Bajeti 2006/07 ni ya Matumaini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,391
39,484
Leo ni siku ya Bajeti nchini. Watanzania wanasubiri kwa hamu kusikia ni nini serikali ya Kikwete imepanga ili kufanya Tanzania yenye neema iwe halisi kwa kila mtanzania. Ahadi nyingi zilitolewa wakati wa uchaguzi, je zinaweza kutekelezeka? Je ni kitu gani kitaashiria kuwa bajeti hii ni nzuri? Sikiliza maoni yangu juu yahili nikichambua vitu kadhaa ambavyo kila mtanzania anatarajia asikie kwenye hotuba ya bajeti hii; vitu ambavyo vitaleta nuru na mwanga kwa maisha ya baadaye ya nchi yetu.

Ni kutokana na utekelezaji wa bajeti hii ndo tunaweza kwa haki kuanza kumhukumu Kikwete na watendaji wake. Je wenzangu mnatarajia nini kwenye bajeti hii?
 
Mwanakijiji:

Nimekusikia kwenye podcast yako na mapendekezo yako ya bajeti. Nakupongeza kwa ushauri wako, ila ushauri huo ungetoa kabla ya bajeti ingefaa zaidi.

Nimependa zaidi suala la kilimo, na kama unaweza kuandaa hotuba yako juu ya mapinduzi ya kilimo Tanzania itakuwa safi. Bado ninavyoona hatujapata raisi ambaye anaweza kuleta mapinduzi makubwa ya kilimo ambayo ni nguvu kazi kubwa inayoajiri watu zaidi ya 80% ya watu wetu wa Tanzania.

Pili ushauri kwenye radio yako, karibisha wataalamu wengine kuongelea maswala mbalimbali isiwe ni wewe tu kila siku.
 
Mzee wa Busara, hivi sasa niko mbioni kuweza kuweka mahojiano. Najaribu kupata vifaa vitakavyoniwezesha kurekodi mahojiano ya simu na hatimaye kuyaweka hewani. Nina uhakika kabla kikao hiki hakijaiva tutaweza kufanya hivyo na natumaini waheshimiwa humu mtanipa contact za watu muhimu. Binafsi, nataka viongozi wetu wawe tayari kuhojiwa na KLH News na siyo BBC na VOA (no offense intended) peke yake.

Hata hivyo sasa hivi, pembeni ya podcast kuna namba ya simu ya show yangu.. na ukiingia huko ni kama voicemail.. unaweza kutoa maoni yako na mimi nitayabandika na watu watakusikia!!!
 
2006/2007 Budget Speeches:
Hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mheshimiwa Sophia Mnyambi Simba (Mb.),akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007
Hotuba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Mheshimiwa Nazir Mustafa Karamagi (Mb.),akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007
Hotuba ya Waziri wa Usalama wa Raia Mheshimiwa H. Bakari Mwapachu (Mb.),akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007
Hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo Mheshimiwa Dk. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb.),akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007 [PDF Version] Hotuba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta (Mb.),Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007 [PDF Version]
Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia (Mb.), Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/2007 [PDF Version]
Hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa Joseph Mungai (Mb.), Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa Mwaka 2006/2007 [PDF Version]
Hotuba ya Waziri wa Miundombinu Mheshimiwa Basil P. Mramba (Mb.), Akiwasilisha Bungeni Mpango wa Maendeleo na Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2006/07 [PDF Version]
Hotuba ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa Zakia Hamdani Meghji (Mb.), Akiwasilisha Katika Bunge Mapendekezo ya Serikali Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2006/07 [PDF Version]
Speech by the Minister for Finance Hon. Zakia Hamdani Meghji (Mp), Introducing to the National Assembly the Estimates Of Government Revenue and Expenditure for the Financial Year 2006/07 On 15th June, 2006 [PDF Version]
Hotuba ya Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Mhe. Dkt. Juma Ngasongwa (MB), Akiwasilisha Bungeni Taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2005 na Mapendekezo ya Mpango wa muda wa kati na mfumo wa Matumizi ya Serikali kwa kipindi cha Mwaka 2006/2007– 2008/09 [PDF Version]

Speech by the Minister for Planning, Economy and Empowerment, Hon. Dr. Juma Ngasongwa(MP), Presenting to the National Assembly the Economic Survey For 2005 and Proposals for the Medium Term Plan and Expenditure Framework for 2006/07– 2008/09
[PDF Version]

 
Fikiraduni,

Unajua nimefurahi sana kuona hii bajeti ya Bi. Mkubwa na naweza kusema kuna mengi sana wameyachukua toka kwetu.

nadhani unakumbuka nilisisitiza sana kuanzishwa kwa Special economic Zone badala ya madaraka kamili ya zones kiserikali na kujitegemea kama alivyodai Free. CCM wameipokea hoja hii na sasa wanaifanyia kazi. Hatua hii ndiyo waliiutumia China kuweza kutenganisha matatizo ya zone hadi zone na kutambua utajiri wa zone hizo. La muhimu hapa ni kuwepo na utafiti mkubwa tosha kwa kila zone kuhakikisha utajiri wa hizi zone unaboreshwa zaidi kwa manufaa ya wananchi.

Inasikitisha tu kwamba pato kubwa la taifa limekwenda kuboresha Dar -es salaam kwani swala la Umeme -Tanesco ni swala la mkoa wala sio zone na fedha nyingi imetengwa kwa kuboresha mahitaji ya mkoa wa Dar hali mahitaji makubwa ya baadhi za mikoa hayakuangaliwa kwa usawa huo huo.

Labda kilichokosekana ktk utaratibu huu ni kuwepo na vituo vya utafiti ktk hizi zones vikiongozwa na wananchi wa sehemu hizo kwa ushirikiano kati ya serikali kuu, Union, benki husika na mwisho wawekezaji. Nakumbuka nilipendekeza vituo vya JKT vitumike kama sehemu za utafiti wa wizara nzima ya KILIMO na MALIASILI. Hapa iwe ufugaji, Uvuvi, ukulima misitu, au madini lazima utafiti wa dhati ufanyike kwanza kabla ya makubaliano na mikataba. Na wananchi waelemishwe vya kutosha kwa kuwa na wataaalam wenye ujuzi, wataalam ambao kama kuna upungufu basi tuwatumie ndugu zetu Waamerika weusi kujihusisha moja kwa moja na vituo hivi kama wanavyofanya Israel.

Pili, upatikanaji wa mikopo kwa wananchi ili kuendeleza miradi ama ubunifu wa miradi ambayo ni tegemezi ni hatua nyingineyo ambayo tuliwahi kuizungumzia Bsctimes, nayo imepokelewa ktk bajeti hii.

Sikupenda sana kipande cha kodi hasa pale nilipoona msamaha wa kodi kwa kipato cha chini kufikia shillingi 80,000. Kusema kweli mimi ningependa kuona mshahara wa chini umepandishwa mara mbili na wananchi wa chini walipe fungu dogo sana kulingana na ukubwa wa familia zao. Kwani sasa hivi kima cha chini bado kidogo sana kwa mwananchi wa chini kuweza hata kulipia nauli, malazi na mlo mmoja kwa siku akiwa kazini. hali hii inazidisha ujambazi na fikra za kuiba - crime in general. sasa hivi nchi yetu imefika ktk njia panda ambapo mashika ya watu binafsi ndiyo yatakuwa waajiri wakubwa na sio serikali tena.

Ongezeko la kodi lingekuwa zaidi ktk sigara na pombe kwa malengo ya kudhoofisha kidogo utumiaji wake. Kuna wataalam wa afya wanaosema kwamba utumiaji wa sigara na pombe ni matokeo ya hali mbaya za wananchi kiuchumi kwa hiyo basi ikiwa maneno haya yana ukweli ndani yake basi nadhani ongezeko la mishahara, masaa mengi kazini na kupanda kwa bei kwa vitu vyote vya anasa kungehamasisha wananchi kutumia muda wao mwingi ktk uzalishaji badala ya kujirusha kuondoa mawazo.

Zaidi ya hapo nadhani bajeti hii ni nzuri sana ukilinganisha na bajeti za nyuma kwa sababu imechukua mazuri ya Mkapa ambayo hakuyafanyia kazi ili kuyaweka wazi kwa wananchi. Swala la ardhi bado litanitatanisha kwa sababu kabla ya Uhuru wengi wetu tulikuwa na ardhi kubwa sana ambayo ilichukuliwa na serikali. Na sidhani kama kuna mtu leo hii ana kibali cha kumiliki mashamba hayo ambayo wengi baada ya kuchukuliwa na serikali waliondoka na kutafuta njia nyinginezo.

Mashamba hayo leo hii yanamilikiwa na viongozi wa serikali ambao bado hawajaridhika na mali walizokwisha iba.
 
Fikiraduni, hii bajeti ni ya kiinimacho!!! Hebu ipitie tena halafu unijibu maswali haya.

a. Je sekta ya Kilimo imepewa kipaumbele cha namna gani ili kuanza kubadilisha kilimo chetu toka cha kujihemi hadi kuwa cha kisasa na cha kujitosheleza?

b. Ni jinsi gani Sekta ya Elimu imepewa kipaumbele kuhakikisha elimu inayotolewa ni bora na inawafikia watu wengin kwa njia nyepesi zaidi na kwa gharama nafuu?

c. Je sheria gani imependekezwa itakayosimamia, mijadala ya madini na kuhakikisha kuwa wale wote wanaoingiza serikali kwenye mikataba bomu ambayo inawanufanisha wao binafsi wanachukuliwa hatua za kisheria? Serikali haipotezi fedha kwa watu kukwepa kodi tu bali pia kwa kujiingiza katika mikataba inayokosesha serikali mapato!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom