Bahari Beach, Dar: Uzinduzi wa Sera za CHADEMA toleo la 2018 - yaliyojiri

Kinachotia moyo Chadema inaonyesha ni kubwa sana bila Jeshi wala Ikulu..
Kuna watu wanasema inakufa... Sipati picha wao wakibaki bila Jeshi kama chama chao kitakuwepo.

M4C sio TBC.
 
Yaani chama kimechokwa.. ni hao waliopo tu wakurekodi inaonekana hata chai hawajapewa.. njaa zimewabana..

Nashangaa nyie wa humu iweje hampo humo.. haya iteni wapita njia wasaidie kupajaza basi.. hata chai kuwanywesha si hamuwezi kushindwa.. 🤣🤣🤣
We kasichana hata mumeo amekuchokaa pia
 
Mkakati mpya Chadema uchaguzi 2020 waanikwa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanika mkakati wake mpya wa kuongeza wanachama na kueneza sera zake kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Kimesema mkakati huo unaohusisha uenezaji wa sera za kisiasa kuanzia ngazi ya familia, kimeanza kuufanyia kazi nchini kutokana na serikali ya awamu ya tano kupiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi 2020, uchaguzi mkuu ujao.

Katika mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, viongozi wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) walisema kuwa licha ya kuwapo kwa zuio hilo, chama kimeamua kuja na mbinu mpya za kufanya siasa, ili kiendelee kuvuna wanachama wapya na kunadi sera zake.

Makamu Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Hawa Mwaifunga, alisema baraza hilo ambalo limekuwa na mkutano wake wa mwaka kwa siku mbili kuanzia juzi jijini hapa, limeazimia kuwatumia wanawake kufanikisha mkakati huo mpya wa Chadema.

Mwaifunga alisema viongozi wa chama hicho sasa watakuwa wanafanya siasa kuanzia ngazi ya chini ya familia ili kuhakikisha zuio la mikutano ya kisiasa halikiathiri zaidi chama chao.

Alisema kuzuiwa kwa mikutano hiyo kumeminya demokrasia na kamatakamata ya viongozi wa upinzani iliyopo nchini imesababisha kina mama wengi kukosa nafasi na kuwaogopesha kufanya siasa majukwaani.

“Tunajua kuwa serikali sasa imekuwa mstari wa mbele kukandamiza upinzani kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuwakamataviongozi wa upinzani. Mambo haya yanasababishwa na kuminywa kwa uhuruwa watu kujieleza na kutoa maoni yao," Mwaifunga alisema.

“Kutokana na hali hiyo, baraza (Bawacha) tutafanya mafunzo kwa kinamama ili kuwajengea uwezo wa kujiamini, lakini ikumbukwe kuwa kwa sasa tumeanzisha mkakati mpya wa kufanya siasa kuanzia ngazi ya chini kabisa ya familia.

“Tunayo majimbo sita ambayo yanaongozwa na wabunge wanawake wa Chadema. Mkakati wetu sasa ni kuhakikisha majimbo yetu hayachukuliwi na kuongeza mengine zaidi.

“Tupo imara. Hata kama serikali imekuwa ikiwakamata viongozi wetu, wamezuia mikutano ya hadhara na kuna ukiukwaji wa katiba, tutapambana na tutaendelea kufanya siasa na kutoa mafunzo kwa wanachama wanawake jinsi ya kufanya siasa mbadala na kuwajengea uwezo wa kujiamini ili kuhakikisha tunaongeza majimbo zaidi.”

Majimbo sita yanayoongozwa na wabunge wanawake wa Chadema ni Kawe lililopo chini ya Halima Mdee, Mrimba (Susan Kiwanga), Bunda Mjini (Esther Bulaya), Tarime Mjini (Esther Matiko), Babati Mjini (Pauline Gekul) na Same Mashariki analoliongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka.

BAJETI HEWA

Mwaifunga pia alisema baraza hilo linaunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kwamba bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha ni 'hewa' na haitekelezeki kutokana na serikali kutokuwa na mipango yenye dira ya kumsaidia mwananchi wa kawaida.

Alisema wanaona serikali bado haijaweza kusaidia kukuza uchumi wa Mtanzania kutokana na matumizi mabaya ya fedha zinazokusanywa.

“Kutokana na hali hiyo, Bawacha tunaendelea kupiga kelele kwa ajili ya kudai Katiba mpya ili kujibu matakwa ya Watanzania sambamba na kutaka kuwapo kwa uhuru wa kufanya siasa, mihimili kuheshimiana sambamba na kuwapo uhuru wa kujieleza na kupata habari," alisema Mwaifunga.

Kiongozi huyo wa Chadema pia alisema baraza lao linaona kuna haja kuwa na mjadala wa wazi kuhusu hatima ya watoto wanaopata ujauzito wakiwa shuleni.

Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Bawacha, Grace Tendega, alisema kwa sasa wanaendelea na mikakati mbalimbali ya muda mfupi na mrefukuhakikisha chama kinaendelea kuwa imara katika kipindi hiki alichodai ni ngumu kufanya siasa.

Mkutano huo wa Bawacha uliwahusisha makatibu wote wa baraza hilo, kutoka mikoa yote pamoja na viongozi wengine wa juu kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa, uchumi na kujengeana uwezo wa kisiasa.
 
Tume ikiwa Hii waliyoikataa kuwa hawatasshiriki chaguzi au?
 
CHADEMA WAZINDUA KITABU CHA SERA…MBOWE ADAI NYERERE ALIITAMANI CHADEMA

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freema Mbowe akikata utepe kwenye kitabu kuashiria uzinduzi wa sera toleo la Mwaka 2018.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua kitabu cha sera za chama hicho toleo la mwaka 2018 ikiwa na sera 12 ambazo zimezungumzia namna ambavyo chama hicho kimejipanga kuinua maisha ya mtanzania na taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa toleo hilo, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema sera za chama hicho kimelenga kuinua uchumi wa mwananchi mmoja kama ilivyokua ikitamaniwa na mwalimu Julius Nyerere kupitia sera za ujamaa na hasa kupitia azimio la Arusha la mwaka 1967.

“Mwalimu Nyerere alisema sera za Chadema zilikua sera za kuinua maisha ya watanzania, kwa hiyo chama chetu sio chama cha kutafuta uhuru, bali sera zetu zimejikita zaidi kuhakikisha kila mtanzania anakua na maisha bora, sera hizi zimelenga maeneo 12 na tutaweza kuzifanyia marekebisho mara kwa mara pindi zitakapohitajika pia ni ruhusa kunakiliwa na vyama vingine.”

Miongoni mwa vitu ambavyo sera hizo zimejikita ni masuala ya katiba, utawala bora, uchumi wa jamii, mazingira, mambo ya nje, elimu na sayansi, mambo ya siasa ya ndani, pamoja na uchumi wa vijijini.

Chanzo- EATV
Mbowe%20na%20CDM.jpg
 
Maghufuli, baadaye historia itakuja kumuweka pahala anapostahili.

Atakuwa ndiye kiongozi aliyeuimarisha upinzani ndani ya mioyo ya watanzania kuliko kiongozi mwingine aliyewahi kutokea Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika!

History will be the judge.
 
We kasichana hata mumeo amekuchokaa pia

Ha ha ha haaaaaaa
Unatamani iwe hivyo..
Basi jua kabuku na besidei getaway wiki hii twende kula bata tutumie pesa tunazoingiza.. kama vipi lia tu maana nitahakikisha nafanya na shopping ya nguvu kama kawa.. eti rate ya pesa za nje zile za kule kwa nchi zenyewe zinazotumia tuendapo £ na $.. na za tshs ikoje kwa sasa.. maana bata ananipa haswaa.. chake changu..
 
Maghufuli, baadaye historia itakuja kumuweka pahala anapostahili.

Atakuwa ndiye kiongozi aliyeuimarisha upinzani ndani ya mioyo ya watanzania kuliko kiongozi mwingine aliyewahi kutokea Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika!

History will be the judge.
Mnajua kujifariji kweli kweli.
 
Heshima kwenu wakuu,

CHADEMA leo inazindua Sera toleo la Mwaka 2018.

Kauli mbiu ni "Tumedhamiria kutoa uongozi makini kwa taifa hili kwa kuwa na Sera Madhubuti na zinazotekelezeka na hatimaye maendeleo ya Uchumi. "

Tutapena kinachojiri hapa hapa kwenye hii thread.

======

UPDATES:
View attachment 877247
View attachment 877284
1125hrs: Wageni waalikwa, Wanachama na Viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasiri

1210hrs: Viongozi wanawasiri.

Viongozi wa CHADEMA wameingia ukumbini. Viongozi wote wa juu wapo, Mnyika, Sumaye, Lowassa, Mashinji, Mbowe, na Lazaro Nyalandu.

Ubalozi wa Nigeria, Marekani

Shekh Rajab Katimba anafungua kwa sala akifuatiwa na Peter Msigwa kwa upande wa Wakristo.

1220: Baada ya Salum Mwalimu kufanya Utambulisho, Katibu mkuu Mashinji anakaribishwa ba kusema, Sera za CHADEMA zimekuwa zikitekelezwa kwa miaka 25 sasa. Leo tunafanya rejeo la Sera zetu.

Mpango wa maendeleo ya taifa huathiliwa sana na chama kilichopewa Uongozi.

Hata janga lililotupata ni kutoka na mfumo wetu wa uchumi. Ungekuwa nj mfumo wa Soko, ungekuwepo ushirikishwaji wa Serikali na Sekta binafsi. Huu ni muda mwafaka wa kuchagua Sera zilizo sahihi.

Wakati tunafanya rejea. Sera ni kitu kinachoathiriwa na mazingira na wakati pia. CHADEMA imejitahidi kuwa na muendelezo. Sera zetu ni zile ambazo mkutano mkuu wa CHAMA wa 1995 ulizipitisha. Sasa tunafanya rejeo. Sisi ni chama cha mlengwa wa kati, tumeegemea kulia. Tunataka kuweka wazi msimo wa chadema hasa wa kisera.

Tunataka kuwafahamisha watanzania namna Uchumi na Siasa ulivyo. Hatutaki uchumi unaowanufaisha wachache.

Hapa tulipokaa tupo njia sahihi kama taifa? Kila mtu anajibu.

Je, uchumi wa taifa letu upo vizuri? Lazima tukubaliane, uchumi wa kuendeshwa na serikali kama mfanyabiashara. Kama mtu anauwezo wa kufanya biasha apewe fursa.

Tumeishi miaka mingi lakini tumeshindwa kuoanisha kati ya Uchumi na siasa. Siasa lazima ziwe huru na wazi zikiwa na muongozo.

Hivi watu wengi wanaoshindwa uchaguzi mazungumzo yao ni yapi?
Wengi walioshindwa uchaguzi wanapenda kuwa na mtu imara zaidi baada ya taasisi imara zaidi.

Watu walioshindwa wanatumia muda mwingi kulalamika. Uchumi ukiyumba, lawama nyingi zinaenda kwa vyama vya upinzani kwamba tunazuia.

Ukiangalia muendelezo wa Sekta binafsi ambazo haziingiliwi na Serikali zimekuwa zikizalisha.

Wengine wanadhani wapinzani wao ndo wanafanya wasifikie mafanikio, watawatesa, watawanyanyasa na kila aina ya ubaya. Waandishi wa habari watashambuliwa.

Leo hii tumeleta kesho yetu mbele yenu

Lengo sio kubadili msingi, tunaendelea na uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli kwa watanzania. Uhuru wa kujieleza kusikilizwa na kusikiliza,

July 1992 chadema ilitambuliwa kama chama cha Siasa. 1993 chadema iliandika sera za awali, (uchumi wa soko)

1995 tulishafanya reform hadi mabadiliko ya bendela zetu.

Misimamo yetu ya kisera ni pamoja na Wape nafasi wapinzani waongee halafu mtaawala afanye maamuzi

Chadema tunaamini haijalishi unatokea wapi, rangi au kabila. Tunachotaka ni unaleta maendeleo kwa watanzania na nchi kwa ujumla, ndo maana hatuna tatizo na uraia pacha.

1240hrs: Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe anaongea.
View attachment 877377
Anaanza kwa salaam kwa makundi mbalimbali.

Anaomba watu wasimame kwa dakika moja kukumbuka waliotangulia mbele ya haki katika ajali ya MV. Nyerere.

Nia tunataka Tanzania moja yenye kupendana na lengo moja la kitaifa.

Tunazindua toleo letu tukiwa katika hali ya uhasama ambao hausitahili.

Nchi za wenzetu waanakuwa na upinzani wa hoja, mawazo na dira zinazotambulisha msingi, imani, mitazamo na dira ya chama cha kisiasa.

Sera zetu ni mjumuiko wa watu wengi kwa muda mrefu. Chama chetu kinakuwa, kinapokea watu tofauti, wanakuja na mawazo mapya ya kujenga. Sera za chadema zinalenga kuangalia historia ya nchi yetu inatokea wapi?

Huwezi kuijadili sera ya nchi hii bila kuangalia awamu ya kwanza ya Uongozi wa Mwalimu ambao wote tunakubaliana kimsingi ni kiongozi mzuri. Mwalimu alikuwa na misimamo ya kisera na kiitikadi. Sifa ya Nyerere inamtofautisha na kiongozi yoyote wa leo.

Utawala wowote unakuja na kutoka. Mwalimu alifanya kwa upande wake akamaliza muda wake lakini alitujengea misingi mikubwa ya haki za binadamu na taifa letu.

Mwalimu alitujenga tukawa taifa moja, ni vipi misingi hiyo imeendelea kuheshimiwa na viongozi wanaofuatia?

Kuna mambo yalitengeneza dira

1961 hadi 1965 nchi yetu ilikuwa inaongozwa na vyama vingi vya siasa. Mazingira ya kiuchumi na kisiasa, mwalimu aliona ili kujenga misingi imara ya umoja wa kitaifa, watanzania wakakubali kuwa na chama kimoja cha kisiasa cha TANU.

Pamoja na kwamba tuliachana na vyama vingi mwaka 65 lakin tukio la kiuchumi la 1967 likafanyika azimio la Arusha

Nyerere alianzisha Uhuru na umoja na uhuru na kazi uhuru na maendeleo ambapo Nyerere aliandika viatu. Uhuru wa watu sio uhuru wa Viongozi. Haya ni mambo ya msingi wa baba wa taifa aliyapigania.

Umiliki wa njia za kiuchumi ilikuwa mikononi wa sekta binafsi. Sana sana wageni.

Kingine kilichotokea ni 1967 waliamua nchi iwe ni nchi ya Kijamaa. Kuanzishwa kwa fikra za kijamaa, kilipelekea kutaifishwa kwa vitu vilivyokuwa kwenye Sekta binafsi kama mashamba, viwanda, mabenki, nk.

Nyerere aliamini kama taifa tungeweza kujikomboa kiuchumi akaanzisha mashirika ya Umma. Jambo hili lilileta changamoto. Ilipelekea wawekezaji waanze kuhamisha mitaji yao kwenda nchi mbalimbali. 1971 tulitaifisha majumba. Haya majumba ya national housing yalikuwa ni majengo ya wstu wa nje walikuwa wamejenga, ilitaifishwa na serikali Tanzania nzima. Jambo hili lilileta mtikisiko mkubwa kiuchumi Tanzania ambapo wafanya biashara walihamia nchi nyingine. Siasa za ujamaa na kujitegemea zilikuwa na mabaya yake ili zilitupa misingi ya taifa yetu kama jamii

Vijiji vya kijamaa ilikuwa ni nia njema ambayo haukupokelewa vizuri na watanzania kwani wengi walikuwa na makazi ya kudumu

1973 hadi 74 nchi yetu ilikumbwa na ukame, hifadhi ya fedha za kigeni zikatumika kuagiza vyakula nje. Katika hiyo hali Nyerere aliruhusu kuagiza Chakula kutoka zimbabwe na afrika ya kusini.

Kipindi hicho yalianzishwa mashirika mengi ya umma, yote yalimilikiwa na Serikali amabyo yalitegemewa kushika uchumi wa nchi. Baadae yakageuka mzigo kwa watanzania yakiwemo madeni. Yakaanza kuendeshwa kisiasa zaidi.
View attachment 877482
1978 Tuliingia vita ya kagera ambapo mimi nlikuwa form six katika Shule ya Sekondari ya Ihungo. Pamoja na yote hayo, tulikuwa tunasiaidia nchi nyingi za Afrika kujiondoa mikononi mwa wakoloni. Tuliingia vita ya Kagera tukiwa nchi Masikini. Vita ile ilipigana na watanzania wote, sio wanajeshi tu. Madereva, mgambo, raia wa kawaida nk. Utaifa uliojengwa haujawahi kupatikana. Vita ile ilituumiza kama taifa kwa misingi ya uchumi. Uchumi wetu uliyumba sana.

Katika kipindi hiki import yetu ilikuwa kubwa kuliko export na kilimo kilikwama.

Mwalimu aliongoza nchi hii kwa miaka 24 akaweka misingi ya utu.

Miaka ya 1980 kuendesha gari siku ya jumapili lazima upate kibali kwa mkuu wa mkoa sababu mafuta yalikuwa ya shida. Sabuni, viatu, nguo nk vilikuwa havipatikani.

Kununua gari ilikuwa upate kibali kutoka Ikulu.

1983 bunge liliunda sheria ya kuzuia magendo na kuhodhi mali. Waziri mkuu akiwa Sokoine. Kesi za uhujumu uchumi ziliumiza sana uchumi wetu.

Ilidhibitika pasipo shaka kwamba uchumi wa mfumo wa kijamaa, ulishindwa katika mataifa menginkama. Zimbabwe Angola, Msumbiji nk. Hadi ukuta wa berlin ukavunjwa.

Ujamaa ulitujenga kuuhusudu umasikini, hata viongozo wanaona sifa ya kujitangaza wao ni masikini. Kama chadema tunataka nchi watu wahusudu utajiri. Umasikini sio sifa ni laana.

Tunahitaji watanzania wenye kuuchukia umasikini na wananchi wenye kuuchukia umasikini sio kuuhusudu. Huu ndo ugonjwa wa nchi nyetu.

Ujamaa uliua demokrasia ya nchi hii. Maamuzi yote kuhusu maisha yetu yalifanywa na Serikali. Uhuru wa watu kuanzisha biashara haupo. Ukiwa na magari mawili unaonekana ni mwizi, ukiwa na duka unaonekana mlanguzi. Tulisababisha umasikini wa fikra. Yaani kiongozi ili uonekane mtu wa watu lazima uwe masikini. Hiyo hali chadema tunaikataa. Uadilifu, uaminifu ndo tunaangalia.

Nmebahatika kuwa muanzilishi wa chama hiki.

Tulisema Tuanzishe chama cha siasa kitakachowezesha watu kujiendeleza na kuinua uchumi wao. Tulikataa uchumi hodhi. Tulisema ujamaa umeshindwa ambao CCM walinga'ang'ania

Mwaka 1993 tulitekeleza Sera na tukampa Mwenyekiti wetu azipeleke kwa Mwalimu Nyerere, sera zilizokuwa zinaupinga ujamaa. Baada ya kupitia akasema waziwazi kwamba nisoma sera za chadema na nmekubaliana nazo. Akasema ni wakati wa kubadilika. Rais ndo alimshinikiza mwinyi tukubali vyama vingi vya siasa. Huwezi ukajenga maendeleo kama hakuna uhuru wa watu wala demokrasia.

Anaweza akaja mtawala akavuruga, lakini hakuna mtawala ataishi milele. Lakini vuguvugu la demokrasia litaendelea miaka nenda rudi. Leo tuna watu tofauti, hawa Mawaziri wakuu wasitaafu walikuwa Wajamaa hawa, ila sasa wapo kwenye Uchumi wa Soko.

Hiki si chama cha ugomvi bali ni chama chenye mapenzi mema na nchi yetu.

Tumekuwa na sera hizi mwaka 1993.

Walioko madarakani watuambia sera zao za uchumi wa leo.
Sera zetu tunazozizindua leo zinajikita katika maeneo makubwa matatu.

1.Sera zinazolinda uhuru na Ustawi wetu. Kujenga barabara daraja reli bila kuangalia usitawi wa watu unakuwa unajidanganya.

Na huu uhuru unatakiwa uwe katika katiba. Sera zinazolinda uhuru wetu ikiwemo Utawala wa Sheria. Tuna mihimili Bunge, mahakama na Serikali je inasaidia? Bunge linasimamia serikali? Mahakama zinatenda haki bila kuingiliwa?

2.Sera ya kujenga Misingibya Uchumi wetu. Uchumi unaojenga na kuwezesha Sekta binafsi. Haki ya jamii kupata maendeleo nso mlengo wetu

3. Sera zinazolinda na kuhuwisha jamii kama huduma ya maji, barabara, hospitali nk.

Tumengwa katika dhana ya kufikiri serikali ikijenga chochote kile ni zawadi kwa wananchi. Huu ni wajibu wa Serikali sio ombi.

Mambo ya make Tanzania greater again. Ni lini Tanzania ilikuwa great? Hizi ni propaganda za kwenye. Mitandao na upotoshaji na kuiga mambo ya Marekani. Nao wanajiita #Mataga.

Mambo yanaongelea vitu, barabara, ndege, reli nk. Vipi usotawi wa watu?
View attachment 877445
Sera zetu zimefanyiwa utafiti. Tunaomba watanzania wazisome na wachumi wazichambue.

Sera za kujenga uchumi sio sera za ubaguzi. Wenzetu waliopo kwenye madaraka watajitahidi kichakachua, tunawakaribisha wafanye hivyo. Hatuna ubinafsi wa sera zetu. Hata pale watakapoiga, watushukuru. Wasione aibu kuja kwetu tuwape details wa sera zetu. Kama ambavyo mumeweza kubeba watu wetu, hazina ya watu katika chama chetu ni kubwa. Hatutakuwa wachoyo wa Sera zetu.

Mfumo wa utawala katika nchi yetu leo ni moja wapo wa sababu kubwa wa kukwama kwetu katika demokrasia. Nchi yetu ni kubwa sana, tumeweka madaka makubwa sana kwa rais na mawaziri. Watawala wetu wanakiwa wanahodhi mambo yote ya mstakabali wa nchi yetu.

Viongozi wa kisiasa wasiwe wa kuteuliwa bali wapigiwe kura. Namanisha wakuu wa Wilaya na wakuu wa mkoa. Hii itafanya wananchi wajiamulie mambobyao wenyewe. Sisi tuna kanda kumi. Sera ya kuhamia dodoma sidhani kama ni kipaumbele kama taifa.

Kitendawili na mahusiano ya Zanzibar ni lazima tuyafikirie sana. Tunataka Muungano ambao unatokana na maoni ya wananchi. Maridhiano ya muungano yanahitajika. Tanzania ni nchi Tajiri mno tunakwaza na watawala wanaodhani ndo wanaweza kutuamulia kila kitu..

1350Mbowe amemaliza kuelezea yaliyomo kwenye Sera

1440hrs: Anatoa neno la shukurani

Sumaye anasema. Lengo ni kujenga demokrasia ya kweli na watu kuchagua wanaowapenda.. Kwa style hii chadema itachukua nchi asubuhi na mapema.
CCM ilikuwa na Sera iliyoishia kwenye kamati kuu. CHADEMA ndo chama cha kwanza Tanzania kushirikisha watu kwenye Sera.

Nyerere aliwahi kuuliza, Kama wewe unataka kuiongoza nchi hii. Tuambie utaiongoza vipi na tutashiriki vipi. CHADEMA inasema tutashiriki hivi na kuwashirikisha hivi.

Utawala bora ndo swali linaowashinda watawala wengi. Wakishaingia madarakani wanabadilika.

Uchumi wa mfukoni mwa mtu ndo tunazungumzia. Huwezi sema nchi ya viwanda bila kuweka Sera na utaratibu. Kama uchumi umelemaa huwezi kuzungumza uchumi.

Ili kufurahisha umma, ndo maana mnasema hata viwanda vinne ni viwanda.

Huwezi kuboresha huduma za jamii kama uchumi haupo. Sera hii itawavusha watanzania katika matatizo mengi. Tuna uhakika wataibeba lakini hawataweza kuitekeleza bali wataipapasa.

Habari zaidi....Chadema imezidua sera mpya ya mwaka 2018 iliyogawanyika kwenye maeneo matatu.

Akizungumza leo Septemba 25, 2018 wakati wa uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema sera hizo zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati.

Amesema eneo la kwanza lililoko kwenye sera hiyo ni ile inayolinda uhuru wa wananchi.

Mbowe amesema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuzungumzia suala la maendeleo ya watu na uhuru, jambo ambalo wamelijadili kwa kina kwenye sera hiyo.

Amelitaja eneo lingine ni nafasi kuwa na sera zinazolenga misingi ya uchumi.

Amesema katika eneo hilo wameainisha ni kwa namna gani wananchi watapata huduma za kijamii.

Amefafanua eneo hilo limeainisha namna uchumi utakavyokuwa endelevu badala ya kuwa uliohodhiwa na Serikali.

Mbowe ameitaja sera nyingine ni zinazoilinda na kuihuisha jamii kupata huduma ya maji, barabara yasiwe mambo yanayofanywa na sekta binafsi bali yafanywe na Serikali.

"Sasa hivi kumejengeka dhana kuwa Serikali uliyojenga shule, zahanati inakuwa ni kama msaada, hii si sawa hayo ni majukumu ya Serikali," amesema Mbowe.

Mbowe amesema kabla ya kutayarisha sera hiyo wametumia mwaka mzima kufanya tafiti na kukusanya maoni kutoka kwa watu mbalimbali.
Wazee wa Ufipa,halafu kesho wanarudi na suti zao Ufipa halafu eti ndio tuwape nchi wakati hata Ufipa imewashinda
 
Yaani chama kimechokwa.. ni hao waliopo tu wakurekodi inaonekana hata chai hawajapewa.. njaa zimewabana..

Nashangaa nyie wa humu iweje hampo humo.. haya iteni wapita njia wasaidie kupajaza basi.. hata chai kuwanywesha si hamuwezi kushindwa.. 🤣🤣🤣
Muwaambie CHADEMA hatutaki tume huru ya uchaguzi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom