Bajaji za pale Uhasibu Kurasini ni hatari kwa maisha ya wavuka barabara, Polisi ilitazameni hili

halfcastmangi

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
350
930
Habari za uzima wana JF,

Kuna kero huwa naiona na nimewahi kunusurika kugongwa na zile bajaji pale Uhasibu Kurasini, madereva wake wana tabia wanakuja chuo cha Uhasibu kwa kutumia upande wa magari yanayoenda Mbagala, sasa mtu akiwa anavuka anaangalia upande wa magari yaendayo Mbagala then anaanza kuvuka, maskini kumbe bajaji zinatumia upande huo huo kuibia kwenda na pale Uhasibu jambo ambalo ni hatari sana

Nimewahi ona mtu kanusurika kugongwa na bajaji hizo na hata mimi majuzi imenipita tuseme ni Mungu tu alininusuru.

Naomba kuuliza je utaratibu huo ni sawa na wapo sahihi? kama sio sahihi wapi jeshi letu la polisi? mbona mpo polisi wengi tu pale darajani lakini mnashindwa vp kujigawa kupambana na hawa madereva wasiofuata kanuni na sheria za barabarani?
 
Back
Top Bottom