AlmasMAlmas
Member
- Jun 24, 2017
- 28
- 19
Niihitaji full hii riwaya ni kiasi gani...
Akikujibu unitag aisee..Niihitaji full hii riwaya ni kiasi gani...
2500 mkuu,namba zake ziko kwenye kila mwanzo Wa episodeNiihitaji full hii riwaya ni kiasi gani...
Ahsante kwa kuniwakilisha mapema Chief2500 mkuu,namba zake ziko kwenye kila mwanzo Wa episode
Sent from my H8402 using JamiiForums mobile app
Keshakutaga tayariAkikujibu unitag aisee..
Wewee mimi ndo haji makame nashusha kipgo balaaaMe ndo Zedi mjue nawaona tu na hizi ndo harakati zangu hizi (asante sana mtuzi unajua kunikosha na hizi kazi zako)
kwa mwendo huu mpk paje kuchimbika ni xmass tuombe uzima.mpk mlambwa miguu afuraiHuko hard rock kutachimbika
RIWAYA; BAHARIA
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA KUMI NA NANE
***
Zedi alipitia kwenye maegesho akachukua piki piki yake na kuondoka huku kitu pekee alichokuwa anakiwaza ni Hard Rock Cafe na Hard Rock Casino.
Alihitaji kujua mengi kuhusu hizo sehemu lakini pia alihitaji kukutana na Mbondya p.a.k bwana Mapesa.
Kazi anayoifanya ni kazi ambayo ina pesa nyingi ila haiwezi kuwa kazi ya kumpa vibunda vile vya dolali na pia kazi anayoifanya msingi mkuu ni kutokuwa mlevi wa kila muda, hiyo ni kwa usalama wake na abiria anaowabeba pale anapohitajika, sasa ni ajabu kusikia Mbondya ni mlevi wa kupindukia hadi Mama yake analalama.
Lakini pia alijiuliza kuhusu aina ya mtu aliemkuta nyumbani kwa Mbondya.
Mtumiaji wa dawa za kulevya, lakini pia alikuwa na kete kwenye nguo zake na kikubwa yule ni kahaba.
Je Mbondya hakujua hilo au nae ni mtumiaji? Lakini kwanini safari iliomhusu hakwenda na kwanini bado hajaripoti kazini tangu kuanguka kwa ile ndege? na inaonekana muda wote hakusafiri, kwanini asafiri hivi karibuni sasa!
Yalikuwa ni maswali bila majibu.
Pikipiki iliendelea kuburuza barabarani.
Alijikuta anamhitaji sana Mbondya kuliko hata kumhitaji mtu alienyuma ya mchezo ule,mana kumpata Mbondya ni hatua kubwa ya kumfikia mtu alie nyuma yake.
****
Boneka alikuwa bado yupo kwenye foleni huku muda wa kuonana na Vedi ukiwa unakaribia..
Akasikia ujumbe ukiingia kwenye simu.
Akaufungua!
.
Ulitoka kwa Vedi na alimjulisha tayari anamsubiri.
Vedi nae baada ya kutuma ujumbe alienda chumbani kwa lengo la kujilaza kidogo ili walau apate kupunguza kidogo mawazo yake kwa kijiusingizi kitakachomchukua.
Mara Jay akaingia.
"Nilisikia una mgeni badae kidogo sio!" Jay alihoji.
"Ndio na anakuja muda sio murefu" Vedi alijibu.
"Ok sawa!" Jay alisema huku akitoka chumbani na kwenda sebuleni.
Jay alipokea ujumbe ambao ulimwelekeza ya kuwa ajitahidi Vedi asionane na Boneka na hiyo ni baada ya Jay kutoa taarifa ya Vedi kutembelewa na Boneka pale kwake.
Na alipokea ujumbe huo uliosisitiza ajitahidi wasikutane.
Atafanya nini, hilo ndilo alilohitaji kufanya na kujiuliza.
Aliona akimtaka watoke itakuwa ngumu sana kwake July alias akizingatia ya kuwa siku za karibuni wamekuwa hawana maelewano mazuri kabisa.
Akazidi kuwazua bila jibu.
Mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake.
"Muda wa kupata dozi unakaribia, hivyo mwambie aje hapa nyuma ataona gari jeusi alifuate na atakuletea. Ila baada ya kuhakikisha huyo bwana katoka hapo" Ulikuwa ni ujumbe wa Panga.
Akimtuma kwa kawaida sio rahisi Vedi kwenda na atakuwa na kiulizo, jambo ambalo litasababisha Boneka amkute hapo.
Jay akaanza kujinyonga akiwa amekaa kwenye sofa, alijinyonga mithili ya mtu anaepitia mateso makali ya maumivu ya tumbo.
Alipoona juhudi zake hazimvutii Vedi; ikabidi atoe miguno ya maumivu na hila zake zilifanikiwa.
Vedi alisikia ile miguno, akatoka haraka ili kujua kulikoni.
Alikuta Jay anaugulia maumivu huku akiwa ameshika tumbo na kutumbua macho kama mgonjwa anaekaribia kukata roho.
"Shida nini tena jamani!!" Vedi aliuliza kwa mashaka huku akihangaika kumshika hapa na pale.
"Tumbo linaniuma sana na kitu kimebana kifuani" Jay alizungumza kwa tabu kidogo.
Vedi akakurupuka ili kuwahi kuchukua dawa za tumbo ambazo huwa wanaweka ndani kwa dharura.
"Tafadhali naomba nisikilize kwanza" Jay alimwambia Vedi baada ya kuona anataka kutoka na kumwacha.
Vedi akarejea kumsikiliza.
"Kuna jamaa zangu hapo nyuma wana gari jeusi, tafadhali nenda wambie waje mnipeleke hospitali"
Vedi hakutaka kusubiri, akatoka ndani mbio na kuelekea nje kuelekea usawa alioelekezwa.
Alipotoka tu, ni wakati huo ambao Jay alinyanyuka na kwenda chumbani kuchukua simu yake na kuwasiliana na Panga.
"Naombeni msifanye kitu kibaya huyo binti jama!" Jay aliwandikia huo ujumbe.
"Sasa kagua vitu vyake, kuna kitabu kidogo cha kumbukumbu, tunaomba ukichukue na utoke nacho nje" Panga alimwandikia Jay.
Jay akahaha kukitafuta hicho kitabu huku roho yake ikiwa inahangaika na kichwa chake kikipita kwenye tanuru la fikira kujua kitu gani wale jamaa watakifanya kwa Vedi.
Roho ilimsuta ila hakuwa na la kufanya, alihitaji kufanya linalowezekana ili Vedi asiingie matatizoni.
Atafanya nini wakati ameshamtuma kwa wabaya wake.
"ooh shiit!" Alijisemea huku chozi la usaliti likimdondoka,hakika alipitia hali ngumu.
Mikono yake inayotetemeka iliendelea kuhangaika kupekua mikoba ya Vedi.
Hatimae alikipata kitabu kile kikiwa kina kalamu iliobanwa pamoja nacho.
.
Akaanza kutoka ili akipeleke kama alivyoelekezwa.
Lakini alisita kidogo alipofika kwenye mlango wa chumba chake.
.
"Kama hiki nikiwapa ndo watatuua itakuwaje?".Jay alijiuliza bila kupata majibu..
Akajikuta akiwa na maswali mengi kuliko majibu,huku akiwa amekishikilia.
.
Akaamua kutoka ili apeleke!...
Kitu ambacho haukujua ni kuwa kikifika mikononi mwa Panga; wao watakuwa hawana thamani tena.
Hilo hakujua kamwe!
..
*****
ENDELEA KUWASILIANA NAMI 0758573660
0624155629.
Whatsapp 0658564341.