Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
RIWAYA; BAHARIA
NA;BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
VITABU VILIVYOPITA.
• MPANGO WA CONGO
• DAKIKA ZA MWISHO
• URITHI WA GAIDI
• OPERESHENI JICHO LA PAKA
• SAUTI YA MTUTU
• MBWA WA GETI
• KALENDA YA IBILISI
******
--Gazeti Mwananchi—
Ndege ya shirika la ndege la Tanzania imepotea dakika ishirini tangu ilipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA. Ndege hiyo ndogo ilibeba watalaamu wa tafiti za magonjwa ya binadamu wapatao watatu. Taarifa zaidi zinasema ndege hiyo ilikuwa ikielekea jijini mwanza katika uzinduzi wa tiba ya magonjwa ya akili na ukichaa kwa binadamu na wanyama, tiba ambayo ilikuwa imegunduliwa na watalamu hao.
Hadi gazeti hili linaingia mitamboni hakuna taarifa zaidi zinazohusu ndege hiyo na wagunduzi hao wa tiba ya magonjwa ya akili...
Siku mbilli mbele..
---Gazeti la Uhuru—
Mabaki ya ndege ya ATCL yamepatikana katika pori la akiba la Inara Njombe. Taarifa zaidi zinasema hakuna mabaki ya miili ya rubani ama matabibu waliokuwamo katika ndege hiyo. Uchunguzi zaidi bado unafanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo na utafutaji wa abiria ambao walikuwa ni matabibu bado unaendelea ili kuthibitisha ni wazima au wamepoteza maisha. Tutazidi kukupa taarifa kupitia mitandao yetu ya kijamii kuhusu kile kinachoendelea…
----1------
Miezi nane badae
Unaweza kuwa ni ushamba ndio ulikuwa unamsumbua au la basi ni vile maji hayazoeleki. Ila kwa binti huyu ilikuwa ni ushamba na uoga tu zaidi ndivyo vilivyokuwa vikimsumbua mana kila mara alikuwa anawaza ukubwa wa bahari na vipi kama chombo walichomo kikizama? Mawazo yake yalimjengea woga katika nafsi yake na kila mara alikuwa anatajiwazia namna ambavyo atakuwa anahangaika kuinusuru roho yake wakati chombo hicho alichomo kikienda mrama.
Alichukua chupa ya pombe kali na kumiminia kwenye glasi na kufakamia funda kadhaa lengo likiwa ni kuichangmsha akili yake ili iende sawa na tukio lililokuwa likiendelea mle ndani ya meli kubwa wastani ila ya kifahari sana.
Ndani ya meli ile ya kampuni ya Serengeti Marine kulikuwa kuna tukio maalumu lililokuwa linaendelea kwenye moja ya kumbi za kisasa zilizoko mle kwa matukio maalumu.
Watu wawili walikuwa wanafunga ndoa, ndoa ambayo iliandikwa karibu na kila kituo cha radio; gazeti na runinga. Ilikuwa ni ndoa ya kifahari sana kuwahi kutokea ndani ya nchi ya Tanzania.
Vigegele vilikuwa ni kama vimemzindua binti yule ambae alikuwa amekaa mwishoni kabisa mwa ukumbi ule huku akili yake ikiwa imegawanyika mara mbili, huku akiwaza maji na huku akiwaza sherehe iliokuwa inaendelea.
Aliwatizama maharusi wale ambao walikuwa wanafuraha ya ajabu nyusoni mwao.
Akatabasamu huku na yeye akiungana na wanawake wengine kupiga vigelegele.
Harusi ile ilikuwa ni ya rafiki yake kipenzi alietwa Nyamizi.
Kiukweli katika maisha yake hakuwahi kudhani kama angefikia hatua ya kupanda meli na hakuwahi lau kufikiria kuipanda hata bahati mbaya tu,ila kwa upendo aliokuwa nao kwa rafiki yake wa karibu Nyamizi ulimfanya avunje kiapo chake cha kutokuja kuutumia usafiri huo wa majini.
Nyamizi alikuwa anaolewa na mchumba wake mfanyabiashara kijana kabisa alietwa Boneka na sherehe za ndoa yao waliamua kuzifanyia ndani ya meli ya ya Mv Upendo kutoka katika kampuni za Serengeti Marine.
Angewezaje kusimamia msimamo wake wakati rafiki yake kipenzi anafurahia ndoa yake, na angeonekanaje mbele ya watu waliojua vizuri mahusiano yake na Nyamizi!
Alihudhuria harusi ile ya aina yake na kila aliengia mle ndani alikuwa ni mtu alieheshimiwa na familia za pande mbili zote yani familia ya upande wa Boneka na familia ya upande wa Nyamizi.
Vedi alikuwa amecheza muziki na kuchoka na ndipo alipoenda kupumzika kwenye viti vilivyokuwa mle ukumbini huku watu wengine wakila na kunywa kwa furaha. Maharusi walikuwa wamekaa pahali maalumu palipokuwa pameandaliwa kwa ajili yao na kila aliehitaji kuwapa chochote alifika na kupiga nao picha na kufurahi pamoja.
Vedi pamoja na watu kadhaa walikuwa wameshafanya yote na baadhi walibaki ni kula na kunywa na wengine walielekea kujipumzisha kwenye vyumba vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yao ndani ya meli ile.
Meli ile ilikuwa imetengenezwa kwa oda maalumu ili kuvutia wateja wanaopenda kujipumzisha wakati wa safari, hivyo haikuwa na shida kwa walioikodi siku hiyo kutumia vyumba hivyo kujipumzisha na wale waliohitaji kukesha waliendelea kuserebuka wakila na kunywa.
Vedi hakuwa muumini mzuri wa kukesha ama kuserebuka usiku, hivyo pombe kidogo aliokunywa alijikuta ikimchanganya na alihitaji kujipumzisha.
Alimfuata mhudumu mmoja wa meli aliekuwapo maalumu kwa ajili ya kuelekeza watu mambo kadhaa kuhusu huduma walizohitaji. Aliomba kuelekezwa sehemu ya kulala mana alichoka kwa mserebuko aliokwisha serebuka.
Mhudumu yule alimpeleka upande wa chini wa meli ambako kulikuwa kumebaki na chumba kimoja tu baada ya vingine kuwa vimeshajaa na ni kama bahati kukipata hicho alichopata.
Alipokwisha kupewa chumba, alijitupa Kwenye kitanda kidogo kilichokuwa mle ambacho kilitosha kulala mtu mmoja tu, hakuhangaika hata kuvua viatu na usingizi ukampitia.
Ilikuwa karibu saa zima tangu alale, alisikia sauti kama za mabishano kutoka ndani ya vyumba vilivyokuwa kule chini.
Hakutilia mana sana kwa sababu kulikuwa kuna hekaheka nyingi kila pande ndani ya meli ile.
Aliendelea kuuchapa usingizi huku kichwa kikimuwia uzito wa kilo kadhaa kutokana na kugida pombe.
Mzozo uliendelea na sasa waliokuwa wanazozana walikuwa karibu na chumba chake. Vedi alistuka toka usinguzini tena, ila hakusikia kilichokuwa kikiongelewa vyema kulingana na kuwa na wenge la usingizi mzito.
Mkojo!.
Mkojo haunaga adabu siku zote, alibanwa na alijisikia kujisaidia ila kwa kuwa hakuwa mzoefu katika upandaji wa meli, hakuwa amejua upande vilipo vyoo na ukichanganya woga wa kupanda meli basi hakuwa amehangaika kabisa kujua vilipo vyoo.
Akanyanyuka kufungua kile chumba na kutoka nje ambako kulikuwa kuna korido pana na ilikuwa imetenganisha vyumba kadhaa ambavyo vingi vilikuwa vimeandikwa kuonesha vinatumika na mabaharia na vingine viliandikwa kwa kiitaliano na hakuelewa vilimaanisha nini.
Alizidi kuyumba kufuata korido ile upande mwingine tofauti na ule ambao waliingilia na baharia aliempeleka kwenye vyumba vile. Aliendelea kusonga taratibu huku kila mara akiyumba na kubeua.
Korido ile ilimfikisha hadi upande ambao kulikuwa kuna ngazi zilizokuwa zikishuka chini zaidi kwenye meli ile.
Wala hakujiuliza bali alizidi kwenda huku akisoma vyumba kadhaa vilivyokuwa na maandishi.
Kwa mbali alianza kusikia migongano ya vyuma na hewa nzito upande huo alikokuwa anaelekea.
Alikuwa amefika upande wa injini ya meli ile.
Akaamua kugeuza baada ya kuhisi hali ya hewa haiwezi kuwa rafiki nae tena.
Hakupiga hata hatua tatu akaona korido nyingine akaamua kuifuata korido hiyo ambayo ilimfikisha kwenye chumba kilichokuwa wazi na makororo mengi yalioonekana kuwa ya ufundi na dumu kadhaa za mafuta.
Kibofu kilikuwa kimejaa mkojo na ni lazima akojoe la sivyo angeadhirika.
Akaona chumba kile kinamfaa kumaliza shida zake harakaharaka ili arudi kuendelea kuukata usingizi wake kwa raha zake.
Tofauti na alivyodhani kwamba chumba kile ni kidogo,chumba kile kilikuwa kina upana wa kutosha tu na baada ya kuingia alibaini kwa mbele yake kulikuwa kuna taa zinawaka.
Hakujali!
Alianza kupapatua nguo zake za ndani na kuchuchumaaa huku akiwa amejibanza nyuma ya mapipa.
Alipokamilisha hitaji lake akasimama ili atoke kwenye kile chumba, ndipo aliposikia nyayo za miguu ya mtu ikiingia kwenye chumba kile kwa mwendo wa taratibu huku akijiongelesha peke yake.
Vedi akataka kutoka ili aendelee na hamsini zake akiamini ni miongoni mwa watu tu waliokuwa kwenye sherehe ndani ya zile meli.
Ila alijikuta anasita kutoka alipokuwa na kutulia kimya kabisa.
Mtu yule alimpita taratibu na kuelekea mbele kulikokuwa kuna waka taa.
Vedi alinyanyua kichwa chake taratibu na kumtizama mtu yule ambae alikuwa amevaa kofia kubwa ya pama kichwani mwake na koti zito mwilini mwake na alivaa suruali ya jinzi mpauko na mikono alikuwa ameiweka mfukoni.
Vedi alitoka pale alipokuwa akanyata na kujikinga nyuma ya pipa moja lililokuwa karibu na njia alioingilia na hapo aliweza kuona vyema upande ule kulikokuwa na mwanga wa taa.
Mtu yule safari yake iliishia kwenye kontena dogo na akalifungua kisha akaingia ndani yake.
Vedi alistajabu kidogo, tangu aingie mle ndani hajapata kuona mtu alievaa mavazi kama yale isipokuwa kila mtu alikuwa amevaa mavazi mazuri ya kuvutia na hata wahudumu na mabaharia kadhaa waliokuwa mle ndani walikuwa wamevaa mavazi maalumu kwa ajili ya sherehe ile ili watambulike kirahisi na wageni waliokuwa mle.
Sasa vipi tena mtu kuwe na mtu mwingine ambae hana mavazi maalumu na amevaa kiajabu ajabu namna ile?
Na ndani ya kile kikontena kafuata nini mtu yule.
Vedi hakuwa na wakumjibu na alitaka kutoka kuendelea na mambo mengine ila akajikuta anashindwa kufanya hivyo,hajui ni nini kilimsababisha kutaka kuendelea kubaki eneo lile.
Zilipita dakika zaidi ya tano bila kuonesha dalili ya kutoka kwa mtu yule na ndipo Vedi akataka kuondoka mana hakuona kama ni busara kuendelea kukaa pale.
Wakati anataka kunyanyuka ili aondoke,masikio yake yalinasa sauti ya muanguko wa kitu kama chuma kutokea kwenye kile kikontena,akarudi tena kujibanza pale alipokuwa awali na kutulia.
Haikupita dakika; mtu yule alieingia ndani ya kile kikontena akatoka huku akivaa kofia yake kichwani kwa mkono wa kulia.
Ajabu nyingine!
Mtu yule alikuwa amevaa miwani katika usiku ule.
Eeh makubwa!
Alijisemea Vedi huku sasa akiona mtu yule akimpita pale kwa mwendo wa haraka tofauti na mwanzo alivyoingia.
Mtu yule akatokomea akabisa na pale ndani alibaki Vedi peke yake.
Ni kiherehere chake tu kilichomsababisha aelekee kule kwenye kile kikontena,nae akaingia ndani yake.
Alikutana na giza zito na harufu kali ya kitu ambacho hakujua kama ni uozo ama ni vumbi lenye mchanganyiko wa vimiminika kadhaa.
Vedi akawasha simu Janja yake iliokuwa inamwanga wa kutosha tu kumulika mule ndani.
Tofauti na matarajio yake ya kuwa pengine mle ndani ni pachafu sana, la hasha kulikuwa ni kusafi licha ya kuwa kuna mpangilio wa meza za chuma mbili zilizokuwa zimewekwa kwa mtindo wa kulaliana, yani moja ilikuwa imesimamishwa kama kawaida na nyingine ilikuwa imesimamishwa kitako juu ya ile nyingine huku mgongo wake ukiwa umetazamana na Vedi na miguu ikiwa imetizama upande wa pili wa ile kontena.
Pale kwenye meza iliokuwa imeagamiwa na nyingine kulikuwa kuna kitabu kidogo cha kumbukumbu(Diary).
Hakukijali!!
Akapiga hatua zake taratibu na kuelekea kule ambako kulikuwa kuna miguu ya meza iliosimamishwa juu ya meza nyingine.
Alianza kwa kuona viatu vyeusi na suruali ilionza kutatuka,kisha akaona koti jeupe likiwa limefikia usawa wa magoti ya suruali aliiona.
Vedi akaanza kuingiwa na wasiwasi na alizidi kujongea na mara macho yake yakanasa taswaira ya ajabu kwenye miguu ya meza. Vedi aliruka juu na kupiga ukelele wa woga huku akirudi nyuma kwa hamaniko ya kile alichokiona.
Maiti ya mtu!!
Aliona mtu akiwa amesimama huku uhai ukiwa mbali na yeye,mtu yule alionekana kufa siku kadhaa nyuma na tayari ngozi yake ilianza kunatana na mifupa huku nyama na misuli ikiwa imeanza kuyeyuka mithili ya sponji.
Mtu yule alikuwa ameachama kuonesha alikufa kwa mateso na macho yake yalionekana kutumbuka kwa woga wa kifo kilichomkuta. Mikono ya yule mtu ilikuwa imetandazwa kwenye vyuma vilivyokuwa vinaunganisha miguu ya ile meza na miguu yake ilionekana kufungwa pamoja na kamba ambayo ilianza kuoza.
Ilikuwa picha ya kutisha machoni mwa Vedi;pombe yote ikamuisha na roho yake ikachafukwa.
Aliuwawa lini na kwanini; Vedi hakujua ila kitu pekee alichobaini ni kuwa mtu yule alikuwa amevaa mavazi maalumu ya wapishi wa meli, hasa koti lilikuwa limefanana sawa na makoti wanayovaa wapishi.
Mtu yule alikuwa baharia bila shaka kulingana na mavazi aliokuwa amevaa.
Vedi alishindwa kuelewa kwa nini jambo lile limetokea na kwanini auwawe afu aachwe mle mle ndani ya meli bila kutupwa kwenye maji au kuzikwa kabisa. Alishindwa kujua ni nini kusudi la kuihifadhiwa pale yule jamaa.
Au hawajui kama kuna mtu kafia kwenye karakana hii ya ufundi?
Hapana!!
Yule mtu aliemuona akiingia mle anaonekana anajua kinachoendelea ndani ya kikontena.
Aisee!!
Vedi alikurupuka kutoka alipokuwa na kutaka kukimbia kutoka nje ila wakati anafika kwenye meza iliobeba meza nyingine yenye maiti ya mtu, aliona tena kile kitabu kidogo cha kumbukumbu, akakiokota na kukitia kwenye mfuko wa koti la suti yake kisha akarudi tena kuitazama ile maiti na akaona kitambulisho kilichokuwa kinang’inia shingoni mwake, akaamua kukipiga picha na hapo akanasa sura nzuri ya kijana iliokuwa kwenye picha ndogo ilioambatanishwa kwenye kitambulisho kile. Ila hakuona jina kwenye kitambulisho kile na alipokuza picha aliopiga aliona likiwa kimekwanguliwa.
Kwa nini?
Hakujua sababu ya kukwanguliwa kwa jina kwenye kitambulisho kile.
Mikono ilikuwa ikimtetemeka na roho ilikuwa ikimdunda, hajawahi kuona mtu akiwa amekufa katika mateso namna ile.
Kwa nini wamekuuwa baharia!!?
Hakujibiwa na maiti ile.
Vedi aliamua kuondoka ndani ya kikontena kile, akapiga hatua chache na kabla hajatokeza kwenye mlango akasita kutoka.
Nje ya kikontena kile kulikuwa kuna mtu akiongea na mwenzie kwenye simu..
Kwa wizi wizi akarefusha shingo na kufanikiwa kuchungulia nje ya kikontena kile.
La haula!!
Alikuwa ni yule bwana aliemuona akiingia na kutoka ndani ya kikontena kile kidogo ambacho sasa yeye ndo alikuwamo.
Vedi alitamani kufanya miujiza ya kina Shumireta ya kupotea ila haikuwezekana, na alitamani apige kelele ila kwa alivyoona meli ile ilivyo hakuna ambae ambae angemsikia zaidi ya yule bwana ambae alikuwa nje ya kontena na alionekana sio mwema kabisa na wakati huu alikuwa amevua kofia na kufanya upara wake uonekane na kichwa chake kikubwa kilichojaa kisogoni.
Haieleweki sababu gani ilimfanya yule bwana avae miwani usiku.
Vedi alibaki akitetemeka.
Mara simu yake ikatetema kuashiria inaita.
Vedi akaruka juu na kuitupa chini na kuiacha ikisambaratika hovyo.
Aliiogopa mtetemo wa simu yake mwenyewe.
Yule bwana kule nje alisikia msambaratiko wa kitu kwenye kikontena kile na akageuka kutazama.
Ebanaee
Vedi mkojo uligonga hodi langoni kwa kalichumbage wake na jasho la kucha lilimtoka.
Tukutane badae!!