwamba ndio tatizo letu la taifa!


  - Ni kama taifa la wendawazimu flani hivi, maana hata huwezi kusema ni walevi kwa sababu mlevi akiamka asubuhi huwa anakuwa mzima na productive tena, sisi taifa tupo pale pale tunazunguka tu kama taili la gari, na wale wasomi wetu ndio bure kabisaa, mijina mikubwa lakini hakuna faida yoyote kwa taifa. Bunge limejaa ma-Doctor, Wanasheria, Wahandisi, mpaka Wachumi, lakini mpaka leo umeme hakuna, ujanja ujanja tu na ujinga ujinga na kutafuta majibu rahisi rahisi ndio vimetutawala hili taifa!

  IT IS ABOUT TIME SASA TUKAFUTA VYAMA VYOTE VYA SIASA HILI TAIFA, TUANZE UPYA!

  MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


  William Malecela @ New York City; USA.
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tatizo la nchi yetu si la leo hii kama wengi tunavyotaka kuaminishana hapa. Tatizo limekomaa sasa maana lina umri wa uhuru wetu wa miaka 50 kama nchi ilivyo. Ukiangalia taasisi zetu utashangazwa utendaji wake ulivyo. Hata hiyo bajeti unaweza kujiuliza waandaaji wametoka wapi? hiyo ya Upinzani nayo hakuna lolote yaani ni kituko. Tatizo siasa zimekuwa mbele mno. Kila mtu kawa mwanasiasa au akibadili nafasi ya siasa anachukua nafasi ya uchungaji/askofu au sheikh basi hayo ndio yanayowezekana.
   
 3. m

  mwl JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 180
  Mkuu hapo unazungumzia chama twawala ndio walio tufikisha hapa na wewe ukiwa miongoni mwao unabaki kulalama, hatua gani umechukua? Hivi hufuatilii yanayojiri bungeni? Posho zinazozungumziwa ni sitting alowances si pesa za kujikimu, na baya zaidi anaejiita mtoto wa mkulima anasema haziepukiki ni za kuwapa ombaomba wanaokaa nje ya milango ya bunge. Hebu angalia bajeti ya upinzani, nayo ni kama ulivyoona ya chama twawala? Tupe fikra yako ktk vyanzo vipya vya mapato.
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwani waliotufikisha hapo si ni pamoja na baba yako john samwel malecela na CCM yake
   
 5. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Yale yale ya Territory tena! ha! ha! ha! karibu sana mkuu yaani majibu rashisi kwa maswali magumu sana!

  Willie @ NYC, USA.
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  mimi nadhani kabla ya kufanya chochote katika nchi hii kwa sasa kitu cha kwanza ni katiba,
  pili mfumo wa utawala wa nchi yetu ujulikane na viongozi wawe wana wajibika moja kwa moja kwa
  wananchi na sio mtu aliyewateuwa,
  baada ya hapo tuifute CCM kungoa mzizi wa fitina na wanachama wake wasajili chama kinachoeleweka
  huu utakuwa mwanzo mzuri.
  ila katiba kwanza la sivyo tutaatamia mayai ya mbuni
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni mtoto wa kufikia wa mzee JSM.

  akili zako ndogo sana.
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Nimesoma bajeti zote, sioni uwajibikaji na infact ni incompetence at its best, bajeti ya upinzani wanadai tutumie hela zaidi ambazo hawana majibu zitatoka wapi, bajeti zote mbili hakuna mikakati mizito ya namna ya kukusanya kodi ambao ndio hasa tatizo tulilonalo,

  - Wewe unawezaje kuendesha taifa kwa kutegema 70% ya kodi za taifa kutoka makampuni 15 tu, wakati taifa lina makampuni zaidi ya 500, ndio maana Rostam anakuwa jerui sana maana ni makampuni yake yanayolipa sana kodi kwa taifa! Halafu malipo mengi ya watumishi wa serikali hayakatwi kodi, that is insane!

  Willie @ NYC, USA.
   
 9. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani wewe ukijiridhisha nafsini mwako kuwa ni swali gumu unadhani kila mtu anahisi ulichosema ni swali gumu?
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Territory karibu sana! ha! ah! ha! ha! majibu rahisi hayo kwa maswali magumu ya taifa! ha! ha! ha! ha!

  Willie @ NYC, USA.
   
 11. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  japo jamaa ni muongea pumba lakini sio fair kurushia mawe familia yake kila siku
  tujenge nchi bila chuki hii sasa ina kera
  naanza kuna unyama kulika umakini wa wanajiita wapambanaji
  ina maana wewe makosa ya familia yako yote umehukumiwa kwayo?

  tumpe break ni mtanzania kama sisi hapa ni hoja kwa hoja wewe chakachua hoja yake hapo juu
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu kwenye uwajibikaji ni zero kabisaa, na nani wa kushikia kengele mwenziwe awajibike hili taifa?

  Willie @ NYC, USA.
   
 13. G

  Godwine JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kuna kitu lazima watanzania tutambue kwamba viongozi wa nchi yetu wametawala vibaya wanafuja mali na kufanya kizazi cha tanzania masikini na kisha wao wanatumia pesa za wizi walizopata kusomesha watoto wao kwenye nchi zenye kiwango kikubwa cha elimu na kisha kuwatafutia kazi kwenye mashirika yaliyoteka mali za taifa letu. na kulazimisha taifa kuwa la kifalme. kisha watoto wao wakitaka kuingia kwenye siasa wanajifanya wao ni wapinzani wakubwa wa mfumo uliokuwa madarakani na kanuni za uongozi wa wakati huo na kisha kurithi madaraka ya wazazi wao


  TAIFA HILI ALIWEZI KUKOMBOKA KAMA MASIKINI HAWATAJIUNGA NA KUKATAA KUNYANYASWA NA KUDAI MFUMO WA UTAWALA UTAOJALI WATU WOTE LA SIVYO NI MICHEZO YA KUIGIZA TU
   
 14. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Tunalia na wabunge kwa sababu hawa ndo majambazi, na hiyo unayosema tunapoteza ndo hawa wabunge majambazi wao si ndo wanatunga sheria. Kwani ni serikali ipi unayoilaumu inachezewa? I mean wabunge wanalipwa fedha nyingi wakati hata sheria hawatungi na wakitunga ni kwa ajili ya kuwabana wanyonge. I mean, angalau wangekuwa wanalipwa posho hiyo na wao wanatunga sheria nzuri za kuyabana makampuni uliyoyataja.

  I mean, nikiwa kama mie ndo Rais basi wabunge badala ya kuwalipa mishahara na posho ni ngewazawadia viboko 12 mbele ya kadamunasi. Unaposema serikali kuwa na sera mbovu, moja kwa moja unaongelea wabunge wapumbafu.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Interesting sana! ha! ha! ha!

  Willie @ NYC, USA.
   
 16. 911

  911 Platinum Member

  #16
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Nijuavyo ni kuwa hiyo 70,000 ni "sitting allowance".Hivyo haihusiani na gharama za malazi kwa wabunge kipindi wanapohudhuria vikao vya bunge.Kwa gharama ya malazi etc najua kuna fedha ya kujikimu wanalipwa 80,000 per day.So mleta mada naona umepotosha either kwa makusudi au kwa kutokufanya homework yako sawasawa.
   
 17. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kwa sasa wa kushika kengele hakuna , ndio maana mimi naona hata kama tukufuta vyama tunaweza kurudi kule kule
  lakini cha msingi ni kwamba KATIBA iwekwe upya na itoa waziwazi hatua zinazopashwa kuchukuliwa na kiongozi aliyekologa na kama hataki basi kuwe na kitu kama petition kwa hawa viongozi ibadi furani ya wananchi ikisema NO basi anakula kona
  japo kwa raisi BUNGE liwe na mamlaka zaidi ya serikali ili kuweka usawa na hii iwe na pamoja na njia za kupatikana kwa spika
  lakini mambo mengine tutapoteza muda tu bila hii katiba kitusaidi kushika kengele
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - The big question hapa ni kwa nini hili taifa hatulipi kodi? Kwa nini hatupendi kukusanya kodi? bila kulipa kodi hili taifa tutaendelea kupigizana kelele mpaka mwisho wa Dunia na hakuna lolote la maana litakalofanyika, hata Mwalimu alilisema sana hili mwishoni mwa maisha yake kwamba taifa lisilo kusanya kodi haliwezi kwenda popote kimaendeleo!

  Willie @ NYC, USA.
   
 19. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Well mie sina tatizo kama hayo makampuni yanalipa kodi maana ndio hali halisi ya Tanzania. Lakini pia ukweli ni kwamba, kodi ambayo ingewezwa kukusanywa kama serikali ingeamua kuwajibika ipasavyo ni zaidi ya hiyo bajeti. Kuna misamaha ya ajabu saana inaendelea. kwa hilo la serikali kutokulipa kodi, inategemea na idara. Baadhi ya Taasisi za serikali wanakatwa kodi katika kila unachokijua.
  Kwahiyo pamoja na uwepo wa makampuni 500+ kuna haja ya kufikiria kama serikali inapata kodi zake zote kutoka katika vyanzo vilivyopo kisha kuongeza wigo. Si hivyo tu, kuna haja pia kubwa saana ya kuangalia MATUMIZI ya serikali na hili ni tatizo maana miradi mingi inaharibika kabla ya kumalizika.
  Kuhusu bajeti ya CDM, well hata ilani ilikuwa inamatatizo kama ilivyo kwa bajeti. Nadhani wameliona hili na ndio maana sasa hivi wameamua kushirikiana na baadhi ya wapinzani kwa sababu miaka hii mitano ingekuwa rahisi zaidi kwa CCM licha ya kwamba idadi ya wabunge wa upinzani wameongezeka.
  Mwisho niseme incompetency ni tatizo.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Swali la jibu lako ni rahisi saana, tatizo ni weak institutions. Yaani poor enforcement kuanzia kwa taasisi zote zinahusika;mahakama; mamlaka ya kodi; police na hata bunge. Haya ndiyo yanasababisha hata supervision ambayo ndio kazi kubwa ya bunge inakuwa haieleweki. Unaweza kushangaa sasa hivi agenda kubwa ni allowances lakini kuna mengi saana wabunge hawahoji aidha kwa makusudi au kutokana na uwezo wao wa kutambua.
  Suala la kutopenda au kupenda kulipa kodi linasababishwa na kwamba hakuna mechanisms in place ya kumfanya mlipa kodi alipe. Licha ya kwamba kikanuni ya quid-proquo (sorry for mis-spellings) lakini tatizo ni kwamba huwezi kulipa kodi kama huoni matumizi ya kodi hata kwa kiasi kidogo kinachotarajiwa.
   
Loading...