Bajaj business, 12,000,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajaj business, 12,000,000

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bado Niponipo, Oct 9, 2009.

 1. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wakuu heshima mbele,

  Nimefanikiwa kukamata 12,000,000 ambayo nataka kuizungusha kwa biashara ndogo, kuna watu wamenishauri kuwa kwa kiwango nilicho nacho naweza kununua BAJAJ 3 na kufanya biashara ya usafiri ya Bajaj.

  Kinachotakiwa nifanye ni kununua hizo Bajaj 3, baada ya hapo natafuta watu watatu ambao kila mmoja nitampatia Bajaj moja moja, hawa jamaa watakuwa wakinilipa shiling 15,000 kila mmoja kila siku, lakini kufanya shughuri ya kukusanya hela iwe rahisi hawa jamaa watakuwa wana-bank sh 105,000 kila mmoja kila week...hesabu yake imekaa hivi.

  3 bajaj x 105,000 kila bajaj kila week = 315,000 kila week.

  315,000 X 52 weeks a year = 16,380,000

  Kwa hesabu hiyo nitakuwa na uwezo wa kuingiza 16,380,000 kwa mwaka.

  Matengezo ya Bajaj nimeambia ni ya gharama ya chini nitatumia chini ya 100,000 kwa kila Bajaj kwa Mwaka.

  Wadau mnaonaje kuhusu hili, niko mbali na Dar na nadhani Bi mkubwa ataweza kabisa kusimamia mradi huu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Such a good idea, what you need is just a bit of entrepreneurship knowledge, and then...you take-off at jet-speed with your idea!Kupanga ni kuchagua, lakini mimi nasema pia kwamba KUCHAGUA NI KUPANGA, so go for what your heart feels undertaking, nadhani utakuwa na amani ya moyo zaidi, and under a good management you will prosper! Lakini kuna wanaJF ambao hadi dakika hii wanamiliki Bajaj, wanaweza kukusaidia zaidi..
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kweli wa tz sio wabunifu,yaani bajaj zilivyo jaa na wewe unaenda funga foleni???????milioni 12 but ubunifu sifuri.fuga kuku basi
   
 4. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  The Boss,

  Hii imenivutia, Je ni kuku wapi wanalipa zaidi na kwa haraka, wa nyama au wa mayai? Unaweza kutoa mchanganuo wa kufuga kuku hasa kwa mtu anayetaka kuanza na kuku 1000?
   
 5. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  I thought bado upo upo kwanza!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuku popote pale,we hakikisha bei yako haizidi 3500 mmoja.wateja watakuja kukugongea hadi usiku wa manane.
   
 7. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu usiangalie faida tu angalia na risks, kuku wakipata kideri imetoka, Bajaj ikipata pacha unapeleka kwa fundu mwendo mdundo!
   
 8. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sasa maneno ya kejeli ya nini tena kaka, nimeanzisha thread hii kuomba mawazo ya wanachama hapa JF na wala sikuanzisha thread hii kutafuta kejeli bali ushauri, wazo la kuku zuri lakini kama umenisoma vizuri nimewaeleza niko mbali na Dar na hivyo itakuwa vigumu kufanya biashara hiyo ya kuku.

  Samahani kama nimekukwaza mkuu.
   
 9. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bi mkubwa kwetu sisi hunamaanisha mama...na si mke kama ulivyofikiri.
  Bado nipo sana.

  Vipi Biashara ya Bajaj unaionaje inalipa?..hasa hasa wazee wa serengeti inawafaa sana hii jioni mkiwa mnaingia maeneo kukamata moja baridi.
  Unakuwa umeepuka Drink Driving
   
 10. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Uzuri wa biashara hii, unarudisha mtaji wako in one year time, the second year 16,000,000 mfukoni third year 16,000,000 4th year unauza hizo bajaj for 10,000,000.

  So you can make a 42,000,000 profit in 3years time na kumbuka biashara hii haihitaji usimazi mkubwa toka kwako, wewe ni kumake sure jamaa wanakuletea hela yako kila week.

  Mnaonaje.
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Umeula kaka! Hesabu zako kali, lakini umeweka bajeti ya mapolisi na vimada wa madereva wako? Wao nao wanayo hesabu ya kuchuma ili bajaji hizo ziwapatie bajaji za kumiliki wenyewe na nyumba za kuishi na mali ya kuolea na za kumpelekea yule chui anayeshangilia mpira na chupa mkononi kwenye kideo.

  Umeumia wewe peke yako kupata hiyo hela, walaji ni wengi zaidi ya wewe na wana matumbo makubwa zaidi. Vibajaj hivyo wewe unasema laki moja service kwa mwaka, labda utafanya mwenyewe, lakini kama watafanya wengine hiyo laki moja ni mara moja labda kwa mwezi.

  Leka
   
 12. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mkuu Leka, heshima mbele.

  Nimepata wasaa wa kuwauliza wenye bajaj, wanadai mfumo ni kama wa biashara ya taxi, yeye hata akitengeneza 100,000 kwa siku wewe lazima upate 15,000 yako, nasikia biashara kama ikiwa mbaya dereva hakosi 30,000 kwa siku, kwa hiyo 15,000 yako iko palepale.
   
 13. E

  EMMANUEL SHOMBE Member

  #13
  Oct 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu mawazo yako mazuri lakini katika kuweka hesabu yako umesahau
  risks ya dereva wko akigonga mtu je utafanyaje au yeye akifa je. Nionavyo mimi nenda nazo kijijini ukafungue mraji wa KILIMO KWANZA PEMBEJEO.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah mkuu huu ubunifu nimeukubali kabisa ukipata madereva wazuri itakulipa tu.
   
 15. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #15
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hi! i think you real need an assiatance in entrepreneurship as well as bznees kwa ujumla, kimsingi mkuu hatua ya kwanza huwa ni generation of bznes idea and then una fanya screening kupata at least the three best ideas halafu yanafuata mengine kupitia bznes planning, resource mobilization etc or otherwise if you dont mind plz let contanct via safariwafungo@yahoo.com/+255 (0) 713 764589 at any time, your welcome!
   
 16. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kilimo Kwanza SASA, MAISHA BORA 2015....HAHAHA.....lakini bajaj hata UKIWA mbali mtu mwingine anaweza kusimamia..fanya research inaweza lipa kaka..
   
 17. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Duh...

  Hope huta kula million moja 1,000,000 kwa ajili ya Bajaj Business Plan ukamwacha jamaa na 11,000,000.

  MJ
   
 18. m

  mimi-soso Senior Member

  #18
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ushauri wangu usianze na bajaj tatu, biashara huwa hawaanzi hivyo. Wanaanza kidogo kidogo na kuangalia biashara inaendaje. Bora uanze na moja, ukiona biashara inaenda vizuri ndio uongeze, ila usile hizo pesa nyingine ziweke hata kwenye fixed deposit ya miezi mitatu-mitatu ili usiile. ukiona biashara inaenda vizuri unazitoa na kuongezea kwenye biashara yako, ukiona haifai utatumia zile ulizoweka akiba kuanza na wazo lingine
   
 19. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Benki gani hiyo ya fixed ya three moths na Riba yake ikoje.

  MJ
   
 20. s

  shabanimzungu Senior Member

  #20
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Start with one you fool! do not invest all yr monry first...kuwa kama wahindi their success is caution ...frst invest reap and invest agian..and you wll be filthy rich!!!!!!!!
   
Loading...