Bafana Bafana kuumana na Taifa Stars mei 14 taifa uwanja mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bafana Bafana kuumana na Taifa Stars mei 14 taifa uwanja mpya

Discussion in 'Sports' started by Songambele, Apr 28, 2011.

 1. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,018
  Trophy Points: 280
  Habari ambazo zimerushwa na supersport Blitz hivi punde ni kuwa Bafana bafana watacheza game ya kirafiki ya kimataifa na Taifa stars katika uwanja wa mpya mei 14 bongo.

  Hii ni habari njema kwa watu wa mpira uhsusani katika kipindi hiki ambapo mataifa yanatatafuta tiketi za kucheza fainali mwakani. Bafana bafana ni timu kubwa na wanauzoefu mkubwa katika mshindano ya kimataifa mwaka jana tu wametoka kuandaa kombe la dunia na wamechapa misri juzi kati tu. Hii ni platform kubwa kwa timu ya Taifa na wachezaji kuonyesha uwezo katika medani ya kimataifa.

  Kubwa kuliko ni nafasi nyingine kuimarisha uhusiano wetu na SA, manake watanzania huko kwao tumechafuka kutokana na harakati za kutafuta maisha, baadhi ya wabongo ni wapiga ndole maarufu Jberg na capetown, mbali na kuuza ndumu na unga pia ni watu wa michomoko sana (wavunja nyumba) pamoja na kushika bunduki (watu wa bunduki) na magumashi kibao. Ukitaka kuona hili katiza Beit Bridge (boarder ya zimbabwe) na pass ya kibongo uone mtiti wa askari wa kisauz watakavyo kupekua.

  Soka itarekebisha hizi kasoro kwa kuongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili ambazo zinasharikiana kibiashara na kuna fursa kibao kwa wabongo huko kwao.

  Binafsi nawapongeza waandaaji wa pambano hili kwa ubunifu huu wa aina yake.
   
Loading...