Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Watanzania wametakiwa kusimamia ukweli na kutoyumbishwa katika imani yao ili kuliokoa Taifa lisiangamie.
Wito huo umetolewa leo Jumatano Desemba 9, 2020 na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, Dk Bensoni Bagonza wakati akihubiri katika ufunguzi wa Sinod ya 22 iliyofanyika shule ya sekondari Mukire jimbo la Mabira Wilaya ya Kyerwa.
Amesema mara nyingi uongo unaweza kuliangamiza Taifa hivyo lazima kila mtu kuwa tayari kusimamia ukweli na kukubali gharama za kusema ukweli huo.
"Mara zote msema kweli lazima achukiwe na kutengwa hivyo uwe tayari kusimamia, mara nyingi ukiwa muongo watakushirikisha ila ukisema ukweli watasema kwa huyo hata msipoenda, " amesema Dk Bagonza.
Amesema kuna dalili za kuliangamiza Taifa kwa sababu watu wanaamini uongo na kumchukia mtu anayesimamia ukweli.
Askofu Bagonza amesema Petro alitakiwa kuikana nafsi yake lakini wakati huu watu wanajitesa wenyewe kwa kupenda starehe na vitu vyepesi na ndiyo maana Taifa linaweza kuangamizwa.
Amesema kanisa si mali ya mtu na siyo taasisi binafsi bali ni mali ya Yesu hivyo wanaopanga kwa namna yoyote kuliangamiza hawatashinda maana Yesu alisema juu ya mwamba atalijenga kanisa na atalilinda.
Chanzo: Mwananchi