Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 554
- 1,301
Leo naleta kilio ambacho ni kero chetu wananchi tunaoishi Mapinga na maeneo yote yanayopakana na barabara ya Bagamoyo.
Kilio hiki kinahusu nauli za usafiri wa bajaji kwani madereva/wamiliki wa bajaji wamekuwa wakijipangia nauli zinazowapendeza wao kila kukicha kinyume na utaratibu.
Mwaka jana nauli zilikuwa shilingi 500, baadaye walipandisha ikawa shilingi 600, lakini mwanzoni mwa mwaka huu ilipanda zaidi ikawa shilingi 700.
Ghafla mwanzoni mwa mwezi huu, imepanda tena na sasa tunalipa shilingi 800. Yote hayo wanasingizia kupanda bei za mafuta.
Jambo hili limetushtua mno na tunaiomba Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) kuchukulia kwa uzito barua hii ili itoe taarifa rasmi ni kiasi gani cha nauli kinachopaswa kulipwa.