Bahati inawabeba vilaza na kuwabania majembe

Nsimbi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
1,084
2,000
Ama kweli kazi ya Rabuka haina makosa. Humpa amtakaye na kumnyima mwingine.
Nchi nzuri amezipa viongozi wabaya na baadhi ya nchi mbaya kazipa viongozi wazuri.

Mfano ni mama Hillary Clinton. Watu walitarajia angekuwa rais wa Marekani. Lakini kwa vile haikupangwa nchi ikaishia kuwa na kiongozi kama Trump.

Kuna akina mama wengi wazuri wenye akili Marekani lakini bahati ikamwangukia Melania toka Slovenia kuwa First Lady!

Kule Philippines nako wamepata rais mtata balaa. Rodrigo Duterte!!
Venezuela ni nchi tajiri wa mafuta lakini ina kiongozi wa hovyo. Nicolas Maduro!

Nchi nyingi za kiarabu zina utajiri lakini utajiri huo umekumbatiwa na koo za kifalme zisizojali haki za binadamu.

Nchi zenye mali hazina amani na zenye utulivu ni masikini.
Afrika kusini ni nchi yenye wasomi wa kutosha lakini ilikuwa chini ya Jacob Zuma ambaye hakusoma kabisa.

Mambo mengine ni lazima kuwa na neema kuyapata. Bila hivyo hayaji. Ndio maana wanawake wazuri wamepata wanaume wakorofi na wanaume wapole wameoa wake watata balaa.

Wengine wanasoma kwa bidii wengine wanasubiri kuiba mitihani. Waliofaulu na kupata vyeti wanasota wakati waliofoji vyeti wanafanya kazi nzuri.

Wakati mwingine fate huwa favor watenda maovu, wajinga ma vilaza.

Watu wangapi wanafaa kuongoza jiji la Dar. Lakini fate imetuletea Makonda. Mtu asiyefaa kuongoza jiji kama lile .
Kule Zanzibar kuna watu mahiri sana wa kuiongoza lakini fate ikamuibua Shein! Mtu wa blabla!!

Kuna majembe kibao CCM yangefaa kuwa wasemaji wa chama hicho lakini fate from no where imemleta Polepole!! Mtu asiye na mvuto wowote kwa kazi husika.

Ni fate tu ndio imempaisha Kasim kuwa PM. Kuna majembe kibao yangeweza kufanya vizuri zaidi. Jamaa ana bahati sana.

Wangapi walitamani kuchukua mikoba ya Salva pale Ikulu lakini bahati ikamwangukia Gerson Msigwa! Mtoto wa Songea.

Fate imewapa baadhi utajiri huku wengine wakihangaika in vain. Wewe unahangaika miaka 21 kudunduliza Sh mil. 15 , mtu mwingine anapata Sh mil. 300 kwa siku moja kwenye bahati nasibu nk.

Wengine wakilipwa mafao yao baada ya mwezi tu. Wewe unaambiwa kusubiri hadi uzeeke! That is what the crazy story of life is.

Fate imewapa masikini watoto wengi huku matajiri wakifa bila watoto hata wa kusingiziwa.

Fate imewanyima wenye akili na busara vyeo na mali ikawapa wapumbavu.
Fate imewapa uzima watu wasio na tija ikawanyima wenye mchango katika jamii. Hangaikeni kutafuta hizo riziki nk lakini tujue kufa ni lazima.

Life is very short. So ukipata live it to the fullest. Usijihangaishe saaaaaaaaaana na maisha haya. Life is not fair. Get used to it.

Tabu ya wengi ni kwamba wanahangaikia sana vitu watakavyoviacha hapa duniani kuliko watakavyoondoka navyo. You will surely die. At any moment! Take it easy.
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,762
2,000
Ni kweli kabisa, wengine wanajiandaa kuwa viongozi wazuri wengine wanasukumizwa ndani hata kama ni vichaa
 

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
1,560
2,000
Big up, maneno mazito sana haya tunayaona maofisini, mashambani, makanisani nk, mfn asiye na uwezo wa kulea watoto Mungu anampa watoto wengi mwenye uwezo anatafuta hata mtoto wa kusingiziwa bila mafanikio. Mungu ni mwema...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom