Baharia wa MV Magogoni aendesha kivuko akiwa amelewa!

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
556
500
Katika hali ya taharuki leo majira ya saa mbili nikiwa najiandaa kupanda kivuko nikitokea kigamboni nilishuhudia kivuko kikipoteza uelekeo mahli kilipokua kimepaki na kutaka kugonga mitumbwi na boti ndogo zilizokua zimepaki pembeni ya kivuko hicho! Wengi tulishtuka na waliozoea hali hiyo walisema kua baharia mda huo hua amelewa na si mara ya kwanza tukio hilo kutokea kwa sababu anajua hakuna wa kumkemea na ameajiriwa na mjomba wake kwa hiyo nyie walalahoi hamuwezi mwambia kitu......wamiliki wa boti na mitumbwi waliokuwapo katika eneo husika walivurumisha matusi ambayo kama yangekua na nguvu yangedondosha mv magogoni....Sasa najiuliza jamani tutaendelea hivi hadi lini au mpaka yatokee maafa kivukoni hapo ndio tutashtuka? Jamani wahusika naomba mchukue hatua leo watu wametukanana kesho watarushiana mawe kesho kutwa risasi....
 

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,767
2,000
Kwa Fikra, Siasa na Sera hizi;
Tanzania itabaki shuhuda wa ajali kubwa za majini
 

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,536
1,250
Wahusika chukueni hatua kwani kuna utata kwenye uendeshaji wa boti za magogoni na kigamboni.
 

SIKUOGOPI

Member
Oct 3, 2011
27
0
Kamata Dereva Piga Makofi ya Uso mpaka ule wamotomoto utoke mbela Pambafuuuuuu! Unataka ustaarabu kwenye Kifo! Utakufaa!
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
52,600
2,000
haya yanattokea mita 100 toka IKULU ya nchi ..sasa je huko mikoani kupoje?? uzembe wa serikali ya ccm utatuangamiza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom