Bado tuna safari ndefu sana kupiga vita UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado tuna safari ndefu sana kupiga vita UKIMWI

Discussion in 'JF Doctor' started by TIMING, Nov 24, 2009.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu, naomba kuwasialisha hii mada;

  Pamoja na jitihada kubwa zinazoendelezwa na wadau mbalimbalia kwa mfano mashirika ya maendeleo ya kijamii, serikali, sisi wenyewe kama wananchi na kampeni nyingi tu za upimaji, ARVs nk.; Takwimu ambazo si rasmi (but reliable, confidentiality is observed here) zinaonnyesha kwamba hali ni tete zaidi kwenye makundi yafuatayo

  • Wanandoa - extra marital affairs zinaongezeka hasa kwenye miji mikubwa ambayo elimu ya ukimwi hutolewa zaidi
  • Wasanii - hasa wa bendi zetu
  • wanavyuo - ingawa hii haina data kubwa hasa kutokana na wengi wao kutokupima (bado wana afya nzuri
  What do we have to do??
  Je tuwe wakatili kwa wanaofahamika kuwa na ugonjwa na kuusambaza makusudi? tuwafanyeje waume au wake za watu wanaoongoza kwa kwenda nje

  Tuwasaidiaje wasanii na wanamichezo?

  Tusaidiaje kubadili tabia?
   
 2. M

  Matumaini Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mkuu MTM,heshima mbele!

  Mi nadhani watanzania tufanye kitu kinachoitwa "kupenda maisha". Kivipi? Hakuna mtu anayependa kufa lakini nadhani pamoja na elimu yote ya UKIMWI/VVU iliyotolewa bado Wa-tz tunachukulia mambo rahisi na kuwa UKIMWI/VVU ni ugonjwa wa mbali au ni ugonjwa wa watu wahuni na malaya..lakini takwimu hazionyeshi hivyo-watu tunaodhani ni wahuni/malaya m.f machangudoa wapo safe zaidi ya hayo makundi uliyotaja hapo juu m.f wanandoa na wanachuo.

  Pia Wa-tz wengi hatuna mipango endelevu ya maisha yetu, tunaishi tu, kwa hiyo tunakosa maana ya kweli ya maisha ambayo ingeweza kutufanya tufikiri mara mbili kabla ya kutenda ngono isiyo salama au kutokua waaminifu kwa wapenzi wetu.
  Elimu ipo ya kutosha, sidhani kama leo mtu akiulizwa UKIMWI/VVU ni nini atatoa macho au hatajua nini kinazungumziwa. Kinachokosekana ni watu kukosa kujua maana ya maisha yao na yanaelekea wapi.

  Swala la kupima limekua kama taarifa ya kifo...mtu anaogopa kupima kwa kua anawaza ndio mwisho wa maisha yake..lakini kama wewe una mpango wa kumaliza chuo na kupata kazi/kujiajiri na hujui afya yako.unapoteza muda. Sawasawa na mtu anayechukua mkopo benki bila kujua biashara gani atafanya!

  Mwisho kwa wale wanaoogopa kupima VVU/UKIMWI nawashauri wafanye hivyo kwa kuwa hakuna njia ya mkato, kama hujaoa-utapima kabla ya ndoa, kama umeoa-mkeo atapimwa akiwa mjamzito/clinic, kama umemaliza uzazi-dalili zikianza utapimwa tu! Kwa hiyo kama wasemavyo wazungu-"The early the better" Hima hima jamani tukapime na tuchukulie maisha yetu kimakini zaidi..."Life is what you make it"

  Nawasilisha
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Mkuu,

  nadhani tatizo kubwa kwetu ni jinsi ukimwi ulivyochukuliwa kama mradi kuliko serious issue... hasa katika mapambano.

  About a week ago nilikuwa katika kazi zetu nikapata bahati ya kuwa miongoni mwa wasanii wengi sana, kwakweli hali sio nzuri na nilipojaribu kuuliza chanzo, wengi waligusia kwamba wanaelewa kuna njia za kuepuka lakini nyingi haziaminiki kutokana na sisi wenyewe kuziwekea doubts...

  I think we need to change our strategies na kuweka ownership kwanza kuliko hali ya sasa ambao NGOs/CSOs zimeovershdow serikali kwenye mapambano
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Survey ya mwisho ya UNAIDS inaonyesha kwamba waTz wengi (near universal knowledge), lakini tatizo sio knowledge, tatizo ni mapokeo ya elimu kuhusu kubadili tabia

  with this i challenge akina mama ambao hasa ni nguzo za families kuongoza mapambano, akina baba tumelegalega
   
Loading...