Bagamoyo kuuzwa haikubaliki-wenyewe tupo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bagamoyo kuuzwa haikubaliki-wenyewe tupo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by enzihuru, Aug 19, 2012.

 1. e

  enzihuru Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za kuaminika ni kwamba kuna mpango wa kuiuza Bagamoyo kwa 'wawekezaji' kupitia mpango wa epz.kwa kuanzia, wamechukua zinga yote kwa kubadili ramani mara tatu na kuwadhulumu wananchi malipo yao huku wakiwatisha viongozi wao na kuwaamuru wakae kimya vinginevyo...wananchi wa zinga tayari wametishia kutishiriki sensa kama hawatapewa malipo yao,viwanja walivyoahidiwa na ramani ya kwanza kufuatwa. Kisha mpango wa kamal estates au mtu mwingine kubadili matumizi ya ardhi hayatakubalika hata kama mtalazimisha,tunajua ameomba kufanya hivyo. Je ni nia yenu watoto wetu waje kukosa sehemu ya kuishi? Je sisi hatuhitaji upepo wa pwani hata kama nyumba zetu ni za makuti?kuna sababu gani ya kubadili ramani kinyemela hadi kufikia kilomita mbili ng'ambo ya barabara kuuYA DAR-B'MOYO? Jeuri ya fedha na vitisho havisaidii, vinginevyo marehemu Ghadaffi angeendelea kuwepo kwa fedha na madavu yake.
  Wananchi wa wilaya ya Bagamoyo tuna haki ya kubakia kwenye makazi yetu ya asili na wote mmjjuuue hilo.wapnda amani wote naomba muone namna ya kuwasaidia wananchi waZinga-Bagamoyo na kwingineko wasidhulumiwe na kuishia kuwa manamba kwenye nchi yao.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kama ni kweli ujue wakati wa enzihuru unaelekea ukingoni.
   
 3. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  waache bagamoyo waipate fresh nadhani kwa hili watazinduka na kujua kwanini CCM watu hawaipendi. Na hii ndio jinsi CCM inavyoisaidia CHADEMA
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CCM na serikali yake wanatekeleza M4C 2015 si mbali.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Epza inavuka hadi ng'ambo ya barabara?
  Huwa nashangaa ni kwa nini wawekezaji wasiende maporini huko ili wapeleke miundombinu ambayo serikali legevu imeshindwa kupeleka. Is there a need to relocate people?
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  Ccm oyeeeee
  kidumu chama cha mapinduzi....

  Wakimaliza kuuza ardhi na maliasili watauza wananchi, kaeni mkao wa kuuzwa....
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Makubwa,Bagamoyo kuuzwa ni mwanzo wa nchi nzima kuuzwa kwa wawekezaji.
   
 8. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Katika moja ya mada zilizopita kulikuwa na Mada moja ilikuwa inaongelea Waziri Muhongo akataa mwekezaji mwenye dollar 20 mill. mdao bila kujali uwekezaji huo ulikuwa na masharti gani alilaumu kuwa hiyo ni hujuma. Mwingine leo analalamika kuwa bagamoyo imeuzwa kwa kuwa kuna mwekezaji mkubwa anapewa hilo eneo kwa njia ya EPZ.


  Hawa wote wenye maoni kama haya ni watanzania. Siku zote na shindwa kuelewa ni lipi jema kwetu wtz? do we real know what we want? au tunaongea tu pale tunajisikia kuongea na kupinga kila kitu na kuingiza siasa zisizokuwa na maana. Mimi siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini pia siamini kuwa kama ccm ikiondoka madarakani chama kitakachotawala kitafukuza wawekezaji na waachia wazawa kuendesha miradi yote mikubwa. Kama ndiyo huo utakuwa mwanzo wa kuianganiza kabisa Tanzania na itakuwa muhimu kwa wtz kuwa makini na wanasiasa wanaohubiri siasa zenye malengo ya kupinga uwekezaji wa nje. Hakuna nchi hapa duniani ambayo inakataa wawekezaji kutoka nje. Hata China ambao ni communist country hivi sasa wanakaribisha makampuni makubwa kwenda kuwekeza kwao. Sisi wtz tunahubiri kukataa uwekezaji. Nadhani imefika mahali sasa tuwe makini, vinginevyo tunaandika vitu ambavyo hatumaanishi katika uhalisia.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Serikali mufilisi kila sehemu wanataka kuuza,wamasai tumesikia wanahamishwa,kigamboni nao bush kawanunua haya sasa zinga nao wanataka kununuliwa ehee serikali mufilisi!
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Sasa mtoa hoja heleweki,
  Anapinga maendeleo au anasema hatashiriki sensa kwa vile hawajalipwa?
  Kwa uzoefu wangu wananchi wa eneo lote tajwa ni wavivu wa kupindukia.
  Kuuza ardhi kwao ni hobby.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nchi iuzwe mara ngapi? kuliko kufanya sensa ya watu na makazi ingekuwa busara kama tungefanya tathmini ya ardhi iliyobaki. Mbuga za wanyama zimeuzwa, migodi imeuzwa, Ardhi imeuzwa ( kwa afrika Tanzania tunaongoza kwa kugawa ardhi kwa investors), mijini kiwanja vinatolewa kwa wageni bila kujali matakwa ya dhahiri ya sheria.

  Sehemu ambazo wazawa wa mijini walikuwa wanalima mazao ya chakula, kwa mfano songwe( mbeya), mawiti ( tabora), wazo ( dsm), zinga ( bagamoyo) etc sasa hivi tunauza na kubembeleza wawekezaji waje kuwekeza na kusahau kuwa wazawa hawatabakiwa na sehemu ya kulima mazao yao ya chakula, kitu kitakachosababisha wazawa kuwa wategemezi wa supermarkets.

  Tubadilike tunaleta janga kubwa sana mbele yetu tujihadhari sana.
   
 12. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Imefika wakati kuiangalia upya hii sera ya uwekezaji, kumekuwa na malalamiko ya utekelezaji wake karibu nchi nzima. Kama nakumbuka vizuri hii sera iliibuka sana kipindi cha awamu ya tatu ya uongozi wa nchi, naomba kujuzwa hii sera haina mwisho??
  Nionavyo hii nchi itaingia kwenye ukombozi mwingine,huko nyuma tulijikomboa kisaisa kutoka kwenye mikono dhalimu ya wakoloni na huko tuendako hali itakuwa ngumu sana wakati watoto na wajukuu zetu watakapokuwa wanatafuta ukombozi wa kiuchumi katika nchi yao wenyewe. Nasema haya kwa nia njema tu na sio uchochezi kama baadhi yetu mtakavyotafsiri.
   
 13. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kiongozi usisahau na bandari ya Mtwara!
   
 14. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Tume thubutu,tume weza na tuna songa mbele!
  Idumu chama cha mwabwepande!
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuuzwa wakwere sisi tutaenda wapi?au tutakuwa watumwa kwenye ardhi yetu.....na kuishia kuwa vibarua!!
   
 16. l

  lugano5 JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 4,342
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  huo ni mwanzo tu..........makubwa yanakuja
   
 17. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kanda ya pwani watu wa ulojo mtayaweza ya magamba, hebu tusubiri
   
 18. e

  enzihuru Member

  #18
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  '
  Anapinga maendeleo au anasema hatashiriki sensa kwa vile hawajalipwa?
  Kwa uzoefu wangu wananchi wa eneo lote tajwa ni wavivu wa kupindukia.
  Kuuza ardhi kwao ni hobby.'
  Sensa ni ya watu na makazi sasa kama wataondolewa kwenye makazi yao,umuhimu wake ni upi? Kumbuka ni sisi ambao wakati wa operesheni vijiji vya ujamaa tuliondolewa kinguvu kuja kwenye hivi vijiji ambavyo leo wanatuuza tukiwemo tuondoke.Si kote nchini wameonja madhira hayo.Sasa kunyanyaswa tenaunadhani wewe ungejisikiaje? Akutukanaye hakuchagulii tusi, sisi tumezoea maneno ya waropokaji kama wewe wakati nazi, nanasi, samaki, na vitu kadhaa vinaliwa Dar tokea kwetu, na bado mnadai ni wavivu.Isitoshe hujasikia tunahitaji msaada wa chakula kama wengine ambao kwa asili hawaitwi wavivu .tunawajua na hatusemi hayo. Lakini Je, wavivu wanastahili kuonewa kiasi cha kunyang'anywa makazi yao?Haikubaliki.Tutasimama kutetea haki zetu za msingi na haki za vizazi vyetu.
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,536
  Likes Received: 10,457
  Trophy Points: 280
  mpaka kikwete akamalize ngwe yake wakati nchi imebaki theluthi.! Nina wasiwasi na washauri wa raisi nahisi sio watanzania halisi!
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  kila mahali pameuzwa?? Kigamboni, serengeti, na sasa bagamoyo.
   
Loading...