Bagamoyo mpya

ESAM

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,163
546
Dar es Salaam. Mradi wa Bandari ya Mbegani Bagamoyo, mkoani Pwani ndiyo mradi mkubwa wa uwekezaji nchini utakaoifanya wilaya hiyo kuwa na mwonekano.

Aidha, kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuliingizia taifa kiasi kikubwa cha fedha na kuzalisha fursa nyingine nyingi za kiuchumi.

Serikali ya Tanzania na Serikali ya China kupitia Kampuni ya China ya Merchants, ziliingia mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa bandari hiyo kwa utaratibu wa ubia kati ya sekta ya Umma na sekta Binafsi (PPP).

Ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo, ambao hufanyika kwa kipindi cha miaka mitano mitano.

Kupitia mradi huo, vipaumbele katika kipindi cha kwanza kuanzia 2011/12 2015/16 ni kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji katika sekta za nishati, usafirishaji na Tehama.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2014/15 bungeni hivi karibuni, Waziri wa wizara hiyo, Dk Abdallah Kigoda alisema kuwa wizara yake ina mpango wa kulipa fidia kwa wakazi wa maeneo yaliyofanyiwa uthamini Bagamoyo na maeneo mengine nchini.

Alieleza kuwa Mradi wa Bandari unahusisha Maendeleo ya Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (SEZ) katika eneo lenye ukubwa wa hekta 9,080 litakalojumuisha shughuli za ujenzi wa barabara, mitandao ya mawasiliano, mifumo ya maji na umeme.

Shughuli zitakazofanyika katika eneo hilo ni pamoja na viwanda, vituo vya biashara, vivutio vya utalii, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Huduma ya Makazi, Taasisi za Fedha na Makao Makuu ya Mkoa.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Mbegani Bagamoyo kutasaidia kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa katika Bandari ya Dar es Salaam na kuifanya Tanzania kuwa na bandari kubwa na ya kisasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Dk Kigoda alisema wataanza uendelezaji wa miundombinu ya msingi kwa Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (SEZ) yaliyolipiwa fidia kama vile Bagamoyo SEZ.

Aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga Sh7 bilioni kwa ajili ya kumalizia ulipaji fidia katika eneo la Bagamoyo.

Alifafanua kwamba mwaka 2013/14, kampuni 31 zilipewa leseni za kujenga viwanda chini ya Mamlaka ya EPZ na tayari kampuni nane zimeanza uzalishaji. Kampuni hizo zinatarajiwa kuwekeza mtaji wa jumla ya Dola za Marekani 485 milioni na kuajiri watu 10,276.

bagamoyo+clip.jpg


Muonekano wa mji wa bagamoyo utakavyokuwa baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekezaji wa bandari. Picha na Maktaba

Chanzo:Mwananchi
 
Kuna mijinga bado itaendelea kuamini hizi ahadi hewa.... Vipi mradi wa mji mpya wa kigamboni?.. CCM inatufanya watz mazezeta,,,
 
Tuweke records vizuri ili mwaka kesho wakati wa kampeni tuzungumze kwa data kwamba mliahidi hiki hamkufanya na sio waendeleze ngonjera za ahadi zisizoekelezeka.
 
Muhimu vyote ila kwasasa ilitakiwa tuanze na Reli kwanza

Reli ingefungua milango/fursa nyingi za biashara kati ya nchi wanachama wa EA mfano usafirishaji wa mazao hivo kunufaisha mkulima na wafanya biashara.
 
Makao makuu ya mkoa yatahamia Bagamoyo kwa sababu zipi tena
 
tutabakia kujenga kwa muonekanoooo wa picha tuuuu....vp khsu new kigamboni city
 
Mara Kigamboni's project way back, currently fly over na reli ya kisasa Dar es salaam, Bagamoyo na mengine kibao.. mwisho wa siku utekelezaji pole pole sana tofaut na mda wa makadilio kama c hakuna kabisa.. Tanzania naifananisha na mfa maji.
 
wakuu viwanja Bagamoyo bado vinapatikana?

Hekari moja napata kwa bei gani?


Kwa anayefahamu tafadhali,.
 
Kenya waanweza kwasababu chama kilichowaletea uhuru kilishapinduliwa muda mrafu, bongo mnaambiwa wakitawala wengine amani itatoweka nasi tunaamini, mbaya sana!
 
Kuna Las Vegas, Los Angeles, Atlanta, New York.............

Ila Makao Makuu ni Shamba kabisa, WASHINGTON DC.

Kuna Istanbul kaali, ila Capital City ni ANKARA.
Kuwe kuna mji kama huo kwenye ramani halafu makao makuu ya mkoa yawe Kibaha?

Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Kuna Las Vegas, Los Angeles, Atlanta, New York.............

Ila Makao Makuu ni Shamba kabisa, WASHINGTON DC.

Kuna Istanbul kaali, ila Capital City ni ANKARA.

Hata Tanzania kuna Dar ES Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Tanga zote "Cities" hizo lakini Capital ipo Dodoma "Town".
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom