mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,337
Katika hali ya taharuki leo majira ya saa mbili nikiwa najiandaa kupanda kivuko nikitokea kigamboni nilishuhudia kivuko kikipoteza uelekeo mahli kilipokua kimepaki na kutaka kugonga mitumbwi na boti ndogo zilizokua zimepaki pembeni ya kivuko hicho! Wengi tulishtuka na waliozoea hali hiyo walisema kua baharia mda huo hua amelewa na si mara ya kwanza tukio hilo kutokea kwa sababu anajua hakuna wa kumkemea na ameajiriwa na mjomba wake kwa hiyo nyie walalahoi hamuwezi mwambia kitu......wamiliki wa boti na mitumbwi waliokuwapo katika eneo husika walivurumisha matusi ambayo kama yangekua na nguvu yangedondosha mv magogoni....Sasa najiuliza jamani tutaendelea hivi hadi lini au mpaka yatokee maafa kivukoni hapo ndio tutashtuka? Jamani wahusika naomba mchukue hatua leo watu wametukanana kesho watarushiana mawe kesho kutwa risasi....