Bado sijaona faida ya Elimu ya Tanzania hasa Chuo Kikuu na kidato cha sita

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,298
2,000
1.Mimi naomba nitofautiane mtazamo kitu wasichokijua watu wengi ni kwamba wanafikiri elimu unayofundishwa au ya huko ughaibuni inamfundisha mtu kujiajiri au kuvumbua kitu..

2. Swala la kujiajiri au kuvumbua kitu ni suala la mtu binafsi na udadisi wa mtu huyo husika shuleni ama darasani haufundishwi wala nini ni wewe mwenyewe binafsi kuona changamoto inayokuzunguka na kuitafutia suluhisho ndo maana anaekufundisha wewe kujiajiri yeye mwenyewe ameajiriwa
Mtoa mada hajasema watu wasome wavumbue bali waweze kutenda mambo pasi na cheti kwa kuzingatia mazingira ya sasa.
Hata ulaya sio wote wanaovumbua ila vwengi wanaweza tendea waliosomea japo nao mfumo wao wamekuwa wakiuona kama umepitwa na wakati.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,298
2,000
Ukweli ni kwamba viongizi wengi hawana mbinu za kuleta mtaala wa kisasa wa vijana kujikomboa, hawana!
Hata hao watunga sera ni mabo@##s waliokusanya vyeti hawana jipya!
Kama mtu yeye binafsi kishindwa kubuni mambo yake yanayoonekana kwenye jamii atakutungia nini cha maana cha kukusaidia.
Watunga sera na mitaala kazi yao ni copy paste hawajawahi umiza vichwa na kuja na vitu tofauti.
Kazi wanayoijua ni kukopi tu vitu vya mataifa mengine.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,298
2,000
Jamaa umeandika mapupu tulioyazoea. Kunanyuzi zaidi ya elfu sabini mia nane humu, zote zinazungumzia ukurutu huu.
Kama wewe ni zao la elimu duni utaona nini zaidi ya mapupu?
Wewe na akili yako unaona sawa kabisa watu maelfu kusoma digrii za kiswahili,historia,sosholojia,saikolojia, na wachache kusoma biashara, sayansi teknolojia na kilimo.
Unasoma historia ili ukaifanyie nini mtaani ?
Hapo ulipo ukipigwa chini kwenye hio kazi waliobuni wanaume wenzio utabaki kulia lia.
Kuna watu kuanzisha na kubuni mambo yenu hamuwezi waacheni wanaoweza kubuni mambo katika mtazamo mpya halafu nyie muwe wafuata mkumbo kama mnavyofuata mkumbo katika mfumo uliopo ulionzishwa na wengine.
Kwa taarifa yako serikali yenyewe inamoango wa kuubadili huu mtaaka unaoushabikia sasa sijui utajinyonga.
We jamaa umeletwa hapa dunia kufuata upepo?
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
4,044
2,000
Elimu ya Tanzania imetumika miaka mingi kumuandaa kijana kuajiriwa na Serikali au Sekta binafsi, Watu ambao wamepata bahati ya kuajiriwa na mfumo huu wa elimu wao wanaona mfumo huu upo sawa kabisa

Mambo yanayoshangaza na kusikitisha zaidi watu wale wale ambao wanaona mfumo upo sawa wa elimu yetu wanahangaika kuwatafutia kazi vijana na ndugu zao maofisini kwa udi na uvumba

Mfumo wa elimu yetu tumeurithi toka kwa mkoloni, Mkoloni alimpa mtu mweusi elimu kwa lengo la mtu mweusi kuja kumtumikia mkoloni, Elimu aliyoitoa mkoloni haikumuandaa mtu mweusi kufikiri nje ya anachofundishwa darasani

Tangu mwaka 2000 mpaka sasa mwaka 2021 maelfu ya vijana wamehitimu vyuo vikuu ndani ya nchi, Waliobahatika kuajiriwa ni chini ya asilimia moja ya wahitimu wote

Kijana anatumia miaka takribani kumi na saba kutafuta elimu toka shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu, Elimu ambayo nje ya cheti kijana hawezi kusimama na kujitetea

Tufanye kitu gani tutoke hapa tulipo na tusonge mbele kwa matumaini

Mosi, Watoto wetu wakishafanikiwa kujua kusoma na kuandika lugha yetu kwa ufasaha na lugha baadhi za kigeni, Wazazi pamoja na shule wawapime watoto wanahitaji wafanye kitu gani na wanapendelea kitu gani, Tuwaendeleze watoto kwa vitu wanavyohitaji na baadhi kama masomo ya teknolojia yawe ya lazima

Masomo ya lugha za computer yaani Coding yawe ni lazima kwenye elimu ya msingi, Masomo ya kutengeneza App yawe ni lazima hapa kwenye elimu ya msingi. Watoto wafundishwe matatizo tulionayo na jinsi watavyoweza kuyatatua kwa teknolojia

Miaka mitano inatosha kwa elimu ya msingi kwa watoto wetu kuweza kuelewa Basics au msingi wa wapi tunalipeleka Taifa hili

Pili, Hakuna haja ya vijana kusoma masomo zaidi ya kumi Katika ngazi ya kati ya Sekondari yaani Kidato Cha kwanza mpaka nne, Kidato Cha kwanza mpaka nne kiwe ni kipindi cha vijana kufundishwa mahesabu na teknolojia, Masomo ya Kompyuta kwa vitendo na Matumizi ya mahesabu kwa vitendo ndio muda wake hapa

Nafahamu hatuna walimu wenye uwezo wa vitendo na wala hatuna maabara za kuwaandaa hawa vijana, Lakini ni muda muafaka kuanza na shule chache na kuingia gharama za kuazima walimu toka China na Marekani

Tatu, Watoto wakitoka Kidato Cha nne waelekee vyuo vya kati vya kisasa sio hizi Amazoni College au University of Iringa au University of Dodoma au Sua au Udsm( Hivi ni vyuo ambavyo watoto wanaandaliwa kukariri mambo ili wafaulu tu mitihani na kutafuta ajira)

Elimu za vyuo kama Udsm, Sua, Udom na rafiki zao kama IFM na CBE vilishafeli kitambo sana kwa kutoa elimu za kukariri

Vyuo vya kati ndio ambavyo ilipasa pesa za IMF za corona na baadhi ya mikopo kuelekeza kununua mitambo ya kisasa ya computer na Machine za high Tech kwa ajili ya vijana kujifunza

Nne, Urafiki wetu na Mabeberu ulenge kutujengea uwezo na tuwatumie mabeberu vizuri, Pesa za Loan Board zitumike kuwapeleka vijana Field huko Google, Amazon, NASA, Microsoft. Na baadhi wapelekwe kwenye mazoezi huko London School of Economics wakajifunze, Harvad School of Medicine.

Ni muda wa kukaa chini na Balozi wa Marekani na China kuongea nao kuhusu mpango wa vijana wetu kila mwaka zaidi ya Mia tano kwenda kujifunza mazoezi kwenye taasisi zao za teknolojia za kati na kubwa ili tuhamishie uwezo wa teknolojia Nyumbani

Tano, Kundi la vijana wapenda masomo ya historia na Sanaa lipewe kipaumbele kidogo tofauti na sasa, Vyuo vyetu wamejaa vijana wa masomo ya uchekeshaji na uigizaji, Uigizaji Katika sociology, Political science, Fine art na watoto wao wanaolingana

Sita, Walimu wetu wa vyuo vikuu hawana uwezo wa kumuandaa kijana tena kujitegemea, Walimu tulionao sasa ni zao la watu waliokariri mambo kwa muda mrefu sana

Ni muda tupate walimu wa vitendo, Hawa walimu wa nadharia wa kuandaa notes na kutunga Test hawatufai tena hapa Tanzania

Serikali iwaondoe walimu wasiokuwa na umuhimu vyuo vikuu hasa wale ambao hana uwezo wa vitendo, Waletwe wataalamu toka China na Marekani kupima uwezo wa hawa walimu wetu Katika kila sekta toka Engineering, Accounting mpaka kozi za usanii

Nje ya Cheti cha darasani, Vijana waliomaliza chuo kikuu kwa sasa hawawezi kusimama, Ukimpokonya cheti chake ukamuuliza Haya sasa simama songa mbele lazima atadondoka tu

Tujiulize maswali muhimu kwa lengo la kusaidia hawa vijana wetu

Je kijana anapomaliza chuo kikuu mfano udsm au udom, Sua. Tukichukua cheti chake atafanya kitu gani huku uraiani, Walimu wa vyuo vikuu hawana uwezo kuwaandaa vijana tena kwa sasa

Je kila kijana neno kujiajiri ni kuuza nguo, maandazi, Nyanya, Mikate, mitumba na kuanzisha duka kariakoo?

Hitimisho
Tuna watu ambao wamesoma na wamepata taaluma ya vitendo kwa juhudi zao na ujanja wao, Ni muda wa kuwatumia hawa watu, Kuna watu wanafanya kazi Serikalini na Sekta binafsi wana uwezo mkubwa kwa vitendo kuliko hawa walimu waliopo vyuo vikuu kwa sasa,

Ni kuboresha mazingira tu na kuwa ondoa walimu wote ambao hawana uwezo kufundisha kwa vitendo

Mazingira yakiboreshwa hata mimi Gussie Nipo tayari kwenda Front line kugawa mbinu za kupambana kwa wanafunzi wetu kisiasa na hata kukabiliana na Biashara za kimataifa na kuachana na hawa wabunge wa kujua kusoma na kuandika tu

Tusipowaza matumbo yetu na Mamlaka tunaweza jenga Taifa imara kwa watoto na Vizazi vijavyo
Kwa uzoefu wangu wa kusoma vyuo vya ufundi,na kufanya kazi,ni vzr waalimu wa vyuo vikuu,Kama DIT,lectureres,wawe wamewahi kufsnya kazi kwa hicho wanachokifundisha.
Nilipokuwa chuo,nilifundishwa PLC(programmable logic controller),lakini sikupewa ufahamu mkubwa kwamba hii PLC ipo kwenye vifaa vingi.kuanzia kwenye radio,tv,cm,zama za kilimo,magenereta nk.
Kuna umuhimu wanaowaandaa Hawa vijana huko vyuoni wasiwe ma academicians tu na ma gpa makubwa ya kukalili.inabidi wawe na uzoefu wa kufsnya kazi.
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,713
2,000
Mtoa mada hajasema watu wasome wavumbue bali waweze kutenda mambo pasi na cheti kwa kuzingatia mazingira ya sasa.
Hata ulaya sio wote wanaovumbua ila vwengi wanaweza tendea waliosomea japo nao mfumo wao wamekuwa wakiuona kama umepitwa na wakati.
Sasa kufanya mambo nje ya cheti si ndo kile kile tu kutumia udadisi wako wa kufanya vitu kwa kuangalia gap katika jamii yako either unacho cheti au hauna cheti ama mkuu haujaelewa point?
 
Master Arcade

JF-Expert Member
Apr 21, 2021
242
500
Elimu ya Tanzania imetumika miaka mingi kumuandaa kijana kuajiriwa na Serikali au Sekta binafsi, Watu ambao wamepata bahati ya kuajiriwa na mfumo huu wa elimu wao wanaona mfumo huu upo sawa kabisa

Mambo yanayoshangaza na kusikitisha zaidi watu wale wale ambao wanaona mfumo upo sawa wa elimu yetu wanahangaika kuwatafutia kazi vijana na ndugu zao maofisini kwa udi na uvumba

Mfumo wa elimu yetu tumeurithi toka kwa mkoloni, Mkoloni alimpa mtu mweusi elimu kwa lengo la mtu mweusi kuja kumtumikia mkoloni, Elimu aliyoitoa mkoloni haikumuandaa mtu mweusi kufikiri nje ya anachofundishwa darasani

Tangu mwaka 2000 mpaka sasa mwaka 2021 maelfu ya vijana wamehitimu vyuo vikuu ndani ya nchi, Waliobahatika kuajiriwa ni chini ya asilimia moja ya wahitimu wote

Kijana anatumia miaka takribani kumi na saba kutafuta elimu toka shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu, Elimu ambayo nje ya cheti kijana hawezi kusimama na kujitetea

Tufanye kitu gani tutoke hapa tulipo na tusonge mbele kwa matumaini

Mosi, Watoto wetu wakishafanikiwa kujua kusoma na kuandika lugha yetu kwa ufasaha na lugha baadhi za kigeni, Wazazi pamoja na shule wawapime watoto wanahitaji wafanye kitu gani na wanapendelea kitu gani, Tuwaendeleze watoto kwa vitu wanavyohitaji na baadhi kama masomo ya teknolojia yawe ya lazima

Masomo ya lugha za computer yaani Coding yawe ni lazima kwenye elimu ya msingi, Masomo ya kutengeneza App yawe ni lazima hapa kwenye elimu ya msingi. Watoto wafundishwe matatizo tulionayo na jinsi watavyoweza kuyatatua kwa teknolojia

Miaka mitano inatosha kwa elimu ya msingi kwa watoto wetu kuweza kuelewa Basics au msingi wa wapi tunalipeleka Taifa hili

Pili, Hakuna haja ya vijana kusoma masomo zaidi ya kumi Katika ngazi ya kati ya Sekondari yaani Kidato Cha kwanza mpaka nne, Kidato Cha kwanza mpaka nne kiwe ni kipindi cha vijana kufundishwa mahesabu na teknolojia, Masomo ya Kompyuta kwa vitendo na Matumizi ya mahesabu kwa vitendo ndio muda wake hapa

Nafahamu hatuna walimu wenye uwezo wa vitendo na wala hatuna maabara za kuwaandaa hawa vijana, Lakini ni muda muafaka kuanza na shule chache na kuingia gharama za kuazima walimu toka China na Marekani

Tatu, Watoto wakitoka Kidato Cha nne waelekee vyuo vya kati vya kisasa sio hizi Amazoni College au University of Iringa au University of Dodoma au Sua au Udsm( Hivi ni vyuo ambavyo watoto wanaandaliwa kukariri mambo ili wafaulu tu mitihani na kutafuta ajira)

Elimu za vyuo kama Udsm, Sua, Udom na rafiki zao kama IFM na CBE vilishafeli kitambo sana kwa kutoa elimu za kukariri

Vyuo vya kati ndio ambavyo ilipasa pesa za IMF za corona na baadhi ya mikopo kuelekeza kununua mitambo ya kisasa ya computer na Machine za high Tech kwa ajili ya vijana kujifunza

Nne, Urafiki wetu na Mabeberu ulenge kutujengea uwezo na tuwatumie mabeberu vizuri, Pesa za Loan Board zitumike kuwapeleka vijana Field huko Google, Amazon, NASA, Microsoft. Na baadhi wapelekwe kwenye mazoezi huko London School of Economics wakajifunze, Harvad School of Medicine.

Ni muda wa kukaa chini na Balozi wa Marekani na China kuongea nao kuhusu mpango wa vijana wetu kila mwaka zaidi ya Mia tano kwenda kujifunza mazoezi kwenye taasisi zao za teknolojia za kati na kubwa ili tuhamishie uwezo wa teknolojia Nyumbani

Tano, Kundi la vijana wapenda masomo ya historia na Sanaa lipewe kipaumbele kidogo tofauti na sasa, Vyuo vyetu wamejaa vijana wa masomo ya uchekeshaji na uigizaji, Uigizaji Katika sociology, Political science, Fine art na watoto wao wanaolingana

Sita, Walimu wetu wa vyuo vikuu hawana uwezo wa kumuandaa kijana tena kujitegemea, Walimu tulionao sasa ni zao la watu waliokariri mambo kwa muda mrefu sana

Ni muda tupate walimu wa vitendo, Hawa walimu wa nadharia wa kuandaa notes na kutunga Test hawatufai tena hapa Tanzania

Serikali iwaondoe walimu wasiokuwa na umuhimu vyuo vikuu hasa wale ambao hana uwezo wa vitendo, Waletwe wataalamu toka China na Marekani kupima uwezo wa hawa walimu wetu Katika kila sekta toka Engineering, Accounting mpaka kozi za usanii

Nje ya Cheti cha darasani, Vijana waliomaliza chuo kikuu kwa sasa hawawezi kusimama, Ukimpokonya cheti chake ukamuuliza Haya sasa simama songa mbele lazima atadondoka tu

Tujiulize maswali muhimu kwa lengo la kusaidia hawa vijana wetu

Je kijana anapomaliza chuo kikuu mfano udsm au udom, Sua. Tukichukua cheti chake atafanya kitu gani huku uraiani, Walimu wa vyuo vikuu hawana uwezo kuwaandaa vijana tena kwa sasa

Je kila kijana neno kujiajiri ni kuuza nguo, maandazi, Nyanya, Mikate, mitumba na kuanzisha duka kariakoo?

Hitimisho
Tuna watu ambao wamesoma na wamepata taaluma ya vitendo kwa juhudi zao na ujanja wao, Ni muda wa kuwatumia hawa watu, Kuna watu wanafanya kazi Serikalini na Sekta binafsi wana uwezo mkubwa kwa vitendo kuliko hawa walimu waliopo vyuo vikuu kwa sasa,

Ni kuboresha mazingira tu na kuwa ondoa walimu wote ambao hawana uwezo kufundisha kwa vitendo

Mazingira yakiboreshwa hata mimi Gussie Nipo tayari kwenda Front line kugawa mbinu za kupambana kwa wanafunzi wetu kisiasa na hata kukabiliana na Biashara za kimataifa na kuachana na hawa wabunge wa kujua kusoma na kuandika tu

Tusipowaza matumbo yetu na Mamlaka tunaweza jenga Taifa imara kwa watoto na Vizazi vijavyo
Elimu yetu haina shida kabisa
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,298
2,000
Elimu yetu haina shida kabisa
Ina shida sana tu. Wewe sijui upo peponi?
Wahitimu wangapi wa drs 7 wanaweza kutumua macrisoft office applcation?
Kama wanauwezo wameupata wapi ilihali shule hazina vifaa hivyo vya kujifunzia kwa vitendo?
Kama hako kaeneo kamoja hawana uwezo wewe toa mfano wa huo uwezo walionao wahitimu wa drs7.
Hapo Sijaongelea masomo mengine.
 
Master Arcade

JF-Expert Member
Apr 21, 2021
242
500
Ina shida sana tu. Wewe sijui upo peponi?
Wahitimu wangapi wa drs 7 wanaweza kutumua macrisoft office applcation?
Kama wanauwezo wameupata wapi ilihali shule hazina vifaa hivyo vya kujifunzia kwa vitendo?
Kama hako kaeneo kamoja hawana uwezo wewe toa mfano wa huo uwezo walionao wahitimu wa drs7.
Hapo Sijaongelea masomo mengine.
Kwa hilo ulilotaja hapo si kosa la mfumo wa elimu bali ni kosa la kutokuwa na vifaa vya kutosha katika shule zetu.
 
Sep 11, 2019
8
45
Sjaona connection ya title na content..so watu wasiende vyuo sasa..kisa tu elimu inamuandaa mtu kuajiriwa....huhuhu
Jamaa kaongea facts tupu, unakaza tum kichwa kumuelewa .. kikubwa ni serikali kuwekeza katika elimu kama kweli tunahitaji maendeleo kwa kizazi kijacho, huu ni muda sasa wa kufanya mabadiliko katika mfumo mzima wa elimu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom