Bado WaTanzania wanaliwa na Simba

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Mwanafunzi aliwa na simba

2008-09-01 09:13:16
Na Futuna Selemani, Mkuranga

Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi, Mwanzega katika Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungumbweni wilayani Mkuranga, Ali Athmani Mbotoni (10), amefariki dunia baada ya kuliwa na simba.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Henry Orauya Clemens, alisema mwanafunzi huyo alikumbwa na mkasa huo, wiki iliyopita saa 12.00 jioni nyumbani kwao katika kijiji cha Mwanzega.

Bw. Clemens alisema alipewa taarifa hiyo na wazee wa kijiji hicho, mara bada ya kutokea kwa tukio hilo.

Alisema mtoto huyo alikumbwa na mkasa huo wakati akirejea nyumbani kwao kutoka dukani kununua vitu alivyotumwa na wazazi wake.

Mkuu huyo wa wilaya alisema aliwaagiza askari wa wanyama pori, ambao walikwenda eneo la tukio lakini giza lilikuwa limeshaingia hivyo walilazimika kusubiri hadi kesho yake ili kufanya msako katika pori lililopo kijijini hapo.

Alisema kuwa askari hao waliendesha msako na walifanikiwa kumuua simba huyo jike anayesadikiwa kuwa alikuwa na watoto wawili, ambao walikimbia.

Alisema fuvu la kichwa la mtoto huyo lilikutwa kichakani na mwili wake ukiwa umeliwa wote na mnyama huyo mkali.

``Juhudi za kuwasaka watoto hao wa simba zinaendelea,`` alisema Clemens na kutoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa taarifa mapema pindi wanapoona wanyama wakali kwenye maeneo yao.

SOURCE: Nipashe
Tumsaidieni waziri wa mali asili na Utalii ,hii ni aibu hadi leo bado kuna watu wanaliwa na wanyama pori tena ,kama huyu ni katoto kadogo ambako kalienda dukani kununua pipi.
 
..Mkuranga hapo. siyo mbali sana na capital city.

..kwa kweli inauma sana tena sana.

..sijui wazazi na ndugu zake wana hali gani.
 
Hapo Shungubweni ni noma niliwahi kuharibikiwa na gari usiku na simba walikuwa wanavinjari mitaa hii ilikuwa patashika nguo kuchanika.
 
Masatu,
Pole sana ndugu yangu. Hata sisi kule kwetu Mara katika miaka ya 50 hili tatizo lilikuwa sugu sana. Kilichotusaidia ni uwindaji. Simba walikuwa wakizurura hadi Mwibara kutoka Serengeti. Lakini waliuawa wengi sana mpaka ikabidi wajiwekee mipaka wasitoke nje ya Serengeti. Wawindaji wetu mashujaa waliwatafuta hao simba, hasa wale waliokwishaonja nyama ya mtu na kuwaua, na mpaka leo simba hathubutu kuvuka ile barabara ya Mwanza-Musoma.
 
Sasa tutawasaidia vipi wananchi wanaokumbwa na mambu haya,tuna jeshi ,tuna polisi,tuna sungusungu,tuna mgambu,tuna askari wanyama pori(Hawa ndio wa kulaumiwa)maana wanatakiwa wawe kwenye patroo kuzunguka eneo na kuweka mabango ambayo yatampatia mpita njia tahadhari na kuweza kupeleka jicho kila pembe mbali na karibu au hata kuweza kufananisha kichuguu na kichwa cha simba na kutimka zake mbio.
 
Italazimu mgambo au kikosi cha jeshi kipinge kambi kule. Ukishauwa simba wawili watatu wengine wataogopa kusogelea eneo hilo.
 
Hivi hakuna program za Idara na wizara husika na wanyama pori ku-monitor wanyama pori na wanavyoingia katika anga za Uraia?

Tusubiri mfadhili aje atusaidie katika hili nalo?
 
...hivi wale smba wala watu wa Tunduru walikomeshwa na nini miaka ilee...
 
Masatu,
Pole sana ndugu yangu. Hata sisi kule kwetu Mara katika miaka ya 50 hili tatizo lilikuwa sugu sana. Kilichotusaidia ni uwindaji. Simba walikuwa wakizurura hadi Mwibara kutoka Serengeti. Lakini waliuawa wengi sana mpaka ikabidi wajiwekee mipaka wasitoke nje ya Serengeti. Wawindaji wetu mashujaa waliwatafuta hao simba, hasa wale waliokwishaonja nyama ya mtu na kuwaua, na mpaka leo simba hathubutu kuvuka ile barabara ya Mwanza-Musoma.

Mimi nilikulia sehemu za Mwibara pale (kaka Mkandara upo hapo?) na kweli mwishoni mwa miaka ya 50 na mwanzoni mwa miaka ya 60 eneo lile lilikuwa na simba wengi sana pamoja na wanyama pori wengineo. Kuanzia maeneo ya Kasuguti hadi Kalukekele kelekea Nyantale na Guta ilikuwa ni skwea ya wanyama pori. Jina Nyantare limetokana kuwapo kwa simba wengi eneo hilo. Ninakumbuka kuwa tulikuwa tunasisitizwa kuhakikisha kuwa ifikapo usiku tuwe karibu na moto unaowaka kwa vile simba hasogelei moto, na kweli huenda hiyo ilisaidia kuokoa maisha yetu kwa vile eneo loter nililokulia hatukuwahi kusikia mtu kuliwa na simba.

Uwindaji ulipokolea sana mwanzoni mwa miaka ya 60 baada ya uhuru, wanyama wale walihama wenyewe. Leo hii ukienda sehemu hizo hukuti hata sungura. Sana sana utasikia fisi tu wakati wa usiku na mara moja moja utakutana na Mbweha.

Tatizo la watu wetu kuliwa na wanyama pori linatia aibu sana hasa ukizingatia kuwa tumekuwa huru kwa karibu nusu karne, na miaka yote hii tuna wizara ihusuyo wanyama pori. Wizara hiyo ingekuwa inafanya kazi zake sawasawa, ingekuwa imshedhibiti wanyama pori wasifike maeneo wanakosihi watu. Badala yake Wizara ina watu wanaofikiria kuanzisha makampuni yao ya kuwinda tu.
 
Back
Top Bottom