Bajaji ipi yenye faida kubwa Kati ya bajaji ya abiria na bajaji ya mizigo

Anko Kong

Senior Member
Jul 3, 2020
130
72
Wakuu nawasalim kwa jina lipitalo majina yote.

Kama kichwa cha habari kinavyosema naombeni mchanganuo wenu kati ya bajaji ya abiria na bajaji ya mizigo ipi inafaida kubwa na ipi yenye ubora zaidi.

Naamini humu kuna wazoefu wa mambo haya.

Asanteni.
 
Bajaj ya mizigo ila uendeshe mwenyewe.. Ukila vichwa viwili vya elfu 20-20, unafunga kazi.. Bajaj ya abiria mpaka upate Tsh elfu 40, lazima uwe umebeba abiria 80 wa Tsh 500.
 
Bajaji ya abiria hukosi 30 mpaka 40 per day uhakika, chukua ya mizigo ujute
 
Uzi mzuri je kumvua mtu Bajaj nzima kwa mil 3 au kununua mpya kwa mil7 ipi imekaa njema wadau?
 
Bora bajaji ya mizigo kuna jamaa yangu anafanya kazi hiyo hadi biashara za dukani kaamua kuachana nazo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom