Bagonza: Tanzania ina tatizo la mmomonyoko wa Maadili. Watu wanaheshimu matokeo kuliko mchakato uliotumika kupata matokeo husika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Benson Bagonza, alipohojiwa na MwanaHALISI Online juu ya maoni yake kuhusu sakata la CHADEMA.

Sakata hilo liliibuka baada ya wanachama 19 wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu na Spika wa Bunge, Job Ndugai Jumanne ya tarehe 24 Novemba 2020.

Wanachama hao wanadaiwa kwenda kinyume na msimamo wa Chadema wa kutopeleka bungeni wawakilishi wake, wakipinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, kwa madai mchakato wake haukuwa huru na wa haki.

Alipouliza sababu za mgongano huo, Askofu Bagonza amesema Tanzania inakabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa maadili, kwa kuwa watu wanaheshimu matokeo kuliko mchakato.

“Nadhani kuna mpalaganyiko wa kimaadili katika Taifa letu, kwamba mara nyingi tuna heshimu matokeo kuliko mchakato. Nchi yenye maadili ina heshimu michakato kuliko matokeo, nchi isiyo na maadili ina heshimu matokeo kuliko mchakato,” amesema Askofu Bagonza.

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, wanachama hao wa Chadema waliokubali uteuzi ubunge viti maalumu wameheshimu matokeo badala ya mchakato uliotengeneza nafasi hizo.

“Penye maadili unahehsimu mchakato kuliko matokeo, pasipo na maadili unaheshimu matokeo, mchakato unauacha maadamu ufike unapokwenda, waliokubali uteuzi wa ubunge viti maalumu wameheshimu matokeo na si mchakato,” amesema Askofu Bagonza.

Kufuatia sintofahamu hiyo, Askofu Bagonza amekishauri Chadema kichukue hatua kwa wahusika bila kujali upendeleo.

“Tukio hili sio la kwanza kutokea katika historia ya nchi yetu, kwa hiyo, ningeshauri lishughulikiwe kama mengine yalivyoshughulikiwa yenye sura kama hii. Ili kuepusha mgongano wa kimaslahi,” amesema Askofu Bagonza.

Wito huo wa Bagonza umekuja siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuwaomba Watanzania kuishauri Kamati Kuu ya chama hicho, namna ya kulishughulikia suala hilo.
 
Punguani huheshimu matokeo kuliko mchakato.
Matokeo ni zao la mchakato uwe halali, batiri, sahihi, hovyo, nk. Kinachohitajika ni kuutathmini huo mchakato. Km mchakato wa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, kwa Katiba ya hicho chama chenye huo mgogoro, kama alivyoeleza Katibu Mkuu, ni jukumu la Kamati Kuu.

Hapa la kujiuliza ni kama kundi la watu wachache (ambao nao mchakato wa uteuzi wao una walakini) linaweza kuwa na uhalali wa mamlaka hayo! Ikizingatiwa kuwa ni kundi hilohilo hudai Tume huru ya Uchaguzi, demokrasia na utawala wa sheria. Ni kundi hilo hilo linadai Katiba mpya ya kumpunguzia Rais madaraka.

Je, tuliite ni kundi la Punguani, kwa lugha yako Mkuu Behaviourist?
 
Amesema kweli kabisa Dr. Bagonza, mchakato wa uchaguzi uligubikwa na uchafuzi mkubwa hivyo hata matokeo yake ni haramu pia. Na hata hao wabunge wenyewe bado wamepitia mchakato haramu kupatikana kwao huku wakinajisi sheria na taratibu zetu. Hawafai tena wafukuzwe tu.

Kazi ya leo kwa Chadema CC ni nyepesi sana kuwasikiliza kama formality tu lakini uamuzi unajulikana tayari ni kuwafukuza tu ili kulinda heshima na hadhi ya chama.
 
Tusiogope ni muhimu kwa CHADEMA kukabiliana na adui ndani na nje ya Mbunge.Wasamehewe waombe radhi na tamko utii kwa chama yatosha.

Mbali ya njaa bado Mdee ni yuleyule.
 
Tusiogope ni muhimu kwa CDM kukabiliana na adui ndani na nje ya mbunge.Wasamehewe waombe radhi na tamko utii kwa chama yatosha.
Mbali ya njaa bado Mdee ni yuleyule.
Don't force a square peg into a round whole. It will never fit.
 
Hahaha ushauri wangu kwa kamati kuu ya Chadema, ili chama kiendelee kuwepo basi hakina budi kuwatokomeza COVID-19.

Wanawake wapo wengi tu tutatafuta wengine.
CHADEMA ni mikakati na sio mawazo yenu,
Mnaweza kuondoka nyie na CHADEMA ikakuwa bila mgogoro na kuwa chama kikubwa.
Kinachotakiwa ni kubadili tabia ya uana harakati.
 
Matokeo ni zao la mchakato uwe halali, batiri, sahihi, hovyo, nk. Kinachohitajika ni kuutathmini huo mchakato. Km mchakato wa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, kwa Katiba ya hicho chama chenye huo mgogoro, kama alivyoeleza Katibu Mkuu, ni jukumu la Kamati Kuu...

Hicho kikundi ni kipi? Ni akina nani hao unaozungumzia?
 
Wanapenda kuitwa PhD, Dr lakini wakihojiwa I halali wa elimu zao wanaua watu.
Jikite kwenye mada. Angalau kwa suala la wazi linaloonekana. Achana na mambo ya hisia usiyoyafahamu na hoja za kukisia. Hata Halima uliaminishwa ni Kamanda wa nguvu, leo unaona tofauti na ulivyoaminishwa. Mangapi mengine usoyajua uliaminishwa kweli kumve si kweli? Hujui. Basi zungumzia hili ulopata ufahamu wake japo kidogo
 
Back
Top Bottom