Bahati nasibu ya kuhamia Marekani-dv 2020 imeanza rasmi

Dive

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Messages
417
Points
500

Dive

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2013
417 500
Kuna wadada wameapply na wamefanikiwa wanasuburia next steps. Kuedit picha walitumia MS Word ili kupata background nyeupe na size kupitia hapa My new passport photos . Ni rahisi na kitu cha chini ya dakika 1 hakuna vitu vingi vya kujaza.
2018-10-24_20-38-01 (2).png
2018-10-22_12-00-01 (2).png
2018-10-24_20-38-01 (2).png
2018-10-22_12-00-01 (2).png2018-10-22_12-00-01 (2).png
2018-10-22_12-00-01 (2).png
 

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
2,698
Points
2,000

dalalitz

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
2,698 2,000
Habari Wadau,

Niwakumbushe wale wote wenye nia ya kushiriki katika Bahati nasibu hii ya DV-2020.

Muda umekwenda sana.
Kwa Mwaka huu;
MWISHO Kushiriki kwa kutuma Ushiriki wako ni Tarehe 6/11.

Kumbuka haishauriwi kusubiri ili kucheza muda wa mwisho kwakuwa huwa kunatokea msongamano katika mtandao ambao huweza kupelekea kuchukuwa muda mrefu kwa ingizo lako kupokelewa au mara nyingine kushindwa kabisa kwa ingizo kukubali kupokelewa.

Hivyo, Iwapo unauhitaji wa kushiriki HIMA fanya sasa na bila kuchelewa.

Nawasilisha.
 

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
2,698
Points
2,000

dalalitz

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
2,698 2,000
Vp mkuu iwapo nitakutumia wew ktk taratibu zote, lakini nikawa sijui kiingereza hata kidogo, hapo kutakuwa na swala la mm kutarajia muujiza wa mungu kweli eti bahati itanidondokea?
Vigezo vikuu ni Elimu au Uzoefu na Uraia wako kama inavyoelekezwa na utaratibu wa Bahati nasibu hii.
Ukiwa navyo hivyo tosha.
Kuongea Lugha yoyote kiufasaha si kigezo kikuu ingawa ni faida ya ziada.
Ingawa kuwa na Elimu ya juu lakini kutokuwa na Kizungu hata cha kuombea Maji kwa aliesomea Tanzania ni itakuwa maajabu ya mwaka.

Tuwasiliane iwapo unayo Nia kweli tushauriane: +255 714 59 15 48.
 

dalalitz

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2013
Messages
2,698
Points
2,000

dalalitz

JF-Expert Member
Joined Sep 6, 2013
2,698 2,000
Habari Waungwana.

Naam,


Kwa wafuatiliaji wapya:
DV-Lottery nini?
Ni aina ya pekee ya Bahati Nasibu itakayokupatia Kibali/Viza ya Kuhamia/Kuishi Marekani upendavyo.

Hutolewa kwa Raia wa Nchi kadhaa tu zilizoainishwa kwa sababu maalum na kwa kwa watu wenye vigezo maalum.

Maelezo na michango ya Wadau ya kuongeza ufahamu wako toka kwa wadau wa hapa JF, Tembelea:


HOJA YA MSINGI MWAKA HUU HUENDA UKALAZIMIKA KUWA NA HATI YA KUSAFIRIA NDIPO USHIRIKI.

Tufahamishane kwa wale ambao hawana taarifa hadi sasa,
Ni kuwa imetoka taarifa kuwa imepetendekezwa kufanyika marekebisho/maboresho kidogo katika taarifa zinazohitajika kwa mchezaji wa Bahati nasibu hii kwa mwaka huu 2019 Oct.
Kwaajili ya Programu inayotambulika kama DV-2021.
Kwa kila Muombaji mkuu
(Principal Applicant) atalazimika aweke taarifa za Hati ya kusafiria.
Hivyo iwapo ungependa mwenza wako nae acheze pekeyake akikujumuisha nawe pia atalazimia kuwa na Hati ya kusafiria vilevile.

Ieleweke:
Ni taarifa ya mapendekezo ambapo yakipitishwa rasmi itatangazwa na kuwa utaratibu rasmi wa kufuatwa wakati wa kucheza mwaka huu.

Mwaka jana na miaka kadhaa iliyopita Mchezaji wa Bahati nasibu hii hakuhitajika kuwa nayo/kuweka taarifa za Hati ya kusafiria (Passport) wakati wa mwanzo wa kucheza (Electronic registration)

Kwanini nimeleta Uzi huu mapema Hii?

Nadhani pengine nimechelewa pia, kwani najua ilivyo changamoto upatikanaji wa Hati ya kusafiria(Passport) kwa hapa kwetu.

Ikumbukwe Dirisha la BAHATI NASIBU Hii huwa linafunguliwa tarehe za mwanzo za mwezi wa kumi na uchezaji unadumu kwa Mwezi mmoja tu hivyo, Naamini kwa ambae anayo Nia ya kushiriki mwaka huu atakuwa na wasaa wa kufuatilia Hati katika muda huu uliobaki kuliko kusubiri hadi siku za mwisho.

Dokezo:
Kigezo cha Hati kinadhaniwa huenda kitapunguza wachezaji kanjanja na wasio na Nia ya dhati kushiriki hivyo pengine kuongeza nafasi ya kufanikiwa kwakuwa idadi itapungua ya wachezaji.

Maswali ya tu,
Namba yangu Ipo kwenye link hapo JUU.

Nawasilisha.
 

Forum statistics

Threads 1,344,654
Members 515,967
Posts 32,830,940
Top