Bajaji zilizoibiwa Dar

killo

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
401
225
Habarini wandugu, Ndugu yangu aliibiwa bajaji yake mwanzo wa mwezi huu na nikapata taarifa kwamba Bajaji na Pikipiki zinazoibiwa huku bara huwa zinapekekwa kuuzwa Kigamboni maana kule hakuna askari polisi wengi barabarani kama ilivyo huku bara.

Kufuatia habari hizi, nikiwa naendelea na uchunguzi nikapewa habari nyingine kwamba askari polisi kupitia kitengo maalum wameendesha msako mkali hususani kwa bajaji katika eneo la Kigamboni na wamefanikiwa kukamata bajaji nyingi tu ambazo zipo kituo kikubwa cha Kigamboni.

Tulifika hapo mara moja asubuhi hii na kwakweli ziko nyingi sana japokuwa ya ndugu yangu sijaipata/Sijaikuta.

Natoa rai kwa wengine ambao wameibiwa bajaji kwamba wafike kituo kikubwa cha Kigamboni wakaangalie kama watakuta bajaji zao.

Pamoja katika ushirikiano.
 

vanmedy

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
2,609
2,000
bajaj hukimbiziwa kigamboni.. huko hupanguliwa kila kitu na kwenda kuuzwa spare parts hasa mikoa ya kusini... jamaa mmoja mtaani hapa alinyang'anywa bajaj yake ila kwa kudra akishirikiana na wenzake wakaiwahi inataka kuvushwa kigamboni.. bad thing yule mwizi walimuua aisee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom