Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,185
^^
Classmate wangu huyu tulipotezana nilipohama shule nikiwa kidato cha pili.Tangu wakati huo sikupata mawasiliano yake ikizingatiwa kuwa wakati ule hata hizo simu hatukujua kama zipo.Lakini milima haikutani binadamu hukutana.
Tumekutana nae na isingekuwa yeye kunitambua bila shaka kwa kona nyingi na mahangaiko ya hapa na pale mjini basi pengine ingenichukua miaka mingine kuonana au tusionane tena maishani.
....
Aliniita katikati ya umati wa watu.Nilipogeuka kutazama sikumtambua.Alikuwa ni dada ambaye tayari mabadiliko mengi ya mwili.Alionekana mwenye afya njema sana.Aliponitajia jina lake,,mambo mengi yalipita akilini mwangu.Nilimkumbuka katika mengi.Tuliahidi kukutana tuongee vizuri na kwa kirefu
....
Siku ilipofika alikuja ninapotafutia riziki yangu ya kila siku.Hapo ndipo nilipojifunza kuna watu wanapitia mambo mazito katika ndoa zao! Ana tatizo katika ndoa yake,tatizo kubwa ni KUKOSA MTOTO. Alikuwa akitiririka machozi.
....
Lakini kama kuna mtu anaemfahamu vizuri historia ya dada huyu,mmojawapo ni mimi,,tumesoma nae tumekimbia nae mchakamchaka! Jambo moja ambalo sitalisahau kwa dada huyu ni ule usiku wa saa 5 alipogonga mlango (shule ilikuwa ya kutwa) kuomba msaada wangu nimpeleke hospitali. Niliwaamsha rafiki zangu tusaidiane kumbeba.Alikuwa akivuja damu nyingi sana. Hospitali ilikuwa mwendo wa kilometa 6.5 hivii hivyo tulipeana zamu kumbeba. Tukiwa karibu na kufika,nguvu zilimuishia kabisa akaniita na kuniambia 'kama ntakufa waambie nyumbani ni kwa sababu nimetoa mimba,ni mimba ya sita kutoa' nilishituka mpaka nywele zilisisimka. Hata hivyo Mungu ni Mwema,alipata matibabu na akapona
....
Siri hiyo niliishi nayo huku picha za vipande vya nyama nyama vilivyokuwa vikitolewa kwa mkasi wa Mganga wakati nachungulia dirishani usiku ule,zikiumiza hisia zangu.
....
Sasa juma lililopita,dada ananisimulia alipata mume mwenye sifa zote za ndoto ya mwanamke kumpata.Mwenye nyumba,kazi nzuri na pesa ya kutosha. Lakini nyumba haina mtoto,sauti nzuri ya mtoto hakuna,utamu wa neno baba au mama hakuna! Yeye anasema kuolewa ilikuwa bahati!
....
Mimi nae sina adabu! Nikamuuliza kuhusu mimba alizotoa! Akasema mumewe hajui hilo. Akasema amemruhusu mumewe aoe mke mwingine,, Lakini mumewe anasema yeye ni mshika dini hivyo mtoto watapata tu,asihofu na avumilie.Nikamshauri ajifanye wanaenda hospitali kupima uzazi ili iwe njia ya kumjulisha mumewe kuwa hana uzao,,akasema atajaribu japo hataki kuipoteza bahati ya mume,kwani ameteseka kukaa benchi kwa miaka mitano bila kuolewa! Anasema akiacha bahati hii atasumbuka.
....
Ilinisikitisha Ikaniachia Maswali bila majibu,,
Mapito ya maisha yana mengi.