Bado sijaona faida ya Elimu ya Tanzania hasa Chuo Kikuu na kidato cha sita

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Elimu ya Tanzania imetumika miaka mingi kumuandaa kijana kuajiriwa na Serikali au Sekta binafsi, Watu ambao wamepata bahati ya kuajiriwa na mfumo huu wa elimu wao wanaona mfumo huu upo sawa kabisa

Mambo yanayoshangaza na kusikitisha zaidi watu wale wale ambao wanaona mfumo upo sawa wa elimu yetu wanahangaika kuwatafutia kazi vijana na ndugu zao maofisini kwa udi na uvumba

Mfumo wa elimu yetu tumeurithi toka kwa mkoloni, Mkoloni alimpa mtu mweusi elimu kwa lengo la mtu mweusi kuja kumtumikia mkoloni, Elimu aliyoitoa mkoloni haikumuandaa mtu mweusi kufikiri nje ya anachofundishwa darasani


Tangu mwaka 2000 mpaka sasa mwaka 2021 maelfu ya vijana wamehitimu vyuo vikuu ndani ya nchi, Waliobahatika kuajiriwa ni chini ya asilimia moja ya wahitimu wote

Kijana anatumia miaka takribani kumi na saba kutafuta elimu toka shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu, Elimu ambayo nje ya cheti kijana hawezi kusimama na kujitetea

Tufanye kitu gani tutoke hapa tulipo na tusonge mbele kwa matumaini

Mosi, Watoto wetu wakishafanikiwa kujua kusoma na kuandika lugha yetu kwa ufasaha na lugha baadhi za kigeni, Wazazi pamoja na shule wawapime watoto wanahitaji wafanye kitu gani na wanapendelea kitu gani, Tuwaendeleze watoto kwa vitu wanavyohitaji na baadhi kama masomo ya teknolojia yawe ya lazima

Masomo ya lugha za computer yaani Coding yawe ni lazima kwenye elimu ya msingi, Masomo ya kutengeneza App yawe ni lazima hapa kwenye elimu ya msingi. Watoto wafundishwe matatizo tulionayo na jinsi watavyoweza kuyatatua kwa teknolojia

Miaka mitano inatosha kwa elimu ya msingi kwa watoto wetu kuweza kuelewa Basics au msingi wa wapi tunalipeleka Taifa hili

Pili, Hakuna haja ya vijana kusoma masomo zaidi ya kumi Katika ngazi ya kati ya Sekondari yaani Kidato Cha kwanza mpaka nne, Kidato Cha kwanza mpaka nne kiwe ni kipindi cha vijana kufundishwa mahesabu na teknolojia, Masomo ya Kompyuta kwa vitendo na Matumizi ya mahesabu kwa vitendo ndio muda wake hapa

Nafahamu hatuna walimu wenye uwezo wa vitendo na wala hatuna maabara za kuwaandaa hawa vijana, Lakini ni muda muafaka kuanza na shule chache na kuingia gharama za kuazima walimu toka China na Marekani


Tatu, Watoto wakitoka Kidato Cha nne waelekee vyuo vya kati vya kisasa sio hizi Amazoni College au University of Iringa au University of Dodoma au Sua au Udsm( Hivi ni vyuo ambavyo watoto wanaandaliwa kukariri mambo ili wafaulu tu mitihani na kutafuta ajira)

Elimu za vyuo kama Udsm, Sua, Udom na rafiki zao kama IFM na CBE vilishafeli kitambo sana kwa kutoa elimu za kukariri

Vyuo vya kati ndio ambavyo ilipasa pesa za IMF za corona na baadhi ya mikopo kuelekeza kununua mitambo ya kisasa ya computer na Machine za high Tech kwa ajili ya vijana kujifunza

Nne, Urafiki wetu na Mabeberu ulenge kutujengea uwezo na tuwatumie mabeberu vizuri, Pesa za Loan Board zitumike kuwapeleka vijana Field huko Google, Amazon, NASA, Microsoft. Na baadhi wapelekwe kwenye mazoezi huko London School of Economics wakajifunze, Harvad School of Medicine.

Ni muda wa kukaa chini na Balozi wa Marekani na China kuongea nao kuhusu mpango wa vijana wetu kila mwaka zaidi ya Mia tano kwenda kujifunza mazoezi kwenye taasisi zao za teknolojia za kati na kubwa ili tuhamishie uwezo wa teknolojia Nyumbani

Tano, Kundi la vijana wapenda masomo ya historia na Sanaa lipewe kipaumbele kidogo tofauti na sasa, Vyuo vyetu wamejaa vijana wa masomo ya uchekeshaji na uigizaji, Uigizaji Katika sociology, Political science, Fine art na watoto wao wanaolingana

Sita, Walimu wetu wa vyuo vikuu hawana uwezo wa kumuandaa kijana tena kujitegemea, Walimu tulionao sasa ni zao la watu waliokariri mambo kwa muda mrefu sana

Ni muda tupate walimu wa vitendo, Hawa walimu wa nadharia wa kuandaa notes na kutunga Test hawatufai tena hapa Tanzania

Serikali iwaondoe walimu wasiokuwa na umuhimu vyuo vikuu hasa wale ambao hana uwezo wa vitendo, Waletwe wataalamu toka China na Marekani kupima uwezo wa hawa walimu wetu Katika kila sekta toka Engineering, Accounting mpaka kozi za usanii


Nje ya Cheti cha darasani, Vijana waliomaliza chuo kikuu kwa sasa hawawezi kusimama, Ukimpokonya cheti chake ukamuuliza Haya sasa simama songa mbele lazima atadondoka tu

Tujiulize maswali muhimu kwa lengo la kusaidia hawa vijana wetu

Je kijana anapomaliza chuo kikuu mfano udsm au udom, Sua. Tukichukua cheti chake atafanya kitu gani huku uraiani, Walimu wa vyuo vikuu hawana uwezo kuwaandaa vijana tena kwa sasa

Je kila kijana neno kujiajiri ni kuuza nguo, maandazi, Nyanya, Mikate, mitumba na kuanzisha duka kariakoo?

Hitimisho
Tuna watu ambao wamesoma na wamepata taaluma ya vitendo kwa juhudi zao na ujanja wao, Ni muda wa kuwatumia hawa watu, Kuna watu wanafanya kazi Serikalini na Sekta binafsi wana uwezo mkubwa kwa vitendo kuliko hawa walimu waliopo vyuo vikuu kwa sasa,

Ni kuboresha mazingira tu na kuwa ondoa walimu wote ambao hawana uwezo kufundisha kwa vitendo

Mazingira yakiboreshwa hata mimi Gussie Nipo tayari kwenda Front line kugawa mbinu za kupambana kwa wanafunzi wetu kisiasa na hata kukabiliana na Biashara za kimataifa na kuachana na hawa wabunge wa kujua kusoma na kuandika tu

Tusipowaza matumbo yetu na Mamlaka tunaweza jenga Taifa imara kwa watoto na Vizazi vijavyo
 
Ukimaliz chuo 3 years umetumia mil 06 tu y serikali... Wakt hela ya ada ipo Kam namba tu udsm hailipwi na bodi! Hii million sita kwend China kujifunza elim yao Ni ndoto ngum sbab kuanzia nauli na makazi ya miez 3 hela kwisha. Nan atakugharmia 3 years!? Ni heri tungeitoa watto wakawekeze kwenye kilimo huku warsha mbalimbali zikiwaboresha
 
Umeongea ukweli mtupu

Ila Serikali haijaamua ku invest kwenye Elimu

Maana Elimu kwa vitendo inahitaji mavifaa na makolokolo mengi ambayo serikali naona haijaamua kufanya hivyo

Kama tu hii Elimu ya sasa hata madarasa hayatoshi je hiyo unayoisema inayohitaji space itakuaje
 
Umeongea ukweli mtupu

Ila serikali haijaamua ku invest kwenye Elimu

Maana Elimu kwa vitendo inahitaji mavifaa na makolokolo mengi ambayo serikali naona haijaamua kufanya hivyo

Kama tu hii Elimu ya sasa hata madarasa hayatoshi je hiyo unayoisema inayohitaji space itakuaje
Sisi tuliokuw matakon mwa dunia huku tusbirien kufa tu manke kila mipango kwa akil zetu itakuw hadithi tu
 
Mawazo ya kijinga kabisaa!
Mambo ya msingi ni kujadili Bernard Morrison amefuga ndevu

Mambo ya msingi ni kujadili Manara ameachana na Mke wake

Mambo ya msingi ni kujadili Mo Dewji ndio kila kitu Simba


Mambo ya msingi ni kujadili Mbona Rais Samia amevaa Gwanda la JWTZ


Mambo ya msingi ni kujadili Rais Kikwete ana miwani nzuri


Kwa mawazo kama haya tutafika tu
 
Umeanza vizuri ila mwisho unataka tupige goti kwa mabeberu wa ukoloni maomboleo watwambie nini hatima ya vijana wetu, aibu gani hii kama siyo fedheha! Rudisheni tawala za kichifu na abakama, muone kama vijana watakosa ajira. Rudisheni jando na unyago, muone kama kuna kijana atakosa elimu sahihi kwa mazingira yake. Unaposema kompyuta liwe somo la lazima, unasahau kwamba dunia ya sasa inaendeshwa na automation chini ya mfumo wa A.I(Artificial Intelligence). Nimalize kwa kusema mwanadamu haitaji elimu ya mfumo rasmi ili aishi, ila mfumo rasmi ndo unamwitaji mwanadamu ili uendelee kuwepo. Tukiua mfumo rasmi wa kielimu tutakuwa tumejikomboa katika nyanja zote kimaisha.
 
Sjaona connection ya title na content..so watu wasiende vyuo sasa..kisa tu elimu inamuandaa mtu kuajiriwa....huhuhu
Mfano, Unaenda chuo kikuu miaka mitatu kusomea How Africa were colonilized by British Halafu wanaongezea kozi ndogo ndogo ishirini inaitwa BA in History and Political Science
 
Umeanza vizuri ila mwisho unataka tupige goti kwa mabeberu wa ukoloni maomboleo watwambie nini hatima ya vijana wetu, aibu gani hii kama siyo fedheha! Rudisheni tawala za kichifu na abakama, muone kama vijana watakosa ajira. Rudisheni jando na unyago, muone kama kuna kijana atakosa elimu sahihi kwa mazingira yake. Unaposema kompyuta liwe somo la lazima, unasahau kwamba dunia ya sasa inaendeshwa na automation chini mfumo wa A.I(Artificial Intelligence). Nimalize kwa kusema mwanadamu haitaji elimu ya mfumo rasmi ili aishi, ila mfumo rasmi ndo unamwitaji mwanadamu ili uendelee kuwepo. Tukiua mfumo rasmi wa kielimu tutakuwa tumejikomboa katika nyanya zote.
Chanjo ya Corona tu Africa tupo Chali

Leo kuna kirusi kipya Omicron cha korona
 
Chanjo ya Corona tu Africa tupo Chali

Leo kuna kirusi kipya Omicron cha korona
Herd immunity iliyo gunduliwa na serikali ya Magufuli na Nkurunziza,mliikataa mkaja na ile ya kutestiwa mitambo, usiku, ya mabeberu na hayo ndiyo matokeo yake, apandae uvuna apandacho.
 
Kosa kubwa ambalo serikali inaendelea kulifanya ni ku-promote umachinga na kuhalalisha kuwa ajira kwa vijana wetu!

Ukweli ni kuwa hivi sasa serikali inapaswa kupitia upya sera yetu ya elimu kwa kuanzisha shule na vyuo vingi vya technical badala ya hivi vya academic ambavyo kwa sasa vinaongeza utegemezi na umaskini!
 
1.Mimi naomba nitofautiane mtazamo kitu wasichokijua watu wengi ni kwamba wanafikiri elimu unayofundishwa au ya huko ughaibuni inamfundisha mtu kujiajiri au kuvumbua kitu..

2. Swala la kujiajiri au kuvumbua kitu ni suala la mtu binafsi na udadisi wa mtu huyo husika shuleni ama darasani haufundishwi wala nini ni wewe mwenyewe binafsi kuona changamoto inayokuzunguka na kuitafutia suluhisho ndo maana anaekufundisha wewe kujiajiri yeye mwenyewe ameajiriwa
 
Herd immunity iliyo gunduliwa na serikali ya Magufuli na Nkurunziza,mliikataa mkaja na ile ya kutestiwa mitambo, usiku, ya mabeberu na hayo ndiyo matokeo yake, apandae uvuna apandacho.
Wote wameshatangulia
 
Umeanza vizuri ila mwisho unataka tupige goti kwa mabeberu wa ukoloni maomboleo watwambie nini hatima ya vijana wetu, aibu gani hii kama siyo fedheha! Rudisheni tawala za kichifu na abakama, muone kama vijana watakosa ajira. Rudisheni jando na unyago, muone kama kuna kijana atakosa elimu sahihi kwa mazingira yake. Unaposema kompyuta liwe somo la lazima, unasahau kwamba dunia ya sasa inaendeshwa na automation chini ya mfumo wa A.I(Artificial Intelligence). Nimalize kwa kusema mwanadamu haitaji elimu ya mfumo rasmi ili aishi, ila mfumo rasmi ndo unamwitaji mwanadamu ili uendelee kuwepo. Tukiua mfumo rasmi wa kielimu tutakuwa tumejikomboa katika nyanya zote.
Hayo unayosema yalishabihiana na civilization ya kale. Civilization ya sasa imetengenezwa kwa mfumo rasmi wa elimu: shughuli za ujenzi, viwanda, kilimo, mwingiliano mkubwa wa watu n.k; vyote haviwezi kwenda bila mfumo rasmi wa elimu.

Hayo unayosema yanawezekana endapo tutarudi nyuma kule kwenye mtindo wa kale wa maisha, mfumo rahisi wa kuishi kila jamii sehemu yake tu na kwa ajili ya kula na kunywa tu kama wale watu wa asili wa misitu ya Amazon na wahadzabe wa hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom