Bagamoyo Road haina 'service road' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bagamoyo Road haina 'service road'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bondpost, Jun 16, 2012.

 1. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kwa siku kadhaa, dhidi ujenzi wa barabara ya bagamoyo unavyoendelea, nimegundua kuwa njia za watembea kwa miguu na baiskeli hazitakuwepo. Ukiangalia toka makongo mpaka africana kuna dalili zote juwa hawatajenga service road. Najiuliza hivi wapanda baiskeli watapita wapi? Je gari ikiharibika unaipaki wapi? Vituo vya daladala wameweka barabarani kabisa, yani vimeibana barabara, nimeanza kugundua mapungufu haya na sijui mh. Magufuli anatuambia nini au anasubiri wakimaliza ndio aje na makelele yake?
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,906
  Likes Received: 2,335
  Trophy Points: 280
  Nakupongeza mkuu kwa kutambua hilo, lakini kwa kadri ya usukununu wangu service road zipo lakini ni jukumu la Serikali kupitia TaNROADS.

  Swali ni je TaNroads wamejipanga kwa hilo jukumu au ni mgumashi.
  Natumaini ujumbe huu utamfikia Magufuli.
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Service Road zipo mkuu, hebu tazama pale makongo upande wa kushoto kama unaenda tegeta utaona nafasi kati ya mitaro na itakapopita service road. Msikurupuke kabla ya kutafiti
   
 4. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kama wewe ni mtumiaji wa barabara ile utaelewa ninachosema. Au ukipita jaribu kufuatilia ule ujenzi. Ukifika pale interchick na ple jogoo utaona barabara ilipoishia then kuna ukuta wa chemi & cotex industry! Labda service road ya fly over itajengwa. Pamoja mie sio engineer wa barabara ila ujenzi wa barabara haiwezekani hata wasiwe wameandaa service road toka mwenge mpaka tegeta hata kwa kuijaza kifusi. Sijui lakini.
   
 5. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mtumiaji wa njia hiyo naishi Kunduchi, nilicho na uhakika nacho ni kuwa, service road ipo ila sio pana ni nyembamba hebu tazama pale makongo , lugalo utaona zile kalavati zimezidi upana wa mifereji ama zimekata barabara mpaka kwenye mifereji halafu kuna kipande kinazidishwa baada ya mtaro kwa ajili ya service road. Inawezekana kuna baadhi ya sehemu service road inaweza kuwa upande mmoja wa njia ila lazima iwepo
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  unasema kweli hii barabara magumashi vituo vyote vimewekwa ndani yaani bila kuangalia kwa makini unaweza kusema barabara haina vituo vya daladala mfano ni kituo cha pale makongo kilichokamilika yaani kiko ndani :nono::nono: barabara yenyewe nyembamba cjui huyu contractor katoka wapi

  Kuhusu service road sizioni maan from makongo mapak african hakna dalili, kama hili ni jukumu la tanroad kwanini wasiende sambamba na huyu contractor? au wanasubiri magumashi kama waliyofanya KILWA KWA MAGUMASHI YA MITALO
   
 7. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Bora mwenzangu unaetilia mashaka suala zima la ujenzi, maana huwezi kusema unajenga nyumba bila kufahamu wapi utajenga sewage system!

  Ni ukweli usiopingika kuwa pale makongo kile kituo cha basi kipo ndani ya barabara! Sijui wenzangu wanaojua ujenzi watasemaje maana kuna wajenzi wa aina mbili, wale wanaotaka bora liende au liende bora!!!

  Hata anaesema kuna service road nyembamba mbona pale lugalo kwa mfano pale super kuna ukingo mrefu, je hao TANROADS watakuja kulima tena baadae .
   
 8. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Tabu iliyopo watu wengine hawajui service road maana yake ni nini, anayesema ipo yeye mwenyewe anakiri ni nyembamba swali ni je scania 40ft linaweza kupaki? Kama la hiyo siyo service road itakuwa njia ya waenda kwa miguu
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Ujenzi wenyewe umechukua muda mrefu sana kumalizika.
   
 10. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hebu acheni ubishi wa kitoto, service road ipo. Tatizo mnaongea huku mko ndani ya magari, shukeni mtazame na kupima kwa uhakika. Service road ipo tena pande zote
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  na wewe utakuwa umeamka sasa hivi na usingizi ebu rudi ukalale

  Ebu niambie kutoka pale LUGALO mpaka bondeni service road iko wapi?

  Mkuu angalia hata viwango vya barabara hivi watarudia tena au ndo imetoka? maana ukipita na gari barabara ina manundu haiko smooth
   
 12. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kati xangu nawe hapa ni yupi mwenye ubishi wa kitoto bwana mkubwa? Unaona ile sam nujoma road ilivyo? Fananisha na ile ya bagamoyo! Ukitoka makongo hakuna service road nadhani we jamaa ni mbishi zaidi. Wacha nikaongee na engineer fulani wa ile barabara nimuulize.
   
 13. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kila mtanzania sasa ni mkandarasi lol
   
 14. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hebu chukua upana wa service road ya Mandera kisha nenda pale makongo ambako wameanza kujenga kingo za service road kisha kapime ujihakikishie. Kama alivyosema Wa Ndima watu wabishi kwa kutazama kwa macho
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hakuna service road,wanajenga njia ya watembea kwa miguu. Sitashangaa baada ya muda mfupi kusikia ujenzi mpya wa kupanua hiyo barabara tena kati ya Mwenge na Bunju maana ni nyembamba kulinganisha na idadi ya magari yanayotumia hiyo barabara!
   
 16. O

  Ogah JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  watu wengine sijui vipi.........nawaonea huruma Civil Engineers........kwani kazi zao mara nyingi hufikirika kama ni kazi rahisi na kama vile kufuata personal "thinking" ya mtu fulani huku watu wengine wanaona kana kwamba walio-design hawakufikiri kama wanavyofikiri wao kwa sasa........na pia hawaelewi ni hatua zipi zinapitiwa mpaka kufikia barabara inajengwa...........

  Contractor/Mkandarasi anajenga kazi iliyokuwa designed na scope yake imekuwa defined......kumlaumu mkandarasi eti barabara ni nyembamba au eti hakuna service road....ni ujinga...........na mtu unaposema barabara ni nyembamba what is your qualification to your statement/claim?........

  Kwa bahati nimeshirikiana sana kwenye shughuli zangu za kikazi wakiwamo ma-Civil Engineers kwa miaka mingi.........Ulizeni maswali ili mpate kuelimishwa na muwe na subira.........nawaomba Morani75 au fundimchundo au Waberoya waje watoe elimu hapa............


  ....acheni ku-undermine field/profession za watu........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,957
  Likes Received: 23,639
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ogah umemaliza. Well said.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,300
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni tafsiri ya "SERVICE ROAD",,wengine wanajua ni njia yoyote iliyoko pembeni mwa barabara kuu ambayo hutumika kwa waenda kwa miguu.

  Wengine wanajua kua ni njia itumikayo hata kwa magari makubwa in case umepata dharura.
  Tuseme kama umepata pancha basi unaingia service road na kubadili tairi yako, kisha unarudi main road.

  Tukijadili kwa mustakabali huu hakutakua na ubishi kama ipo au haipo.
   
 19. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  1. 1.Mwenye macho haambiwi tazama, huhitaji darubini wala hadubini kuona mapungufu yaliyopo kwenye majenzi hayo. Nawapa pole madereva wenzangu watumiao maji ya ilala/temeke chang'ombe wakati wa usiku, wajiandae ku-dive kwenye mtaro unaojengwa pembeni kabisa mwa barabara ukiwa hauna kingo yoyote ya kuzuia japo tairi ya gari. Anyway labda baadaye watapandisha kingo hizo za barabara ili ziwe juu kidogo lakini kwa sasa tumeumia.
  2. Kuhusu njia za waendao kwa miguu na watumiao baiskeli sipendi kuamini kama hawataweka njia hizo labda kama wana mpango wa kuwanunulia wakazi wote wa jimbo la kawe magari/pikipiki.
  3. Mwisho nawapa pole abiria wote mnaopenda kuongea kwa sauti ya juu (kupiga kelele) wakati mkisubiri usafiri vituoni, dawa yane imepatikana. Dawa ni kujengewa kituo karibu kabisa na jengo la Military Police (MP) kama ilivyo kituo cha Super ya Lugalo.
   
 20. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Afadhali wewe ndugu umeelewa ninachomaanisha! Maana kama itajengwa barabara ya pedestrians wakati kuna malori yanatoka Twiga cement yanaharibika kila wakati na hakuna pa kuyaegesha itakuwa ishu sana.

  Kumbuka watu wamejenga madale, bungu mpaka mapinga karibu na bagamoyo, pia kuna mradi unaotekelezwa wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya mkoa kule bungu, pia kuna airport, kuna bandari pale mapinga sasa sijui traffic ya magari itakuwaje!

  Ni sawa kuwa siwezi kumlaumu contractor, hata pia nafahamu ile barabara tunajengewa kwa msaada wa JICA ila hata kama ni msaada najua hawautoi bure kuna namna watafaidika tu kwa hiyo ishu ni kuangalia mbali zaidi na sio mipango ya miaka mitano. Itakuwa ni ufinyu wa kufikiri na kudhihirisha mapungufu ya uafrika wetu. Watembea kwa migu ile njia ni wachache ukilinganisha na traffic ya magari.

  Huwezi kuniambia kuwa kama unaweza kujenga njia ya waenda kwa miguu kwa nini ushindwe kuongeza mita mbili ya upana ukajenga njia ya msaada kwa watakaopata breakdown? If you can go fifty steps ahead then why not a hundred? Why?
   
Loading...