Bagamoyo Airport or Extension of JKN Intl. Airport?

JohnShaaban

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
464
114
Bandugu, nimesoma hii habari kwa mshangao mkubwa, pengine ni 'ignorance' yangu kuhusu umuhimu wa viwanja vya ndege. Lakini mshangao wangu ni hapa ambapo tunalipa watu wa Kipawa kupisha upanuzi wa JKN Intl. Airport wakati kumbe maandalizi ya ujenzi wa Bagamoyo Airport yanatafuna pesa!!! Someone mwenye ufahamu zaidi na haya masuala anielimishe tafadhali...!!!!!!!
TheCitizen said:
Feasibility study for new Bagamoyo airport starts
By Bernard Lugongo

Feasibility study for the construction of an international airport in Bagamoyo has already started.

The Tanzania Airports Authority (TAA) director general, Mr Prosper Tesha, said in Dar es Salaam yesterday that the authority had included in its annual budget funds for the feasibility study.

Speaking during the launch of Aviation Week, Mr Tesha said the new facility would be built on a 25,000-hectare land.

He said the feasibility study was being conducted by TAA experts.

Meanwhile, Mr Tesha told the gathering that more than a half of airports under TAA were operating on loss.

Mr Tesha said some 34 out of 58 airports that it operates were unproductive, forcing the authority to use funds obtained from Julius Nyerere International Airport to support their operations.

"We appeal to the Government to help in financing operations of these airports," he appealed.

He said poor infrastructure and outdated equipment were to blame for low volume of cargo and passenger planes.

But, the Minister of Infrastructure, Dr Shukuru Kawambwa noted that the Government would continue upgrading the country's airports.

The Minister called upon TAA and TCAA to be creative in their work and improve the sector.
 
mradi wa airport bagamoyo umekaa kiubinafsi...mpango wa awali tangu enzi mwandosya yupo mawasiliano ni kujenga airport mkuranga na eneo limeshatengwa ....mtu haoni hata aibu airport bagamoyo....,bandari mpya bagamoyo[wakati mtwara na tanga hazijaendelezwa na dar ...ipo karibu just 40 km apart]......na hivi anajenga kempski wami bagamoyo[for your infromation].....
nyumba zake msoga-makao makuu ya mkoa ,chalinze...just in five years ......he is so hurry........
nadhani ni vema mji wa bagamoyo uendelezwe uwe wa kitalii...pengine hata kama ni bandari ijengwe ya tourist cruise ships ambazo hatunufaiki nazo......lakini kupeleka kila kitu pale si sawa....aiport irudi mkuranga....na pesa ya kujenga bandari ...wajenge ndogo ya kitalii pale pesa inayobaki waboreshe natural harbour yetu ya mtwara ...kwa kuunganisha na reli ya tazara na barabara...na kuilink bandari ya tanga na musoma...
 
Nafikiri ni wazo zuri sana kujenga airport Bagamoyo. Statistics zinaonyesha Dar airport inaelemewa sana na traffic ya midege inayotua kila dakika. Hata ikipanuliwa hivi inavyotakiwa kupanuliwa bado haitaweza kuhimili. Tunahitaji specifically airport mpya bagamoyo kwa sababu ya urahisi wa bagamoyo road kuingia dar. Barabara ni pana sana, haina magari mengi hasa kutokea Tegeta-Mbezi Beach-Ali H Mwinyi hadi city centre; barabara iko idle kabisa, pana ya kutosha magari yanaenda full speed. Bandari pia itajengwa Bagamoyo kwa sababu hiyo hiyo ya urahisi wa barabara kuingia Dar. Mizigo mingi zaidi itashukia kule italetwa na magari fasta jijini. Yaani serikali hii ina mawazo endelevu mazuri sana.
 
Suala la Bagamoyo kupata upendeleo lilishawahi kujadiliwa hapa jamvini.
Kuna mada niliwahi kuileta hapa inakwenda kwajina "Bagamoyo ni Yamousoukro ya Tanzania" baadhi ya wachangiaji hawakunielewa vyema cha kushangaza leo wameanza kustuka.

Nyie mbona hamtaki kueleze ukweli

hivi vyote vingejengwa Moshi au Arusha ingeonekana its normal

wacha wajenge Bagamoyo wakimaliza wakajenge na ule mradi mkubwa zaidi kule Pemba

sioni tatizo liko wapi
 
Nyie mbona hamtaki kueleze ukweli

hivi vyote vingejengwa Moshi au Arusha ingeonekana its normal

wacha wajenge Bagamoyo wakimaliza wakajenge na ule mradi mkubwa zaidi kule Pemba

sioni tatizo liko wapi

.....bandari ijengwe arusha????>>>.....una lako jambo,...sisi tunaongea kama watanzania ....tunataka airport ijengwe kule kule ilikopangwa mwanzo MKURANGA...na bandari bagamoyo ijengwe ya kitalii[for cruise ships-kumbuka we dont have that facility here na watalii wanaokuja na meli hawatiii nanga kwenye container au bulk terminals wanahitaji special passengers terminal...hatuna !! ijengwe bagamoyo]....
tunataka bandari za Tanga NA mtwara ziimarishwe zaidi....badala ya kujenga bandari mpya ya mizigo bagamoyo....kwanza mtwara patakuwa na usafiri na umeme wa uhakika karibuni......nadhani hivyo sio vitongoji vya arusha wala moshi ni mikoa ya Tanzania...
 
Mkuu hii nchi inaendeshwa kisiasa sio kimaendeleo..tatizo tunalijua...ndo maana experts wetu wengi wa planning wapo busy na private busines au as consultants nchi za nje...wamechoka na huu upumbavu wa serikali yetu!! Tanga port na Mtwara would have been key! Inachosha!
 
mradi wa airport bagamoyo umekaa kiubinafsi...mpango wa awali tangu enzi mwandosya yupo mawasiliano ni kujenga airport mkuranga na eneo limeshatengwa ....mtu haoni hata aibu airport bagamoyo....,bandari mpya bagamoyo[wakati mtwara na tanga hazijaendelezwa na dar ...ipo karibu just 40 km apart]......na hivi anajenga kempski wami bagamoyo[for your infromation].....
nyumba zake msoga-makao makuu ya mkoa ,chalinze...just in five years ......he is so hurry........
nadhani ni vema mji wa bagamoyo uendelezwe uwe wa kitalii...pengine hata kama ni bandari ijengwe ya tourist cruise ships ambazo hatunufaiki nazo......lakini kupeleka kila kitu pale si sawa....aiport irudi mkuranga....na pesa ya kujenga bandari ...wajenge ndogo ya kitalii pale pesa inayobaki waboreshe natural harbour yetu ya mtwara ...kwa kuunganisha na reli ya tazara na barabara...na kuilink bandari ya tanga na musoma...

PM,

Umeeleza vizuri sana, tutakubishia kwa sababu tu tunataka kukubishia wakati ukweli unajulikana!

Kama ulivosema suala la New Airport, eneo kubwa sana lilishatengwa Mkuranga karibu na kijiji kimoja kinaitwa Marogoro lakini ghafla plan hiyo ikabadilika baada ya mkulu kuingia ikulu.......! Tusimung'unye maneno hapa; tumejiuliza sana suala na Bagamoyo na Mkulu hasa kwenye issues zifuatazo;
  • New big Airport Bagamoyo
  • Upanuzi wa barabara kutoka Chalinze hadi Segera kuwa njia mbili (tulishajadili sana hapa)
  • Ujenzi wa New Kempsnik pale Wami
  • Ujenzi wa ''kijiji'' cha Mkulu pale wami
  • Mradi wa ujenzi wa bandari bagamoyo
Je, haya yanafanyika kwa sababu ni plan ya nchi yafanyike hivyo au kwa sababu mkulu anatokea Bagamoyo? let's be honest hapa!
 
kaka philemon, binafsi umenizindua usingizini...... sikujua juu ya yote haya, huu ndio umuhimu wa JF. pamoja na hayo mengine mi nilidhani ule mradi wa airport mkuranga unaendelea.
 
.....bandari ijengwe arusha????>>>.....una lako jambo,...sisi tunaongea kama watanzania ....tunataka airport ijengwe kule kule ilikopangwa mwanzo MKURANGA...na bandari bagamoyo ijengwe ya kitalii[for cruise ships-kumbuka we dont have that facility here na watalii wanaokuja na meli hawatiii nanga kwenye container au bulk terminals wanahitaji special passengers terminal...hatuna !! ijengwe bagamoyo]....
tunataka bandari za Tanga NA mtwara ziimarishwe zaidi....badala ya kujenga bandari mpya ya mizigo bagamoyo....kwanza mtwara patakuwa na usafiri na umeme wa uhakika karibuni......nadhani hivyo sio vitongoji vya arusha wala moshi ni mikoa ya Tanzania...

hujawahi kusikia inland ports?
anyway it doesnt matter

HUko Bagamoyo wacha wajenge zote zinazohitajika kujengwa wakimaliza wakajenge vingine kule Pemba

mimi nadhani hata ule uwanja wa Taifa mpya umejengwa pale kimakosa

wangeenda kuujenga Kisarawe

Bandari ya Dar ilitakiwa ichukue the whole of Changombe including uwanja wa Taifa

enzi za kuthink small zilishapitwa na wakati
 
Nisingependa kuingia kwenye mjadala wa kimkoa wala kimajimbo lakini nataka kuliangalia hili kwa mtazamo wa kitaifa zaidi. Suala la Bandari na Airport ijengwe wapi linatakiwa liwe kwenye mipango ya muda mrefu ya nchi hasa kwa kuzingatia manufaa ya kiuchumi na kijamii ya miradi hiyo kwa nchi.

Kwa mtazamo wangu Tanzania inahitaji uwekezaji mkubwa kwenye upanuzi wa bandari ya Dar na uboreshaji wa huduma za garimoshi kwenye reli ya kati kutoka Dar mpaka Mwanza na Kigoma na Rwanda. Tunahitaji pia uwekezaji mkubwa kwenye bandari ya Kigoma na Mwanza South Port kwa mizigo inayoelekea DRC na Burundi. Lakini pia tunahitaji kuiimarisha reli ya Tazara ili iweze kuongeza uchukuzi wa mizigo inayokwenda kusini mwa Tanzania na nje ya nchi.

Kuhusu Airport sioni sababu ya kujenga airport bagamoyo kwa kuwa tayari kuna mkakati wa kupanua hii ya Dar es salaam, juhudi zingeelekezwa kwenye kuinua kiwango cha airports za Tabora na Kigoma ili kuzifanya ziweze kutoa huduma bora kwa mwaka mzima. Kwa sasa airport ya Tabora hufungwa wakati wa masika. Mtakumbuka hivi karibuni Precision Air walisimamisha safari kwenye mikoa hiyo kwa sababu ya ubora wa chini wa viwanja vya ndege. Airport ya mkuranga ni muhimu lakini inaweza kujengwa baadaye hasa pale uwezo wa airport ya Dar iliyopanuliwa utakapopungua.

Uwekezaji katika reli na bandari za magharibi na kusini mwa nchi ni muhimu kwa sababu utafungua soko kubwa sana kwa nchi za Rwanda, Burundi, DRC, Uganda, Malawi na Zambia ambazo zote hazina huduma ya uhakika za bandari na reli. Kwa kufungua milango hiyo siyo tu kwamba nchi yetu itanufaika kwa mapato, bali pia wananchi wa mikoa inayopitiwa na miundombinu hiyo watanufaika sana kwa biashara na shughuli nyingine za kiuchumi. Kama tukijipanga vizuri, Tanzania itakuwa ikitoa huduma kwa nchi sita za Afrika.

Naungana na mchangiaji aliyependekeza kuwa Bagamoyo pajengwe bandari ya kitalii hasa kwa kuzingatia historia ya sehemu husika. Lakini ukijenga bandari pale bila ya kuweka miundombinu ya reli haitasaidia sana uchumi wa nchi. Hizo barabara tunazodhani kuwa zinaweza kubeba mizigo toka Bagamoyo kuja Dar zitajaa malori makubwa na kutakuwa na msongamano zaidi ya huu wa Dar es salaam. Kama kweli wanajenga bandari pale Bagamoyo itabidi wafikirie kuweka reli kuunganisha bandari hiyo mpya na reli za kati na Tazara.
 
Umenena kuhusu priorities. Sioni umuhimu wowote wa kujenga airport mpya wakati hata hii iliyopo haina traffic ya kutosha wala kutisha. Ndege zinazotua kwenye International Airport si nyingi kiasi cha kuhitaji airport nyingine.

Aidha Bagamoyo ni mji wa kihistoria. Kwa mawazo yangu ni vyema ukahifadhiwa jinsi ulivyo ili kudumisha historia yake.
 
Kama walikuwa wanahiyo plan ya kujenga airport nyingine kwa ajili ya upanuzi mbona hizi nyumba za kipawa zinabomolewa??
Swali:
1. ubomoaji wa nyumba za kipawa ni waka ajili ya nn??
2. ni trafiki gani tunayo ya ndege zetu??
 
yote wafanye.bagamoyo wajenge kiwanja kidogo kwa ajili ya ndege dogo za ndani ambazo zitakuwa zinasafirisha watalii na watu wengine wa humu humu ndani ya nchi.
 
Kitu kimoja kinachowafungamanisha viongozi wengi wa kiafrika tangu enzi za uhuru[1960] mpaka wakati huu ni ubinafsi.Ukiwatazama viongozi kama Mabuto Kuku wazabanga wa Zaire sasa Congo,
Houphouet Boigny wa Ivory Coast na Daniel Arap Moi wa Kenya wote walitumia rasilimali za taifa kuneemesha sehemu walizotoka.Analofanya Jakaya Mrisho Kikwete bila shaka ni upuuzi waliokuwa wakifanya marais wa zamani niliowataja,ameshindwa kujifunza kwamba atakapo ondoka madarakani miradi yote anayoikimbiza Bagamoyo itakufa kama ilivyotokea Kenya na zaire baada ya Moi na Mobutu kuondoka madarakani.

Hii niliiandika 03/10/2009
Rais wa kwanza wa nchi ya Ivory Coast Marehemu Felix Houphouet Boigny aliufanya mji aliozaliwa wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa ivory Coast badala ya Abidjani.Zoezi la kuufanya mji wa Yamoussoukro kuwa mji mkuu wa Ivory Coast liliambata na matumizi makubwa ya fedha za nchi kuelekezwa Yamoussoukro kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na maofisi ya wizara mbali mbali ambayo tayari ilikuwepo Abidjani.Uwanja wa ndege,mabarabara makubwa,mahospital na lile kanisa kubwa [ Basilica of our lady of peace of Yomoussokro] lilijengwa kwa gharama ya U$ 300 million peke yake.

Rais Jakaya M Kikwete tangu alipochaguliwa kuingia madarakani mwaka 2005 kumekuwa na juhudi kubwa sana za kuuendeleza Mji Bagamoyo kwa kutumia kodi za wananchi au kutumia mikopo au misaada.Kuna mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa,kuna mpango wa kujenga bandari sijui kwanini tusijenge bandari kubwa Tanga au Lindi,kumekuwa na juhudi za chini chini za kujenga kituo cha mikutano cha kimataifa badala ya Arusha,Kumekuwa na juhudi za kujenga kijiji cha michezo badala ya ule mpango wa kukijenga sambamba na uwanja wa taifa Dar es salaam,ujenzi wa barabara nne kutokea Chalinze hadi Segera wakati barabara ipo tena tusisahau kuna sehemu nyingi Tanzania hazijawahi kuona barabara ya lami,ujenzi wa barabara msata hadi Bagamoyo.

Baba wa taifa Julius alikuwa Rais wa JMT kwa miaka 24 lakini hakuwahi kufikiria kuijenga Musoma / Butihama kwa kutumia rasilimali chache za nchi kama anavyofanya Muungwana katika kipindi kisichozidi miaka 4 tu.Najaribu kutafakari tukimpa tena miaka 5 mingine Bagamoyo itakuwaje ?.
 
Ngongo umenena! Tena nasikia Mwalimu Nyerere alikataa kijiji cha Butiama kufanywa Wilaya, alitaka kijiji hicho kibaki jinsi kilivyo ili kiweze ku-preserve historia. Hata kama kinapanuka yawe ni makazi ya kawaida tu ya wanakijiji na sio magorofa ya maofisi ya Wilaya n.k.

Wajukuu, Vitukuu na vilembwe wanayo haki ya kuachiwa sehemu hizo za kihistoria zibaki jinsi zilivyo ili na wao waweze kuja kuielewa vyema historia ya nchi yao kwa kuziona sehemu hizo. Kuanza kuvuruga historia, kuharibu mandhari kwa kujenga viwanja vya ndege kwenye maeneo ya kihistoria ni kutowatendea haki watoto na vijukuu vyetu kwa kuua historia ya taifa letu kwa ujumla.
 
_46852852_camara_ap.jpg

Shot Guinea strongman Camara 'flies to Morocco'

Guinea's military leader Capt Moussa Dadis Camara has been flown to Morocco for medical treatment after being shot by an aide on Thursday, officials say. They had earlier said that Capt Camara had only been lightly wounded in the attack and was in "good health". Separate reports say the international airport in the capital Conakry has been surrounded by presidential guards.

This is believed to be the first time Capt Camara has left the country since seizing power last December.
Analysts say he may fear a counter-coup in his absence and so his departure indicates that his condition may be serious. However, Communications Minister Idrissa Cherif said Capt Camara was "walking and talking and doing fine", the AP news agency reports. He told Reuters that the military leader had gone to Morocco for a check-up.

Capt Camara has not been seen in public or appeared on national TV or radio since the shooting.
A Senegalese medical team flew to Guinea to treat him on Thursday night. The whereabouts of Aboubacar "Toumba" Diakite, the officer allegedly behind the attack, is unclear. Mr Cherif had said he had been arrested after the shooting but reports on Friday say road-blocks have been set up in Conakry by security forces trying to find him.

Analysts say the shooting highlights deep rifts within the junta after the killing of an estimated 157 opposition supporters in September. BBC West Africa correspondent Caspar Leighton says the presence of the United Nation investigation team in Conakry this week has heightened concerns among some parts of the military that they may be singled out by the government to take the blame for the attack. Lt Diakite has been accused by witnesses and human rights groups of commanding the troops who carried out the massacre. Several women have reported being gang-raped by soldiers.
 
Huyu Shukuru na rafiki yake hawana soni. Ndege 20-30 zinaruka na kutua DIA kwa siku - uwanja mwingine wa nini? Halafu mara wanahamisha watu kipawa/ukonga ili wapanue uwanja, mara sasa wanateka Mradi wa Mkuranga na kuupeleka kwao Bagamoyo ... na hii ni kwa miaka 3 tu - je tutaona mangapi baada ya miaka 10 (in case)?
 
yote ni maendeleo lakini yaende kwa utaratibu wakunufaisha TZ yote. Vipi uwanja wa ndege Mbeya na ntwara...ingewekwa katika viwango vya kimataifa ili kukuza uchumi wa mikoa ya kusini. Ni vizuri tukapanua wigo wa vitega uchumi kuliko kulimbikiza vyote DAR , Arusha na sasa Bagamoyo
Dira ya nchi inategemea aliyeko madarakani au inakuwaje tena hapa wachumi na wataalamu mnaojua haya mambo ya mipango??/
 
hujawahi kusikia inland ports?
anyway it doesnt matter

HUko Bagamoyo wacha wajenge zote zinazohitajika kujengwa wakimaliza wakajenge vingine kule Pemba

mimi nadhani hata ule uwanja wa Taifa mpya umejengwa pale kimakosa

wangeenda kuujenga Kisarawe

Bandari ya Dar ilitakiwa ichukue the whole of Changombe including uwanja wa Taifa

enzi za kuthink small zilishapitwa na wakati
You right.sijui mpango mji haoni JKNA pamebana na ipo mjini mno.badala ya upanuzi wangejenga uwanja mkubwa mpya kisarawe,mkuranga au bagamoyo.
 
Back
Top Bottom